Kombe la Dunia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 06 Apr 2026 17:54:15 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kombe la Dunia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 DR Congo yafuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 52 https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/dr-congo-yafuzu-kombe-la-dunia-baada-ya-miaka-52/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/dr-congo-yafuzu-kombe-la-dunia-baada-ya-miaka-52/#respond Wed, 01 Apr 2026 18:12:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14513 Jalisco, MexicoTimu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ‘DR Congo’ imefuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Jamaica na hivyo kurudi katika fainali hizo walizoshiriki mara ya mwisho miaka 52 iliyopita.DR Congo ilipambana na Jamaica katika mechi hiyo ya play-off iliyochezwa Jumanne Machi 31, […]

The post DR Congo yafuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 52 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Jalisco, Mexico
Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ‘DR Congo’ imefuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Jamaica na hivyo kurudi katika fainali hizo walizoshiriki mara ya mwisho miaka 52 iliyopita.
DR Congo ilipambana na Jamaica katika mechi hiyo ya play-off iliyochezwa Jumanne Machi 31, 2026 kwenye dimba la Akron nchini Mexico na kumalizika kwa sare ya bila kufungana katika dakika 90 kabla ya beki Axel Tuanzebe kufunga bao pekee katika dakika za nyongeza.
Ushindi huo umelihakikishia taifa hilo kushiriki fainali hizo zitakazoanza Juni 11, 2026 katika nchi za Canada, Mexico na Marekani na hivyo kujikumbusha walipofuzu mara ya mwisho mwaka 1974 wakati nchi hiyo ikiitwa Zaire chini ya Rais Mobutu Seseseko.
Mechi ya DR Congo ‘The Leopards’ na Jamaica ‘The Reggae Boyz’ kwa kipindi kirefu ilionesha kuwa na nguvu sawa kwa kila timu kutengeneza mashambulizi na umakini katika kujihami.
Hatimaye DR Congo walinufaika na shambulizi walilolifanya katika dakika ya 100 ambapo Tuanzebe aliruka juu kuuwahi mpira wa kona na kuujaza wavuni kwa kichwa hali iliyoamsha shangwe kwa mashabiki wake.
Kwa kufuzu huko, DR Congo inaingia katika fainali hizo ikiwa Kundi K ambalo pia lina timu za Colombia, Ureno na Uzbekistan.
DR Congo inaungana na timu nyingine tisa za Afrika kushiriki michuano hiyo na hivyo kufanya idadi ya timu za Afrika katika fainali za mwaka huu kuwa 10.
Timu nyingine za Afrika zilizofuzu kushiriki fainali hizo ni Misri, Algeria, Afrika Kusini, Senegal, Cape Verde, Morocco, Ghana, Tunisia na Ivory Coast.
Italia yakwama tena
Wakati mashabiki DR Congo wakishangilia kurudi kwenye fainali hizo baada ya miaka 52, nchini Italia ni huzuni baada ya timu hiyo mabingwa mara nne wa Kombe la Dunia kushindwa kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo.
Italia ilishindwa kufuzu katika fainali hizo mwaka 2018 nchini Ufaransa na baada ya hapo ikashindwa kwa mara nyingine kufuzu katika fainali za Qatar mwaka 2022.
Kilichoiangusha Italia hadi kukosa fainali za 2026 ni mikwaju ya penalti katika mechi yao ya play-off dhidi ya Bosnia-Herzegovina iliyochezwa Jumanne Machi 31, 2026 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida na 30 za nyongeza.
Italia chini ya kocha Gennaro Gattuso, kiungo aliyekuwa na timu ya Italia iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, ilishindwa kuonesha umahiri kwenye penalti baada ya kulala kwa penalti 4-1.
Bosnia-Herzegovina chini ya nahodha wake mkongwe Edin Dzeko, 40, kama DR Congo nayo inafuzu kwa mara ya pili katika historia ya nchi hiyo na imepangwa Kundi B na timu za Uswisi, Canada na Qatar.

