Wanawake - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 02 Jan 2024 21:33:13 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Wanawake - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kesi ya aliyepigwa busu yanguruma mahakamani https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/aliyepigwa-busu-ajenga-hoja-mahakamani/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/aliyepigwa-busu-ajenga-hoja-mahakamani/#respond Tue, 02 Jan 2024 19:44:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9119 Madrid, HispaniaMchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso ameiambia mahakama kuwa busu la mdomoni alilopigwa na aliyekuwa bosi wa soka Hispania, Luis Rubiales halikuwa na ridhaa yake.Mara baada ya timu ya wanawake ya Hispania kuibwaga England na kubeba Kombe la Dunia, Rubiales aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania alimkumbatia kwa nguvu Jenni […]

The post Kesi ya aliyepigwa busu yanguruma mahakamani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso ameiambia mahakama kuwa busu la mdomoni alilopigwa na aliyekuwa bosi wa soka Hispania, Luis Rubiales halikuwa na ridhaa yake.
Mara baada ya timu ya wanawake ya Hispania kuibwaga England na kubeba Kombe la Dunia, Rubiales aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania alimkumbatia kwa nguvu Jenni na kumpiga busu la mdomoni.
Kitendo hicho kilizua taharuki na kusababisha Rubiales kusimamishwa na Fifa kujihusisha na soka kwa siku 90 kabla ya kuamua kung’atuka nafasi yake katika shirikisho la soka Hispania lakini Jenni aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.
Baada ya mahakama hiyo ya mjini Madrid kuelezwa hivyo na Jenni leo Jumanne, sasa ni jukumu la Jaji kuamua kama Rubiales atashitakiwa kwa kosa la udhalilishaji kijinsia au la.
Jenni, 33, ambaye ni mfungaji kinara wa mabao wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania aliieleza mahakama tukio zima kwa zaidi ya saa moja na vyombo vya habari vilidai kwamba katika hoja zake alisema kuwa busu alilopigwa hakulitarajia na hakukuwa na makubaliano yoyote.
Rubiales kwa upande wake ameshikilia msimamo wake akikana kufanya kosa lolote wakati mahakama imeamua kuendelea na uchunguzi ikiwamo kutumia kamera za CCTV ili kupata ushahidi zaidi wa tukio hilo kabla ya kutoa uamuzi.
Tukio la Jenni kupigwa busu lilitokea Agosti mwaka jana mjini Sydney, Australia mara baada ya mechi ya fainali wakati wachezaji wa Hispania waliobeba taji hilo wakipita jukwaani kuvalishwa medali zao ndipo Rubiales alimpokumbatia Jenni na kumpiga busu la mdomoni.

The post Kesi ya aliyepigwa busu yanguruma mahakamani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/aliyepigwa-busu-ajenga-hoja-mahakamani/feed/ 0
Tanzanite kuivaa Nigeria kwa tahadhari https://www.greensports.co.tz/2023/11/18/tanzanite-kuivaa-nigeria-kwa-tahadhari/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/18/tanzanite-kuivaa-nigeria-kwa-tahadhari/#respond Sat, 18 Nov 2023 07:00:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8504 Na mwandishi wetuKocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite Queens’, Bakari Shime amesema katika mchezo wao dhidi ya Nigeria wataingia kwa tahadhari kubwa kutokana na mbinu nyingi walizonazo wapinzani wao hao.Timu hizo zitaumana kesho Jumapili kwenye mechi ya marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia baada ya mechi […]

The post Tanzanite kuivaa Nigeria kwa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite Queens’, Bakari Shime amesema katika mchezo wao dhidi ya Nigeria wataingia kwa tahadhari kubwa kutokana na mbinu nyingi walizonazo wapinzani wao hao.
Timu hizo zitaumana kesho Jumapili kwenye mechi ya marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia baada ya mechi ya awali iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Shime alisema hayo Ijumaa hii saa chache kabla ya kuanza mazoezi ya mwisho ya timu hiyo akibainisha kuwa yawezekana Nigeria kuna mbinu zao walizificha, hawakuzitumia kwenye mchezo uliopita, hivyo wanachukua tahadhari juu ya hilo.

“Ni mazoezi ya mwisho ya kutengeneza mipango yetu ya mwisho hapa ugenini, tukiamini tunacheza na timu imara, ngumu na inawezekana walificha baadhi ya vitu tulipokuwa nyumbani na wanaweza kuvionesha hapa kwao, hivyo tunaingia kwa tahadhari kubwa kuhakikisha tunajipanga vizuri kujilinda na kutafuta bao ili tupate faida katika mechi hii,” alisema Shime.


