Kikapu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 01 Oct 2024 06:31:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Kikapu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Dikembe Mutombo afariki dunia https://www.greensports.co.tz/2024/10/01/dikembe-mutombo-afariki-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/01/dikembe-mutombo-afariki-dunia/#respond Tue, 01 Oct 2024 06:31:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11963 Atlanta, MarekaniNyota wa zamani wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Dikembe Mutombo (pichani) amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani (kansa) ya ubongo akiwa na miaka 58.Kwa mujibu wa NBA, Mutombo amefariki jana Jumatatu Septemba 30 ikiwa takriban miaka miwili imepita tangu ndugu zake watoe taarifa kuwa nyota huyo alikuwa katika matibabu ya saratani.“Kwenye dimba la […]

The post Dikembe Mutombo afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Atlanta, Marekani
Nyota wa zamani wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Dikembe Mutombo (pichani) amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani (kansa) ya ubongo akiwa na miaka 58.
Kwa mujibu wa NBA, Mutombo amefariki jana Jumatatu Septemba 30 ikiwa takriban miaka miwili imepita tangu ndugu zake watoe taarifa kuwa nyota huyo alikuwa katika matibabu ya saratani.
“Kwenye dimba la mpira wa kikapu alikuwa ni mmoja wa wazuiaji mahiri na mlinzi bora katika historia ya NBA, nje ya mpira wa kikapu alikuwa mtu mwenye moyo wa kuwasaidia wengine,” alisema Kamishna wa NBA, Adam Silver.
Silver alisema kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa na sifa za kuwa balozi wa dunia wa NBA zaidi ya Mutombo kwani alikuwa ni mtu mwenye ubinadamu wa hali ya juu.
Ni mtu aliyependa kuona kile ambacho mpira wa kikapu ungekifanya kwa kuleta matokeo chanya katika jamii hasa kwa jamii yake ya asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na bara la Afrika kwa ujumla.

“Nimekuwa mwenye bahati ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani na Mutombo na nikaona jinsi alivyokuwa muungwana na mwenye shauku ya kuwainua watu, wakati wote alikuwa mwenye kupatikana katika matukio ya NBA,” alisema Silver.


Katika mpira wa kikapu, Mutombo alizoeleka kwa namna alivyoutumia vyema urefu wake wa futi saba na alipenda kuinua kidole chake cha mkono wa kulia juu baada ya kuzuia mipira iliyoelekezwa katika timu yake.
Wakati wa uhai wake alicheza misimu 18 ya NBA akiwa na timu za Houston Rockets, Philadelphia 76ers, Atlanta Hawks, Denver Nuggets, New Jersey Nets, New York Knicks kabla ya kustaafu baada ya msimu wa 2008-09.
Mutombo ambaye pia ni kati ya wachezaji mpira wa kikapu bora walioingia katika Basketball Hall of Fame, anazungumza lugha tisa, mwaka 1997 alianzisha taasisi ya Dikembe Mutombo Foundation ambayo inatoa misaada ya kuboresha huduma za afya na hali za maisha kwa watu wa DR Congo.
Kupitia taasisi hiyo, Mutombo amewezesha kujengwa hospitali yenye vitanda 170 mjini Kinshasa, hospitali ambayo imetoa huduma kwa watu zaidi ya nusu milioni wakiwamo wenye uwezo mdogo kiuchumi.

The post Dikembe Mutombo afariki dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/01/dikembe-mutombo-afariki-dunia/feed/ 0
Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/thibaut-courtois-kukosa-euro-2024/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/thibaut-courtois-kukosa-euro-2024/#respond Wed, 01 May 2024 19:16:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10799 Brussels, UbelgijiKipa wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois (pichani) sasa ni rasmi kuwa hatoweza kuiwakilisha timu hiyo kwenye fainali za Euro 2024 kutokana na matatizo ya goti yanayomkabili.Habari hizo zimekuja huku kukiwa na habari nyingine zinazodai kwamba kipa huyo huenda akawa tayari kuichezea klabu yake ya Real Madrid katika mechi chache zilizobaki za […]