The post DR Congo yafuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 52 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/dr-congo-yafuzu-kombe-la-dunia-baada-ya-miaka-52/feed/ 0
Rais Fifa: Iran itashiriki Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/rais-fifa-iran-itashiriki-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/rais-fifa-iran-itashiriki-kombe-la-dunia/#respond Wed, 01 Apr 2026 18:06:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14511 Davos, UswisiRais wa Fifa, Gianni Infantino (pichani) amesema kwamba nchi ya Iran itacheza mechi zake za fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani kama ilivyopangwa.Kumekuwa na hofu juu ya ushiriki wa Iran kwenye faianli za Kombe la Dunia zitakazoanza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Marekani, Canada na Mexico kutokana na vita inayoendelea […]

The post Rais Fifa: Iran itashiriki Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
TOPSHOT – FIFA president Gianni Infantino poses with Al Rihla, the official match ball before a press conference during the 72th FIFA Congress in the Qatari capital Doha, on March 31, 2022. – The countdown towards the most controversial World Cup in history really begins tomorrow as the draw for Qatar 2022 takes place in Doha 2022, less than eight months befor the start of the tournament itself. (Photo by FRANCK FIFE / AFP)

Davos, Uswisi
Rais wa Fifa, Gianni Infantino (pichani) amesema kwamba nchi ya Iran itacheza mechi zake za fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani kama ilivyopangwa.
Kumekuwa na hofu juu ya ushiriki wa Iran kwenye faianli za Kombe la Dunia zitakazoanza kutimua vumbi Juni 11, 2026 katika nchi za Marekani, Canada na Mexico kutokana na vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Shirikisho la Soka Iran hivi karibuni lilitoa taarifa likidai kwamba linafanya mazungumzo na Fifa ili mechi zao zisichezewe nchini Marekani badala yake zihamishiwe Mexico.
Taarifa ya shirikisho hilo inahusishwa na kauli iliyowahi kutolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump ambaye alisema kwamba anaikaribisha Iran nchini Marekani lakini hawezi kuihakikishia usalama.
Kwa upande mwingine kauli ya Infantino kuthibitisha ushiriki wa Iran inatafsiriwa kuwa huenda imetokana na mazungumzo na Shirkisho la Soka Iran na hivyo ushiriki wa Iran kwenye fainali hizo utakuwa kama ilivyopangwa na Fifa.

“Iran itakuwapo kwenye Kombe la Dunia, tuna furaha kwa sababu wana timu imara sana, nina furaha kwa hilo, mechi zitachezwa pale zinapotakiwa kuchezwa kwa mujibu wa ratiba,” alisema Infantino.


Iran itaanza mechi zake kwa kuivaa New Zealand na baadaye Ubelgiji, mechi zitakazochezwa mjini Los Angeles Juni 15 na Juni 21 na Juni 26 itacheza na Misri mjini Seattle.
Naye Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum alisema kwamba nchi yake inajiandaa kuikaribisha Iran kucheza mechi zake za Kombe la Dunia katika taifa hilo.
Kauli ya Rais wa Mexico inapingana na ile ya Infantino ambaye alishuhudia Iran ikiichapa Costa Rica mabao 5-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Uturuki.
Baada ya mechi hiyo Infantino alisisitiza kwamba Iran itashiriki fainali za Kombe la Dunia kama ilivyopangwa na ameiona timu, amezungumza na wachezaji na kila kitu kipo sawa.

The post Rais Fifa: Iran itashiriki Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/04/01/rais-fifa-iran-itashiriki-kombe-la-dunia/feed/ 0
Wachezaji Iran wabeba mabegi ya shule kuipinga Marekani https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/wachezaji-iran-wabeba-mabegi-ya-shule/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/wachezaji-iran-wabeba-mabegi-ya-shule/#respond Sat, 28 Mar 2026 15:22:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14493 Belek, UturukiTimu ya soka ya taifa ya Iran imeingia uwanjani na vitambaa vya rangi nyeusi na mabegi ya watoto wa shule kabla ya mechi yao na Nigeria ikiwa ni ishara ya kupinga mashambulizi yaliyosababisha maafa katika moja ya shule nchini humo.Kwa mujibu wa taarifa za nchini Iran, vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi […]