Katika mechi hiyo Tanzanite inahitaji ushindi ili kusonga hatua inayofuata kuelekea michuano hiyo itakayofanyika Colombia, mwakani.
Tanzanite ilitinga hatua hiyo na kukutana na Nigeria baada ya kuifumua Djibouti kwa ushindi wa jumla wa mabao 12-0 baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zilizopigwa Azam Complex.

The post Tanzanite kuivaa Nigeria kwa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/18/tanzanite-kuivaa-nigeria-kwa-tahadhari/feed/ 0
Aliyembusu mchezaji ‘jela’ miaka mitatu https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/aliyembusu-mchezaji-jela-miaka-mitatu/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/aliyembusu-mchezaji-jela-miaka-mitatu/#respond Wed, 01 Nov 2023 05:30:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8302 Madrid, HispaniaAliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amefungiwa na Fifa kujihusisha na mambo yote yanayohusu soka kwa miaka mitatu kwa kosa la kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya Hispania, Jenni Hermoso.Rubiales alimpiga busu mchezaji huyo Agosti 20 mara baada ya Hispania kuibwaga England katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia […]

The post Aliyembusu mchezaji ‘jela’ miaka mitatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amefungiwa na Fifa kujihusisha na mambo yote yanayohusu soka kwa miaka mitatu kwa kosa la kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales alimpiga busu mchezaji huyo Agosti 20 mara baada ya Hispania kuibwaga England katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) na kubeba taji hilo.
Jenni ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Hispania baadaye alisema hakukuwa na makubaliano yoyote kati yake na Rubiales katika jambo hilo.
Busu hilo liligeuka mjadala mkubwa duniani kote hali iliyomfanya Rubiales mwezi Septemba atangaze kujizulu nafasi ya urais kwenye Shirikisho la Soka Hispania licha ya awali kudai kwamba hangekuwa tayari kuchukua uamuzi huo kwa kuwa haoni kosa alilolifanya.
Jumatatu hii Fifa ilitangaza adhabu ya kumfungia Rubiales miaka mitatu kwa kwenda kinyume na ibara ya 13 ya kanuni za nidhamu za Fifa ingawa ametangaza nia ya kukata rufaa.
“Nitakwenda katika hatua ya mwisho ili kuona haki inapatikana na ukweli unadhihirika,” alisema Rubiales kupitia mitandao ya kijamii.
Awali Fifa ilimsimamisha Rubiales kwa siku 90 kujihusisha na soka na kuahidi kulifanyia uchunguzi tukio zima la kumpiga busu mchezaji huyo ambalo pia limelalamikiwa na viongozi wa kiserikali nchini Hispania.
Rubiales pia amefikishwa mahakamani mjini Madrid kwa kosa la udhalilishaji kijinsia na ukatili na iwapo mahakama itamkuta na hatia katika kosa hilo huenda akakumbana na rungu la dola.

The post Aliyembusu mchezaji ‘jela’ miaka mitatu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/aliyembusu-mchezaji-jela-miaka-mitatu/feed/ 0
Busu lililozua taharuki https://www.greensports.co.tz/2023/09/24/busu-lililozua-taharuki/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/24/busu-lililozua-taharuki/#respond Sun, 24 Sep 2023 11:53:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7843 Na Hassan KinguUshindi wa timu ya wanawake ya Hispania kwenye Kombe la Dunia umeibua mjadala wa nje ya soka baada ya mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso kupigwa busu mdomoni na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales.Dunia ya soka ilipumzishwa kufurahia na kujadili ubingwa wa timu ya wanawake ya Hispania, ubingwa uliopatikana […]