The post Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Brussels, Ubelgiji
Kipa wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois (pichani) sasa ni rasmi kuwa hatoweza kuiwakilisha timu hiyo kwenye fainali za Euro 2024 kutokana na matatizo ya goti yanayomkabili.
Habari hizo zimekuja huku kukiwa na habari nyingine zinazodai kwamba kipa huyo huenda akawa tayari kuichezea klabu yake ya Real Madrid katika mechi chache zilizobaki za msimu huu.
Courtois, 31, amekosekana uwanjani msimu huu wote na mwezi Machi mwaka huu, mchezaji huyo alihitaji kufanyiwa operesheni nyingine baada ya kuonekana kulikuwa na tatizo lililofanya asiweze kuwa fiti.
Akimzungumzia kipa huyo na habari za uwezekano wa kurudi kwenye kikosi cha Real Madrid kwa msimu huu, kocha wa Ubelgiji, Domenico Tedesco alimfuta moja kwa moja katika hesabu zake kwa ajili ya fainali za Euro 2024.
Desemba mwaka jana, Courtois ambaye ameichezea Ubelgiji mara 102 alisema kwamba anadhani hatokuwa amepona kwa asilimia 100 kwa ajili ya kuiwakilisha Ubelgiji kwenye fainali za Euro 2024 zitakazofanyika nchini Ujerumani kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.
Kwa upande wake, Tedesco alisema kwamba suala la kipa huyo limekwisha, “kuhusu habari hiyo kila kitu kimeshasemwa, sitaki kurudiarudia, tunawaangalia wachezaji ambao wapo katika ubora.”
Naye kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amenukuliwa akisema kwamba ana matumaini ya kipa huyo kuwamo katika kikosi cha Real Madrid kitakachoumana na Cadiz Jumamosi ijayo katika mechi ya La Liga.

The post Thibaut Courtois kukosa Euro 2024 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/thibaut-courtois-kukosa-euro-2024/feed/ 0
Kikapu wajitoa kwenye mashindano https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kikapu-wajitoa-kwenye-mashindano/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kikapu-wajitoa-kwenye-mashindano/#respond Thu, 01 Feb 2024 18:52:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9542 Na mwandishi wetuTimu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzanite haitashiriki michuano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopangwa kufanyika nchini Rwanda mwezi huu.Awali, michuano hiyo ilitarajiwa kufanyika kuanza Februari Mosi hadi 10, mwaka huu kabla ya kuahirishwa.Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari, Mary Arthur, […]

The post Kikapu wajitoa kwenye mashindano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzanite haitashiriki michuano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyopangwa kufanyika nchini Rwanda mwezi huu.
Awali, michuano hiyo ilitarajiwa kufanyika kuanza Februari Mosi hadi 10, mwaka huu kabla ya kuahirishwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari, Mary Arthur, Tanzanite haitashiriki michuano hiyo baada ya kupewa taarifa ya kuahirishwa hivyo itaendelea na majukumu mengine.
“Shirikisho lilipokea mwaliko kutoka serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wa kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoshirikisha michezo mbalimbali kutoka nchi wanachama,” alisema na kuongeza:
“Lakini baadaye tulipokea taarifa za kuahirishwa kwa mashindano husika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa waandaaji.
“Tanzanite haitashiriki michuano hiyo na kuwaomba radhi viongozi na mashabiki, wadau na dawati zima la ufundi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.”
Nchi nyingine zilizoalikwa awali kwenye michuano hiyo ni Kenya, Uganda, Burundi, Sudan Kusini, DR Congo, Somalia na wenyeji Rwanda.

The post Kikapu wajitoa kwenye mashindano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/kikapu-wajitoa-kwenye-mashindano/feed/ 0
Pazi waahidi mambo mazuri Rwanda https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/pazi-waahidi-mambo-mazuri-rwanda/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/pazi-waahidi-mambo-mazuri-rwanda/#respond Fri, 26 Jan 2024 20:24:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9459 Na mwandishi wetuKlabu ya mpira wa kikapu ya Pazi imeahidi kufanya vizuri katika mashindano maalumu yanayoshirikisha klabu bora za ukanda wa Afrika Mashariki yanayoanza kesho Jumamosi nchini Rwanda.Akizungumza na waandishi kabla ya kuelekea Rwanda, Rais wa Pazi, Mussa Mzenji alisema kwa maandalizi waliyofanya ana uhakika watashiriki kiushindani na kufanya vizuri.“Tuna uhakika tutafanya vizuri, tumejipanga na […]