The post Wachezaji Iran wabeba mabegi ya shule kuipinga Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Belek, Uturuki
Timu ya soka ya taifa ya Iran imeingia uwanjani na vitambaa vya rangi nyeusi na mabegi ya watoto wa shule kabla ya mechi yao na Nigeria ikiwa ni ishara ya kupinga mashambulizi yaliyosababisha maafa katika moja ya shule nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa za nchini Iran, vita inayoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran katika siku yake ya kwanza ilisababisha vifo vya watu wapatao 168 wakiwamo watoto 110 waliokuwa shule.
Mashambulizi hayo ya anga yalifanywa katika Shule ya Shajareh Tayyebeh Kusini mwa Iran ingawa taarifa za nchini Marekani zinadai kuwa mashambulizi hayo yalifanywa kimakosa na jeshi la nchi hiyo.
Katika kupinga mashambulizi hayo, kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki na Nigeria mjini Balek, Uturuki, wachezaji wa Iran walionekana wakiwa na mabegi ya watoto wakiongozwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu za FC Porto na Inter Milan, Mehdi Taremi.
Taarifa ya chanzo kimoja nchini Iran ilieleza kuwa wachezaji hao wamebeba mageni ya rangi ya pinki na zambarau ili kuwakumbuka watoto wa shule waliouliwa katika shambulizi lililofanywa na Jeshi la Marekani.
Maofisa wa Iran walizilaumu Marekani na Israel kwa shambulizi walilofanya kwenye shule hiyo ambayo ipo karibu na kituo kimoja cha jeshi ingawa nchi hizo mbili hazijakiri kuhusika na shambulizi hilo.
Iran ni kati ya nchi ambazo zimefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico ingawa ushiriki wa Iran upo njia panda kwa kuwa haitaki mechi zao zichezwe Marekani licha ya ratiba kupangwa hivyo.
Fainali za Kombe la Dunia zimepangwa kuanza Juni 11, 2026 na Iran imechukua msimamo wa kukataa kupeleka timu Marekani hasa baada ya rais wa nchi hiyo, Donald Trump kusema kuwa anawakaribisha Iran lakini hawezi kuwahakikishia usalama wao.
Wakati huo huo, Iran imepiga marufuku timu zao za michezo kwenda katika nchi ambazo zina ugomvi nao, kauli ambayo imekuja wakati timu ya soka ya Traktor Sazi ya nchini Iran ikijiandaa kwenda Saudi Arabia.
Traktor ikiwa Saudi Arabia inatarajia kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Asia dhidi ya Shabab Al Ahli ya Dubai, mechi iliyopangwa kuchezwa Alhamisi ijayo.
Taarifa ya katazo hilo imetolewa na Wizara ya Michezo ya Iran na huenda ikaathiri moja kwa moja ushiriki wa Iran kwenye Kombe la Dunia kama Fifa hawatohamisha mechi za taifa hilo na kuzipeleka katika nchi nyingine mwenyeji kati ya Mexico au Canada.

The post Wachezaji Iran wabeba mabegi ya shule kuipinga Marekani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/28/wachezaji-iran-wabeba-mabegi-ya-shule/feed/ 0
Iran: Tunaipinga Marekani si Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/iran-tunaipinga-marekani-si-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/iran-tunaipinga-marekani-si-kombe-la-dunia/#respond Fri, 20 Mar 2026 14:21:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14470 Tehran, IranShirikisho la Soka Iran limesisitiza kuwa nchi yao inaipinga Marekani na si fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini humo kuanzia Juni 11, 2026.Kwa mujibu wa chanzo cha habari nchini Iran, Far News Agency, chanzo hicho kimemnukuu kiongozi mkuu wa Shirikisho la Soka Iran, Mehdi Taj akitoa msimamo huo Jumatano Machi 18, 2026.Katika siku […]