The post Busu lililozua taharuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Ushindi wa timu ya wanawake ya Hispania kwenye Kombe la Dunia umeibua mjadala wa nje ya soka baada ya mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso kupigwa busu mdomoni na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales.
Dunia ya soka ilipumzishwa kufurahia na kujadili ubingwa wa timu ya wanawake ya Hispania, ubingwa uliopatikana Agosti 20, badala yake mjadala mkali uliozua taharuki ukawa ni kuhusu Luis kumpiga busu Jenni.
Ni kama ilivyokuwa mwaka 2006, timu ya wanaume ya Italia ilipobeba Kombe la Dunia, mjadala wa ushindi ulipoozeshwa na tukio la beki wa Italia, Marco Materrazi kupigwa kichwa na kiungo wa Ufaransa, Zinedine Zidane.
Tofauti ya mijadala hiyo ni kwamba Zidane au Zizou alijutia alichokifanya lakini Luis hakujutia, licha ya kusakamwa na kutakiwa ajiuzulu badala yake alisema kwamba furaha iliyopitiliza ndiyo iliyomfanya ampige Jenni busu la mdomoni.
Busu hilo likazua taharuki na kuibua shinikizo kila kona la kumtaka Luis ajiuzulu kwa kumpiga busu mwanamke ambaye huenda wapo wanaume wengine wengi waliotamani kufanya hivyo lakini hawajawahi kuipata nafasi ambayo Luis aliipata na Luis mwenyewe amegoma kujiuzulu huku hoja yake ikisimamia katika makubaliano baina yake na Jenni kwamba hakumpiga busu Jenni kwa lazima, walikubaliana.
Mjadala ukashika kasi, mashinikizo ya kumtaka Luis ajiuzulu yakaongezeka siku hadi siku, kuanzia kwa Waziri Mkuu wa Hispania, mawaziri, wanasoka wanawake na makundi mbalimbali ya wanaharakati.
Yote hayo hayakumshtua Luis, aliendelea kushikilia msimamo wa kutokuwa tayari kujiuzulu kabla ya Fifa kuingilia kati na kumsimamisha kujihusisha na masuala ya soka kwa siku 90.


Ikafuatua ofisi ya mwendesha mashtaka kutangaza kusudio la kumshitaki wakati huo huo, Jenni naye alishatangaza nia yake ya kufanya hivyo kwa alichokidai kwamba hakupenda alichofanyiwa na Luis.
Baada ya mashinikizo kuongezeka nje ya Hispania wakiwamo wachezaji wanawake kugoma kuichezea timu ya taifa kama Luis angeendelea kuwa madarakani, hatimaye Luis akakubali yaishe, akatangaza kujiuzulu.
Kujiuzulu kwa Luis hakujazuia mjadala kuendelea, bado watu wanahoji je ni kweli Luis alifanya kosa au tatizo limekuzwa bila sababu?
Watetezi wa Luis
Wanaomtetea Luis wanadai kwamba alichokifanya kilikuwa na ridhaa ya Jenni na wanatumia moja ya picha za tukio hilo kutetea hoja yao, picha inayotajwa ni ile inayoonesha mkono wa kulia wa Jenni ukimshika Luis kiunoni.
Katika picha hiyo kinachoonekana kimetafsiriwa kuwa ni Jenni kumpa ushirikiano Luis, kwa maana nyingine hakuwa na tatizo kwa alichofanyiwa na Luis.


Watetezi hao pia wanaona kama Jenni ameangukia katika shinikizo la watu ambao hawakupenda kile kilichofanywa na Luis na kwamba awali hakuliona jambo hilo kuwa ni lenye ubaya.
Hapa inajengwa hoja kwamba Luis alifurahia baada ya Hispania kubeba kombe la dunia, akafurahishwa na soka la Jenni, akaona kumkumbatia haitoshi bali busu lingeonesha alivyokuwa na furaha, na Jenni picha zinamuonesha akimpa Luis ushirikiano.
Zaidi ya yote hayo hakuna picha ya Jenni iliyomuonesha akiwa amekunja uso baada ya kupigwa busu la mdomoni hivyo hakuwa na tatizo na jambo hilo.
Mama wa Luis amekuwa mstari wa mbele kumtetea mwanaye ikiwamo kufanya mgomo wa kula na hoja yake ni moja tu kwamba mwanaye hakuwa na kosa kwani tukio zima lilifanyika kwa makubaliano baina ya Luis na Jenni.
Wanaompinga Luis
Wanaompinga Luis wanakataa kuwapo makubaliano baina yake na Jenni badala yake wanaliona tukio zima kama ni unyanyasaji na udhalilishaji mwanamke lililofanywa na kiongozi wa soka na suluhisho lake ni kumuondoa kiongozi huyo madarakani.
Hoja nyingine ya kundi hili pia inahusisha picha ile inayomuonesha Jenni akiwa ameiondoa mikono yake kwenye kiuno cha Luis, ni kama vile kwanza kukubali kukumbatiwa lakini hapo hapo kulikataa busu la mdomoni.
Kundi hili linamuweka Luis katika kundi la wanaume wanaodhalilisha wanawake na kuwakosea heshima kwa kutumia nafasi zao, ni kundi ambalo pia limekuwa likishinikiza mabadiliko ya kiungozi katika idara mbalimbali za Shirikisho la Soka Hispania.