The post Iran: Tunaipinga Marekani si Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Tehran, Iran
Shirikisho la Soka Iran limesisitiza kuwa nchi yao inaipinga Marekani na si fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini humo kuanzia Juni 11, 2026.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari nchini Iran, Far News Agency, chanzo hicho kimemnukuu kiongozi mkuu wa Shirikisho la Soka Iran, Mehdi Taj akitoa msimamo huo Jumatano Machi 18, 2026.
Katika siku za hivi karibuni msimamo wa Iran kushiriki fainali hizo ambazo Marekani itakuwa mwenyeji na nchi za Mexico na Canada, umekuwa njia panda tangu Marekani na Israel zifanye mashambulizi ya anga nchini Irani mwishoni mwa mwezi uliopita.
Timu ya taifa ya Iran katika fainali hizo inatarajia kucheza mechi zake tatu za awali nchini Marekani na kwa mujibu wa Taj, watajiandaa kwa mechi hizo lakini wataipinga Marekani na si fainali za Kombe la Dunia.
Taj pia alitumia mtandao wa Twitter au X kufafanua kuwa katika mkakati huo wa kuipinga Marekani, kwa sasa wapo katika mazungumzo na Fifa kwa lengo la kuhakikisha mechi zao zinahamishiwa nchini Mexico.

“Rais Donald Trump aliposema wazi kwamba hawezi kuihakikishia usalama timu ya taifa ya Iran, maana yake ni kwamba hatuwezi kwenda Marekani, tunawasiliana na Fifa ili mechi zetu zihamishiwe Mexico,” alisema Taj.


Kwa upande mwingine Rais wa Fifa, Gianni Infantino alinukuliwa akisema kwamba anatarajia timu zote zilizofuzu fainali za Kombe la Dunia kushiriki katika misingi ya haki na kuheshimiana na matumaini ya Fifa ni kuona fainali hizo zinafanyika kama zilivyopangwa.
Ikitokea mechi za Iran kuhamishiwa Mexico bado timu hizo zinaweza kukutana katika raundi ya pili ya michuano hiyo nchini Marekani kwa kuzingatia nafasi zitakazoshika katika makundi yao.

The post Iran: Tunaipinga Marekani si Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/iran-tunaipinga-marekani-si-kombe-la-dunia/feed/ 0
Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/#respond Sun, 15 Mar 2026 14:02:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14431 New York, MarekaniRais wa Marekani, Donald Trump amesema itakuwa sahihi kwa Iran kutoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa usalama wao na maisha yao wakati Iran wamedai kuwa sababu ya wao kutoshiriki fainali hizo ni Marekani.Katika andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alisema anaikaribisha Iran kwenye fainali hizo lakini hapo hapo akasema […]

The post Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump amesema itakuwa sahihi kwa Iran kutoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa usalama wao na maisha yao wakati Iran wamedai kuwa sababu ya wao kutoshiriki fainali hizo ni Marekani.
Katika andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alisema anaikaribisha Iran kwenye fainali hizo lakini hapo hapo akasema kwamba anadhani hawapaswi kushiriki.
Kauli ya Trump imekuja baada ya Waziri wa Michezo na Vijana wa Iran, Ahmad Donyamali kusema kwamba nchi yake haiko katika nafasi ya kushiriki fainali hizo ambazo zitafanyika katika nchi za Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 mwaka huu.
Katika fainali hizo Iran imepangwa kuanza mechi zake Juni 15 dhidi ya New Zealand na Juni 21 dhidi ya Ubelgiji zitakazopigwa mjini Los Angeles na kumalizia na mechi dhidi ya Misri itakayopigwa Juni 26 mjini Seattle.
Ushiriki wa timu ya Iran hata hivyo bado upo njia panda tangu Marekani na Israel waanze mashambulizi ya anga dhidi ya taifa hilo na kumuua kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Iran nayo ikajibu mapigo kwa kufanya mashambulizi kama hayo Israel na mengine katika nchi za Bahrain, Qatar, Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu, nchi ambazo zina kambi za kijeshi za Marekani.

“Timu ya taifa ya soka ya Iran inakaribishwa kwenye Kombe la Dunia lakini kwa hakika siamini kama ni sahihi wao kuwa hapa, ni kwa usalama wao na maisha yao,” alisema Trump katika andiko lake.


Ujumbe wa Iran hata hivyo umekuwa tofauti kuhusu hoja hiyo ya Trump baada ya kudai kuwa waandaaji wa fainali za Kombe la Dunia ni Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) na si nchi yoyote.

“Timu ya taifa ya Iran pia imefuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia na hiyo ni baada ya kupata ushindi na kuwa moja ya timu za kwanza kufikia katika hatua hii muhimu,” ilieleza taarifa ya kutoka Iran.


Taarifa hiyo pia ilifafanua kwamba nchi ambayo inaweza kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia ni ile ambayo imebeba hadhi ya kuwa nchi mwenyeji lakini haina uwezo wa kuzihakikishia usalama timu zinazoshiriki fainali hizo.
Awali Rais wa Fifa, Gianni Infantino alisema kwamba Rais Trump alimwambia kuwa Iran inakaribishwa kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Wakati Infantino akitoa kauli hiyo, Waziri wa Michezo wa Iran alinukuliwa akisema kwa sababu serikali dhalimu imemuua kiongozi wao haoni kama wapo katika nafasi nzuri ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia.
Ikitokea Iran ikajitoa katika fainali hizo, kanuni za Fifa zinalipa shirikisho hilo nafasi ya kuchagua timu ya kushiriki badala ya Iran ingawa hadi sasa haijaweza kufahamika timu inayoweza kupewa nafasi hiyo.

The post Iran ikikataa Kombe la Dunia, Trump awaita, atoa tahadhari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/15/iran-ikikataa-kombe-la-dunia-trump-awaita-atoa-tahadhari/feed/ 0
Wazo la timu 64 Kombe la Dunia lapingwa https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/wazo-la-timu-64-kombe-la-dunia-lapingwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/wazo-la-timu-64-kombe-la-dunia-lapingwa/#respond Tue, 15 Apr 2025 16:50:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13249 Miami, MarekaniRais wa Shirkisho la Soka Marekani Kaskazini, Kati na Carribean (Concacaf), Victor Montagliani amepinga wazo la kiongozi wa Shirikisho la Soka Marekani Kusini (CONMEBOL), Alejandro Domínguez kutaka timu shiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2030 ziwe 64.Domínguez aliwasilisha rasmi wazo la kupanua mashindano hayo kwenye kikao cha Baraza la Fifa kilichoendeshwa kwa mtandao […]

The post Wazo la timu 64 Kombe la Dunia lapingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Miami, Marekani
Rais wa Shirkisho la Soka Marekani Kaskazini, Kati na Carribean (Concacaf), Victor Montagliani amepinga wazo la kiongozi wa Shirikisho la Soka Marekani Kusini (CONMEBOL), Alejandro Domínguez kutaka timu shiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2030 ziwe 64.
Domínguez aliwasilisha rasmi wazo la kupanua mashindano hayo kwenye kikao cha Baraza la Fifa kilichoendeshwa kwa mtandao akisisitiza timu shiriki ziongezwe kutoka 32 za sasa hadi kufikia 64.
“Kwa upande wetu Concacaf, tumeonesha tupo wazi kwa mabadiliko kwa kuunga mkono fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake pamoja na muendelezo wa mabadiliko wa mashirikisho yetu kwa timu za wanaume na wanawake na mashindano ya klabu,” alisema Montagliani.
“Sidhani kama kuongeza timu katika fainali za Kombe la Dunia za wanaume kufikia 64 ni hatua sahihi kwa mashindano hayo pamoja na mustakabali mpana wa soka kwa mashindano ya timu za taifa, klabu, ligi na wachezaji,” alisema Montagliani.
Fifa itaanza kufanya majaribio ya mfumo wa timu 48 kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 lakini Domínguez alisisitiza haja ya kufanya zaidi ya hilo kwa kupanua wigo wa mashindano.
Naye Rais wa Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Čeferin pia alionesha kutounga mkono hoja ya Domínguez akisema wazo la kuongeza idadi ya timu ni baya.