Luis pamoja na kukubali kujiuzulu uongozi katika Shirikisho la Soka Hispania, bado ana kesi ya kujibu baada ya kushitakiwa na vyombo vya kisheria nchini Hispania.
Tumejifunza nini?
Tukio zima hili linatufundisha kuwa kuna mambo ambayo mtu hufanyiwa kwa ridhaa yake, tofauti na hivyo ni kesi kubwa. Tumefundishwa kuheshimu mipaka kati ya mwanamke na mwanaume.
Awali wengi wetu hatukutarajia kuona dunia ya soka ikijadili busu ambalo kiongozi wa soka ameamua kumpiga mchezaji wake tena baada ya kuvutiwa na soka la mchezaji huyo kwenye timu ambayo imebeba taji la dunia.

The post Busu lililozua taharuki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/24/busu-lililozua-taharuki/feed/ 0
Hatimaye aliyembusu mchezaji ajiuzulu https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/hatimaye-aliyembusu-mchezaji-ajiuzulu/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/hatimaye-aliyembusu-mchezaji-ajiuzulu/#respond Tue, 12 Sep 2023 16:36:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7734 Madrid, HispaniaRais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales (pichani) hatimaye amejiuzulu nafasi yake baada ya kuandamwa na tukio la kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.Rubiales aliyembusu Jenni Agosti 20 baada ya Hispania kuibwaga England bao 1-0 na kubeba taji la dunia, awali alitangaza kutokuwa tayari kujiuzulu akisisitiza hajafanya […]

The post Hatimaye aliyembusu mchezaji ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales (pichani) hatimaye amejiuzulu nafasi yake baada ya kuandamwa na tukio la kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales aliyembusu Jenni Agosti 20 baada ya Hispania kuibwaga England bao 1-0 na kubeba taji la dunia, awali alitangaza kutokuwa tayari kujiuzulu akisisitiza hajafanya jambo lolote baya, aliwasilisha barua ya kujiuzulu Jumatatu hii kwa rais wa muda wa REEF, Pedro Rocha.
Mbali na kujiuzulu REEF, Rubiales pia ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya makamu rais wa Umoja vya Vyama vya Soka Ulaya (Uefa)
Kujiuzulu kwa Rubiales huenda kukapunguza shutuma zilizokuwa zikielekezwa kwake kutoka makundi mbalimbali yaliyomtaka ajiuzulu wakiwamo wachezaji wa timu ya wanawake Hispania waliotangaza kutoichezea timu hiyo kama Rubiales angeendelea kukalia kiti cha REEF.
Wakati Rubiales akichukua uamuzi wa kujiuzulu, Jenni, 33, ameshalifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria akisisitiza kwamba hakukuwa na makubaliano ya yeye kupigwa busu mdomoni.


Katika madai yake ya awali, Rubiales, 46, alisisitiza kwamba hawezi kujiuzulu na kwamba kulikuwa na makubaliano baina yake na Jenni ingawa Fifa walimsimamisha kwa siku 90 na kutangaza kuanza uchunguzi wa tukio hilo.
“Baada ya kusimamishwa haraka kulikofanywa na Fifa pamoja na kufunguliwa mashtaka dhidi yangu, ni dhahiri kwamba siwezi kurudi katika nafasi yangu,” alisema Rubiales.
“Kusisitiza kusubiri na kushikilia msimamo hakutachangia jambo lolote chanya kwa shirikisho la soka Hispania au soka la Hispania,” alisema Rubiales kuutetea uamuzi wake wa kujiuzulu.
“Nina imani katika ukweli na nitafanya kila liwezekanalo kwa uwezo wangu ukweli uwekwe wazi,” alisema Rubiales.
“Wanangu (wa kike) watu wa familia yangu na watu wanaonipenda wameumizwa na matokeo ya adhabu ninayopewa pamoja na kuwapo kwa uwongo mwingi lakini pia upo ukweli kwamba mitaani siku hadi siku ukweli umeendelea kujiweka wazi,” alisema Rubiales.

“Baba yangu, wanangu, hao nimezungumza nao, wanajua hapa si tena suala langu, na baadhi ya marafiki wa karibu wameniambia, Luis ni lazima uangalie hadhi yako na kuendelea na maisha yako kwa sababu tofauti na hivyo utawaumiza watu unaowapenda na mchezo unaoupenda,” alisema Rubiales.