“Nafikiri ni wazo baya, si wazo zuri kwa fainali zenyewe za Kombe la Dunia, na pia si wazo zuri kwa timu zinazofuzu, kwa hiyo siungi mkono wazo hili, sijui limetokea wapi lakini ni hatari kwa sababu hatukufahamu lolote kabla ya wazo hili katika Baraza la Fifa,” alisema Ceferin.


Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka Asia, (AFC), Sheikh Salman bin Ibrahim alisisitiza kwamba ongezeko la idadi hiyo litahamasisha na kuwa mwanzo wa mvurugano.
“Kama jambo hili litakuwa wazi kwa mabadiliko maana yake ni kwamba mlango utakuwa wazi kwa kuongeza timu 64 lakini kuna mtu pia anaweza kuja na hoja ya kutaka idadi ya timu ifikie 132, mwisho itakuwaje? Ni mvurugano,” alisema Sheikh Salman.
Katika fainali za Kombe la Dunia 2026, majaribio yatafanyika kwa timu 48 ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya fainali hizo zitakazochezwa Marekani, Mexico na Canada.

The post Wazo la timu 64 Kombe la Dunia lapingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/15/wazo-la-timu-64-kombe-la-dunia-lapingwa/feed/ 0
Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/#respond Sun, 09 Mar 2025 10:59:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13116 New York, MarekaniRais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia mipango ya fainali za Kombe la Dunia 2026 huku Trump akihoji kama Marekani itabeba taji la michuano hiyo.Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaa hii kwenye Ikulu ya White House, Trump inadaiwa alimuuliza Infantino kama Marekani itaweza […]

The post Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia mipango ya fainali za Kombe la Dunia 2026 huku Trump akihoji kama Marekani itabeba taji la michuano hiyo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaa hii kwenye Ikulu ya White House, Trump inadaiwa alimuuliza Infantino kama Marekani itaweza kushinda Kombe la Dunia na Infantino akaonesha kuwa jambo hilo linawezekana.
Sambamba na fainali za Kombe la Dunia 2026, Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu ambazo zitafanyika baadaye mwaka huu.
Awali baada ya Trump kumuuliza Infantino nchi ambazo zinaweza kushinda Kombe la Dunia, Infantino akazitaJa na ndipo Trump alipomuuliza kuhusu Marekani ambayo haikuwa kwenye orodha ya awali ya Infantino.
“Brazil, Argentina, England, Hispania, Ujerumani,” alizitaja Infantino na ndipo Trump alipohoji iwapo Marekani inaweza kuishangaza dunia na kubeba taji hilo.
Katika ufafanuzi wa hoja hiyo, Infantino alimwambia rais huyo wa 47 wa Marekani kwamba nchi yake inaweza kubeba taji hilo kwa msaada wa mashabiki na hata timu yao ni moja ya timu bora duniani.
“Kwa hiyo uwezekano upo?” Alihoji zaidi Trump na Infantino akamjibu hapo hapo, “Hakika nafasi hiyo ipo.”
Trump pia alimuahidi Infantino kwamba ataunda kikosi kazi kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo safari hii zinafanyika Marekani ya Kusini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.
Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali hizo ikishirikiana na nchi za Canada na Mexico ingawa nchi hizo kwa sasa zipo katika mzozo unaohusisha mambo ya kodi baada ya Trump kutaka bidhaa za nchi hizo majirani zake zitozwe kodi.
Trump hata hivyo anaamini mzozo wa mataifa hayo kuhusu masuala ya kodi utazifanya fainali hizo ziwe na hamasa zaidi.
Katika historia ya fainali za Kombe la Dunia, Marekani ina rekodi ya kufikia hatua ya nusu fainali mwaka 1930 katika fainali za kwanza katika historia ya michuano hiyo na baada ya hapo Marekani pia ilifikia hatua ya robo fainali mwaka 2002.

The post Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/feed/ 0
Rasmi, Saudia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 https://www.greensports.co.tz/2024/12/11/rasmi-saudia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/11/rasmi-saudia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/#respond Wed, 11 Dec 2024 19:38:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12386 Nyon, SwitzerlandFainali za Kombe la Dunia za Wanaume za 2034 zitafanyika nchini Saudi Arabia wakati Hispania, Ureno na Morocco kwa pamoja wataandaa fainali hizo kwa mwaka 2030.Sambamba na hilo, mechi tatu za fainali michuano hiyo kwa mwaka 2030, zitachezwa katika nchi za Argentina, Paraguay na Uruguay kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 100 ya Fifa.Uamuzi […]

The post Rasmi, Saudia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Nyon, Switzerland
Fainali za Kombe la Dunia za Wanaume za 2034 zitafanyika nchini Saudi Arabia wakati Hispania, Ureno na Morocco kwa pamoja wataandaa fainali hizo kwa mwaka 2030.
Sambamba na hilo, mechi tatu za fainali michuano hiyo kwa mwaka 2030, zitachezwa katika nchi za Argentina, Paraguay na Uruguay kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 100 ya Fifa.
Uamuzi huo uliotangazwa siku za nyuma ulithibitishwa rasmi leo Jumatano katika mkutano mkuu wa Fifa uliohusisha wajumbe wote wa mataifa 211 waliopiga kura kwa njia ya mtandao.
Nchi ya Norway ilitangaza kujitenga katika zoezi hilo kwa sababu ya kutokuwa na imani na taratibu za Fifa za kuteua nchi mwenyeji wa fainali hizo na si kwa sababu Saudi Arabia au Saudia imetangazwa kuwa mwenyeji.
Nayo Switzerland iliomba kupitia chama chake cha soka uwakilishi wao utambuliwe katika mukhtasari wa vikao vya mkutano mkuu.
Jana Jumanne Chama cha Soka Switzerland kilitoa taarifa kikidai kwamba kitaridhia Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa fainali hizo lakini kikataka masuala ya haki za binadamu nchini humo yasimamiwe na Fifa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Denmark nayo kupitia chama chake cha soka yaani DBU kilitangaza kuunga mkono taratibu zote za kuipa Saudi Arabia uenyeji wa fainali hizo lakini kikataka Fifa waangazie masuala ya haki za binadamu nchini humo.
Saudi Arabia imekuwa ikituhumiwa kwa kutumia fedha nyingi kwenye michezo kama kinga ya kuusafisha utawala wa kifalme na rekodi mbaya ya haki za binadamu.
Tayari Saudi Arabia imejenga viwanja vya soka vinne kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2034 na mpango uliopo ni kujenga viwanja 15.

The post Rasmi, Saudia mwenyeji Kombe la Dunia 2034 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/11/rasmi-saudia-mwenyeji-kombe-la-dunia-2034/feed/ 0
Kesi ya aliyepigwa busu yanguruma mahakamani https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/aliyepigwa-busu-ajenga-hoja-mahakamani/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/aliyepigwa-busu-ajenga-hoja-mahakamani/#respond Tue, 02 Jan 2024 19:44:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9119 Madrid, HispaniaMchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso ameiambia mahakama kuwa busu la mdomoni alilopigwa na aliyekuwa bosi wa soka Hispania, Luis Rubiales halikuwa na ridhaa yake.Mara baada ya timu ya wanawake ya Hispania kuibwaga England na kubeba Kombe la Dunia, Rubiales aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania alimkumbatia kwa nguvu Jenni […]