“Hili si suala langu peke yangu, misimamo yangu inaweza kuwaumiza watu wengine ambao ni muhimu, ni jambo la busara kwa uamuzi niliouchukua,” alisema Rubiales.

The post Hatimaye aliyembusu mchezaji ajiuzulu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/hatimaye-aliyembusu-mchezaji-ajiuzulu/feed/ 0
Aliyepigwa busu amshitaki aliyempiga busu https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/aliyepigwa-busu-amshitaki-aliyempiga-busu/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/aliyepigwa-busu-amshitaki-aliyempiga-busu/#respond Thu, 07 Sep 2023 06:25:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7675 Madrid, HispaniaMshambuliaji wa timu ya soka ya wanawake Hispania, Jenni Hermoso (pichani) aliyepigwa busu mdomoni na rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales, amemfikisha kiongozi huyo mahakamani.Rubiales alimpiga Jenni busu la mdomoni Agosti 20 baada ya Hispania kuichapa England bao 1-0 na kuibuka kinara wa Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) na tayari […]

The post Aliyepigwa busu amshitaki aliyempiga busu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mshambuliaji wa timu ya soka ya wanawake Hispania, Jenni Hermoso (pichani) aliyepigwa busu mdomoni na rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales, amemfikisha kiongozi huyo mahakamani.
Rubiales alimpiga Jenni busu la mdomoni Agosti 20 baada ya Hispania kuichapa England bao 1-0 na kuibuka kinara wa Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) na tayari Fifa imemsimamisha kiongozi huyo kujihusisha na soka kwa siku 90.
Kitendo cha Rubiales kimekemewa na makundi mbalimbali akitakiwa ajiuzulu lakini amegoma akidai kwamba alichokifanya kilitokana na furaha isiyo kifani baada ya kubeba taji la dunia na kulikuwa na makubaliano katika jambo hilo.
Taarifa ya waendesha mashitaka nchini Hispania ilidai kuwa, Jenni amemfikisha mahakamani Rubiales mwenye umri wa miaka 46 kwa kosa ambalo wengi wanalifahamu.
Awali ofisi ya waendesha mashitaka nchini Hispania ilizungumzia uwezekano wa kumfungulia kesi Rubiales baada ya kauli ya Jenni aliposema kwamba hakukuwa na makubaliano kati yake na Rubiales katika jambo hilo na kutaka taratibu za kisheria ziangaliwe.
Jenni mwenye umri wa miaka 33, inadaiwa aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani Jumanne hii uamuzi ambao unamuweka kiongozi huyo katika wakati mgumu ingawa mwenyewe ameonekana kujiamini akidai kwamba hajafanya kosa lolote.
Wachezaji 81 wa timu ya wanawake Hispania wakiwamo 23 walioiwakilisha timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia, wamegoma kuichezea timu hiyo kama Rubiales ataendelea kuwa kiongozi REEF.

Timu ya wanawake Hispania inatarajia kucheza mechi za Uefa Nations Ligi dhidi ya Sweden na Switzerland, mechi zitakazochezwa Septemba 22 na 26 mwaka huu.
Mechi hizo mbili zinabaki kuwa swali gumu kuhusu hatma ya mgomo huo baada ya Rubiales kusisitiza kwamba hawezi kujiuzulu kwa kuwa hajafanya kosa lolote.
REEF tayari imemtimua kocha mkuu wa timu ya wanawake Hispania, Jorge Vilda aliyeiwezesha timu hiyo kubeba taji la dunia na nafasi yake kuchukuliwa na Montse Tome.
Vilda anatajwa kuwa mshirika wa karibu wa Rubiales na hata baada ya jopo zima la benchi lake la ufundi la timu ya Hispania kujiuzulu kwa kushinikiza Rubiales ajiuzulu, Vilda aligoma kufanya hivyo na kubaki peke yake katika nafasi hiyo.