The post Kesi ya aliyepigwa busu yanguruma mahakamani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso ameiambia mahakama kuwa busu la mdomoni alilopigwa na aliyekuwa bosi wa soka Hispania, Luis Rubiales halikuwa na ridhaa yake.
Mara baada ya timu ya wanawake ya Hispania kuibwaga England na kubeba Kombe la Dunia, Rubiales aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Hispania alimkumbatia kwa nguvu Jenni na kumpiga busu la mdomoni.
Kitendo hicho kilizua taharuki na kusababisha Rubiales kusimamishwa na Fifa kujihusisha na soka kwa siku 90 kabla ya kuamua kung’atuka nafasi yake katika shirikisho la soka Hispania lakini Jenni aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.
Baada ya mahakama hiyo ya mjini Madrid kuelezwa hivyo na Jenni leo Jumanne, sasa ni jukumu la Jaji kuamua kama Rubiales atashitakiwa kwa kosa la udhalilishaji kijinsia au la.
Jenni, 33, ambaye ni mfungaji kinara wa mabao wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania aliieleza mahakama tukio zima kwa zaidi ya saa moja na vyombo vya habari vilidai kwamba katika hoja zake alisema kuwa busu alilopigwa hakulitarajia na hakukuwa na makubaliano yoyote.
Rubiales kwa upande wake ameshikilia msimamo wake akikana kufanya kosa lolote wakati mahakama imeamua kuendelea na uchunguzi ikiwamo kutumia kamera za CCTV ili kupata ushahidi zaidi wa tukio hilo kabla ya kutoa uamuzi.
Tukio la Jenni kupigwa busu lilitokea Agosti mwaka jana mjini Sydney, Australia mara baada ya mechi ya fainali wakati wachezaji wa Hispania waliobeba taji hilo wakipita jukwaani kuvalishwa medali zao ndipo Rubiales alimpokumbatia Jenni na kumpiga busu la mdomoni.

The post Kesi ya aliyepigwa busu yanguruma mahakamani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/02/aliyepigwa-busu-ajenga-hoja-mahakamani/feed/ 0
Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/#respond Sat, 25 Nov 2023 05:01:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8620 Rio de Janeiro, BrazilShirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufanya uchunguzi baada ya kutokea vurugu katika mechi kati ya Brazil na Argentina na kusababisha mechi hiyo kuchelewa kuanza kwa nusu saa.Mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ilichelewa kuanza baada ya kutokea vurugu […]

The post Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rio de Janeiro, Brazil
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kufanya uchunguzi baada ya kutokea vurugu katika mechi kati ya Brazil na Argentina na kusababisha mechi hiyo kuchelewa kuanza kwa nusu saa.
Mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro ilichelewa kuanza baada ya kutokea vurugu zilizosababisha polisi watumie virungu kuwatuliza mashabiki wa Argentina.
Mara tu baada ya kuanza kwa vurugu, nahodha wa Argentina Lionel Mess aliwaongoza wachezaji wake kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na baadaye alinukuliwa akisema kwamba alilazimika kufanya hivyo kwa sababu alihofia hali ingeweza kuwa mbaya zaidi.
Messi aliwalaumu polisi ambao walitumia virungu kuwakabili mashabiki hao ambao nao walivunja viti na kuvitumia kujihami wakati wengine walikimbilia katikati ya uwanja ambapo baadaye shabiki mmoja alionekana akiwa amebebwa kwenye machela na watu wa huduma ya kwanza.
Katika sakata hilo ambalo lilianza wakati nyimbo za taifa zikiimbwa, huenda vyama vya soka vya Brazil na Argentina vyote vikajikuta vikikumbana na adhabu ya Fifa.
Wakati vurugu zikiendelea, wachezaji wa timu zote walionekana kuwafuata mashabiki wao na kuanza kuwatuliza ambapo kipa wa Argentina na klabu ya Aston Villa, Emiliano Martinez alionekana akijaribu kumnyang’anya polisi mmoja kirungu.

“Fifa inathibitisha kwamba kamati ya nidhamu imeanza uchunguzi dhidi ya Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na Chama cha Soka Argentina (AFA),” ilieleza taarifa ya Fifa iliyopatikana Ijumaa.


Adhabu inayoweza kutolewa kwa kosa hilo ni faini au uwanja kufungiwa, Brazil inahusishwa na kosa la kushindwa kutuliza amani kwenye mechi wakati Argentina inahusishwa na kosa la vurugu za mashabiki.
Baadaye mechi hiyo iliendelea na kuchezwa kwa dakika 90 kama kawaida na Argentina ambao ndio mabingwa wa dunia, walitoka na ushindi wa bao 1-0.

The post Fifa yachunguza vurugu mechi ya Brazil, Argentina first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/25/fifa-yachunguza-vurugu-mechi-ya-brazil-argentina/feed/ 0