The post Aliyepigwa busu amshitaki aliyempiga busu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/07/aliyepigwa-busu-amshitaki-aliyempiga-busu/feed/ 0
Xavi amfariji aliyepigwa busu mdomoni https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/xavi-amfariji-aliyepigwa-busu-mdomoni/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/xavi-amfariji-aliyepigwa-busu-mdomoni/#respond Sat, 02 Sep 2023 20:01:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7646 Barcelona, HispaniaKocha wa Barca, Xavi Hernandez amemfariji mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso aliyepigwa busu mdomoni na rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF) aliyesimamishwa, Luis Rubiales.Xavi pia amemshutumu Rubiales kwa kitendo hicho ambacho kimemuweka katika wakati mgumu kiongozi huyo na kujikuta akishutumiwa kila kona duniani akitakiwa ajiuzulu katika nafasi yake REEF.Akiwa […]

The post Xavi amfariji aliyepigwa busu mdomoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Kocha wa Barca, Xavi Hernandez amemfariji mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Jenni Hermoso aliyepigwa busu mdomoni na rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF) aliyesimamishwa, Luis Rubiales.
Xavi pia amemshutumu Rubiales kwa kitendo hicho ambacho kimemuweka katika wakati mgumu kiongozi huyo na kujikuta akishutumiwa kila kona duniani akitakiwa ajiuzulu katika nafasi yake REEF.
Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni, Xavi alieleza kuchukizwa kwake na kitendo alichofanya Rubiales na kusisitiza kwamba yuko pamoja na Jenni katika kadhia iliyomkuta.
“Nataka niwatangazie kwamba ninatoa ushirikiano usio na mipaka kwa Jennifer Hermoso na wachezaji wengine,” alisema Xavi kabla ya kuanza mkutano na waandishi wa habari.

“Namlaumu rais wa Shirikisho la Soka Hispania kwa tabia aliyoionesha na nasikitika kwamba kwa sasa watu hawazungumzii tena mafanikio ya kihistoria ya timu kubeba Kombe la Dunia,” alisema Xavi.


Agosti 20 mwaka huu, Rubiales alimpiga Jenni busu ‘zito’ la mdomoni wakati wa shamrashamra za kufurahia ushindi wa timu ya wanawake ya Hispania iliyobeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC) baada ya kuilaza England bao 1-0.
Baadaye, Jenni, 33, alisema kwamba kitendo alichofanyiwa na Rubiales hakikubaliki na hakukuwa na makubaliano baina yao ingawa awali alinukuliwa akimtetea kiongozi huyo akisema kwamba furaha iliyopitiliza ndiyo iliyomfanya ampige busu la mdomoni.
Fifa imemsimamisha Rubiales kwa siku 90 kujihusisha na masuala ya soka na imeanza uchunguzi wa tukio hilo huku kiongozi huyo akitakiwa na makundi mbalimbali ajiuzulu ingawa mwenyewe amesema hayuko tayari kufanya hivyo.
Wakati huo huo mama mzazi wa Rubiales, Angeles Bejar ambaye alianza mgomo wa kula, ametoka hospitali alipolazwa baada ya hali yake kuwa mbaya kutokana na mgomo huo wa kushinikiza mwanaye asibughudhiwe kwa alichokifanya kwa kuwa kulikuwa na makubaliano.

The post Xavi amfariji aliyepigwa busu mdomoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/02/xavi-amfariji-aliyepigwa-busu-mdomoni/feed/ 0
Mama wa aliyembusu mchezaji alazwa hospitali https://www.greensports.co.tz/2023/08/31/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-alazwa-hospitali/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/31/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-alazwa-hospitali/#respond Thu, 31 Aug 2023 07:37:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7612 Madrid, HispaniaAngeles Bejar ambaye ni mama wa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF) aliyesimamishwa, Luis Rubiales amekimbizwa hospitali akiwa hoi baada ya kuwa katika mgomo wa kula akishinikiza mwanaye asibughudhiwe.Mama huyo alichukua uamuzi wa kugoma kula tangu Jumatatu na kujihifadhi kanisani akifanya maombi kwa alichodai kuwa mwanaye amekuwa akisakamwa kwa madai ya kumbusu mdomoni […]

The post Mama wa aliyembusu mchezaji alazwa hospitali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Angeles Bejar ambaye ni mama wa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF) aliyesimamishwa, Luis Rubiales amekimbizwa hospitali akiwa hoi baada ya kuwa katika mgomo wa kula akishinikiza mwanaye asibughudhiwe.
Mama huyo alichukua uamuzi wa kugoma kula tangu Jumatatu na kujihifadhi kanisani akifanya maombi kwa alichodai kuwa mwanaye amekuwa akisakamwa kwa madai ya kumbusu mdomoni mshambuliaji wa timu ya Hispania, Jenni Hermoso.
Rubiales amejikuta akishutumiwa na kushinikizwa ajiuzulu kwa kumbusu mdomoni Jenni wakati wa shamrashamra za timu ya Hispania kubeba Kombe la Dunia baada ya timu hiyo kuichapa England bao 1-0 katika mechi ya fainali.
Katika tukio hilo lililotokea Agosti 20, awali Jenni (pichani chini) alidaiwa kumtetea Rubiales lakini baadaye alisema kwamba hakupenda alichofanyiwa na kiongozi huyo kwani hakuwa ameridhia kufanyiwa hivyo.

Akiwa kanisani mama Angeles aliahidi kuendelea na mgomo wa kula usiku na mchana bila ukomo lakini jana Jumatano hali yake ilikuwa mbaya na kulazimika kuwahishwa hospitali na hivyo kusimamisha mgomo wa kula kwa muda.

“Unyama na mashambulizi ambayo anafanyiwa mwanangu ni jambo ambalo hapaswi kukutana nalo,” alisema mama huyo.


“Amepelekwa hospitali na kulazimika kusimamisha mgomo wa kula, amekuwa si mwenye kujisikia vizuri kutokana na joto na matatizo mengineyo, miguu yake imelegea na amekuwa katika uchovu,” alisema mchungaji mmoja wa kanisa hilo aliyetajwa kwa jina moja la Antonio.
Jumamosi iliyopita, Rubiales alisimamishwa kwa siku 90 na Fifa wakati uchunguzi wa kadhia inayomkabili ukiendelea wakati baadhi ya viongozi wa soka Hispania wakimshinikiza ajiuzulu.
Wachezaji 81 wa timu ya wanawake wa Hispania wametangaza kutokuwa tayari kuichezea timu hiyo kama Rubiales ataendelea kuwa kiongozi wa REEF.
Rubiales awali alijitetea akisema kwamba alichokifanya kilitokana na furaha isiyo kifani na kutaka wenye mtazamo tofauti na tukio hilo wapuuzwe ingawa baadaye aliomba radhi lakini amekataa kujiuzulu akidai kwamba hakumbusu Jenni kwa kumlazimisha.

The post Mama wa aliyembusu mchezaji alazwa hospitali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/31/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-alazwa-hospitali/feed/ 0
Kocha wa Wanawake Hispania njia panda https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kocha-wa-wanawake-hispania-njia-panda/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kocha-wa-wanawake-hispania-njia-panda/#respond Wed, 30 Aug 2023 07:45:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7569 Madrid, HispaniaHatma ya kocha wa wanawake wa timu ya Hispania, Jorge Vilda (pichani juu) huenda akatimuliwa baada ya kuwapo habari kwamba Shirikisho la Soka Hispania (REEF) linaangalia uwezekano wa kuchukua uamuzi huo.Vilda aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia, ni mtu pekee kwenye benchi la ufundi la timu hiyo aliyebaki katika nafasi yake baada ya […]

The post Kocha wa Wanawake Hispania njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Hatma ya kocha wa wanawake wa timu ya Hispania, Jorge Vilda (pichani juu) huenda akatimuliwa baada ya kuwapo habari kwamba Shirikisho la Soka Hispania (REEF) linaangalia uwezekano wa kuchukua uamuzi huo.
Vilda aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia, ni mtu pekee kwenye benchi la ufundi la timu hiyo aliyebaki katika nafasi yake baada ya wasaidizi wake wote kujiuzulu wakishinikiza kujiuzulu kwa Rais wa REEF, Luis Rubiales aliyembusu mshambuliaji wa timu hiyo, Jenni Hermoso.
Wachezaji 81 wa Hispania wakiwamo 23 walioiwezesha timu hiyo kubeba Kombe la Dunia wameahidi kutoichezea timu hiyo tena kama Rubiales ataendelea kuwa kwenye nafasi ya urais wa shirikisho hilo ingawa tayari Fifa imemsimamisha Rubiales kwa siku 90.
Vilda alionekana kwenye mkutano mkuu maalum wa REEF akimpongeza Rubiales kwa msimamo wake wa kutojiuzulu lakini baadaye alibadili msimamo na kuanza kukosoa alichokifanya Rubiales.
Mabosi ndani ya REEF wanaamini kwamba mwenendo mzima wa tukio hilo unatosha kuwa sababu ya kumtimua Vilda katika nafasi yake.


Jumatatu iliyopita, viongozi REEF walifanya mkutano mkuu maalum ulioongozwa na kaimu rais wa shirikisho hilo, Pedro Rocha na kujadili mpango wa kulifanyia maboresho shirikisho hilo kwa lengo la kuwa na mwanzo mpya.
Habari za ndani zinadai kwamba baadhi ya wajumbe wa mkutano huo hawataki kumshinikiza Rubiales ajiuzulu kwa lazima badala yake walitoa taarifa kama ya kumshauri achukua uamuzi huo jambo ambalo hadi sasa Rubiales hajakubaliana nalo.
Rubiales, 46, amejikuta akishutumiwa kila kona kwa kitendo chake cha kumbusu mdomoni Jenni baada ya Hispania kuichapa England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia.
Baadaye Rubiales alisema kwamba alimpiga busu mchezaji huyo baada ya kuwa na furaha isiyo kifani na kutaka wenye tafsiri tofauti wapuuzwe lakini amejikuta akisakamwa sehemu mbalimbali duniani na alichofanya kutafsiriwa kuwa ni udhalilishaji wa kijinsia.

The post Kocha wa Wanawake Hispania njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/30/kocha-wa-wanawake-hispania-njia-panda/feed/ 0
Mama wa aliyembusu mchezaji mdomoni agoma kula https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-agoma-kula/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-agoma-kula/#respond Mon, 28 Aug 2023 19:31:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7561 Madrid, HispaniaÁngeles Bejar ambaye ni mama wa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales aliyesimamishwa kwa kosa la kumbusu mshambuliaji wa timu ya wanawake, amejifungia peke yake kanisani kwa alichokiita kuwa ni mgomo wa kula kupinga madhila anayopitia mtoto wake.Mmoja wa wanafamilia ya Rubiales alithibitisha Jumatatu hii kuwa mama huyo amechukua uamuzi huo […]

The post Mama wa aliyembusu mchezaji mdomoni agoma kula first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Ángeles Bejar ambaye ni mama wa rais wa Shirikisho la Soka Hispania (REEF), Luis Rubiales aliyesimamishwa kwa kosa la kumbusu mshambuliaji wa timu ya wanawake, amejifungia peke yake kanisani kwa alichokiita kuwa ni mgomo wa kula kupinga madhila anayopitia mtoto wake.
Mmoja wa wanafamilia ya Rubiales alithibitisha Jumatatu hii kuwa mama huyo amechukua uamuzi huo na mgomo huo anaufanyia katika kanisa la Divine Shepherdess lililopo katika mji wa Motril, Andalusia.
Mama huyo amesema kwamba ataendelea na mgomo huo hadi pale kile alichokiita kuwa ni kukosa ubinadamu na mabaya yanayomkuta mtoto wake yatakapofikia mwisho.
Rubiales amesimamishwa na Fifa kujihusisha na masuala ya soka kwa siku 90 wakati Baraza la Juu la Michezo Hispania linataka kiongozi huyo aondolewe madarakani kwa kosa alilolifanya baada ya Hispania kuifunga England bao 1-0 na kubeba Kombe la Dunia la Wanawake (WWC).
Mara baada ya Hispania kutwaa ubingwa huo Jumapili iliyopita, wakati wachezaji wakikabidhiwa medali, Rubiales alimbusu mdomoni mshambuliaji wa timu iyo, Jenni Hermoso jambo ambalo limemuweka pagumu hadi sasa.
Rubiales hata hivyo pamoja na kusakamwa kila kona lakini amekataa kujiuzulu akidai kwamba busu alilompiga mchezaji huyo lilichangiwa na furaha isiyo kifani na mchezaji huyo aliridhia na ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mchezaji huyo na umoja wa wachezaji profesheno.


Kufuatia kashfa hiyo, jopo la makocha wa timu ya wanawake wa Hispania wamejiuzulu nafasi zao wakishinikiza Rubiales aadhibiwe isipokuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Jorge Valda ambaye naye ameeleza kutofurahishwa na alichokifanya Rubiales.
Katika hatua nyingine waendesha mashitaka nchini Hispania wametangaza kuanza uchunguzi wa kosa la udhalilishaji kijinsia dhidi ya Rubiales.
Kuhusu mgomo wa kula wa Mama Angeles, mama huyo amesema kwamba ataendelea kufanya hivyo usiku na mchana hadi mwanaye atakapoacha kubughudhiwa katika kadhia inayomkabili.

“Hakuna udhalilishaji wa kijinsia kwa kuwa kulikuwa na makubaliano ya pande zote mbili, hata picha zinaonesha hivyo, mwanagu hana uwezo wa kumuumiza yeyote,” alisema Mama Angeles.

The post Mama wa aliyembusu mchezaji mdomoni agoma kula first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/28/mama-wa-aliyembusu-mchezaji-agoma-kula/feed/ 0