The post Pazi waahidi mambo mazuri Rwanda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya mpira wa kikapu ya Pazi imeahidi kufanya vizuri katika mashindano maalumu yanayoshirikisha klabu bora za ukanda wa Afrika Mashariki yanayoanza kesho Jumamosi nchini Rwanda.
Akizungumza na waandishi kabla ya kuelekea Rwanda, Rais wa Pazi, Mussa Mzenji alisema kwa maandalizi waliyofanya ana uhakika watashiriki kiushindani na kufanya vizuri.
“Tuna uhakika tutafanya vizuri, tumejipanga na kila wakati tumekuwa tukijitahidi kuhakikisha tunajenga mahusiano mazuri na klabu mbalimbali, tutaendeleza kiwango bora na hatimaye kuwavutia wawekezaji waje watusapoti,” alisema.
Katibu Mkuu, Haby Mayeye alisema mwaliko huo umekuja kutokana na mafanikio ya mwaka jana ambapo walishiriki mashindano ya kufuzu Klabu Bingwa Afrika na kujitahidi kuonesha kiwango kizuri.
Alisema watahakikisha wanawakilisha vyema ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ya msimu huu.
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Nicholas Mihayo alisema Pazi ni mfano wa kuigwa kutokana na kiwango bora ilichokionesha msimu uliopita na kuchangia kupata mwaliko huo wa kimataifa akisema anaamini watapeperusha vyema bendera ya nchi.

The post Pazi waahidi mambo mazuri Rwanda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/pazi-waahidi-mambo-mazuri-rwanda/feed/ 0
Uzoefu Ligi ya Mabingwa waikwaza Pazi https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/uzoefu-ligi-ya-mabingwa-waikwaza-pazi/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/uzoefu-ligi-ya-mabingwa-waikwaza-pazi/#respond Sun, 26 Nov 2023 09:29:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8633 Na mwandishi wetuKocha wa timu ya mpira wa kikapu ya Pazi, Mohamed Mbwana amesema kutolewa mapema kwenye mashindano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika (BAL), kumetokana na wachezaji wake kutokuwa na uzoefu wa kutosha.Akizungumza baada ya mchezo wa mwisho dhidi ya Dynamo ya Burundi ambayo walipoteza kwa pointi 85-88, Mbwana alisema kingine kilichochangia watoke mapema […]

The post Uzoefu Ligi ya Mabingwa waikwaza Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya mpira wa kikapu ya Pazi, Mohamed Mbwana amesema kutolewa mapema kwenye mashindano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika (BAL), kumetokana na wachezaji wake kutokuwa na uzoefu wa kutosha.
Akizungumza baada ya mchezo wa mwisho dhidi ya Dynamo ya Burundi ambayo walipoteza kwa pointi 85-88, Mbwana alisema kingine kilichochangia watoke mapema ni kukosa bahati kutokana na kiwango ambacho kilioneshwa na wachezaji wake.

“Tumekubali matokeo lakini ushiriki wetu umekuwa na faida tumejifunza kitu, kikubwa hapa ni uzoefu mdogo ambao wachezaji wangu wanao lakini nawapongeza walicheza kwa kujituma katika mechi zote nadhani tulikosa bahati,” alisema Mbwana.


Kocha huyo alisema wanarudi kujipanga upya kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na kucheza mechi kadhaa za kirafiki za kimataifa ambazo anaamini zitasaidia kuwapa wachezaji wake uzoefu kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya Afrika.
Pia kocha huyo aliwaomba radhi mashabiki wao kwa matokeo hayo ambayo wameyapata kwenye mashindano hayo na kueleza kusudio lao ilikuwa ni kufanya vizuri na kurudi na ubingwa ingawa imekuwa tofauti.
Timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali kutoka kundi A ilipokuwa Pazi ni Dynamo ya Burundi na Capetown Tigers ya Afrika Kusini.
Katika mashindano hayo Pazi ilipoteza mechi zote tatu za hatua ya makundi, mbali ya Dynamo pia ilipoteza dhidi ya NBA Academy kwa pointi 57-84, ikafungwa na Capetown Tigers kwa pointi 87-95.

The post Uzoefu Ligi ya Mabingwa waikwaza Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/26/uzoefu-ligi-ya-mabingwa-waikwaza-pazi/feed/ 0
Magic Johnson naye ni bilionea https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/magic-johnson-naye-ni-bilionea/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/magic-johnson-naye-ni-bilionea/#respond Wed, 01 Nov 2023 05:47:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8307 Nyota wa zamani wa mpira wa kikapu, Magic Johnson ametangazwa na jarida maarufu duniani la uchumi na biashara, Forbes kuwa bilionea na hivyo kufanya idadi ya wanamichezo mabilionea nchini Marekani kufikia wanne. Kwa kufikia hadhi hiyo, Magic Johnson sasa anakuwa katika kundi moja na wanamichezo wengine, Michael Jordan na LeBron James ambao ni wa mpira […]

The post Magic Johnson naye ni bilionea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Nyota wa zamani wa mpira wa kikapu, Magic Johnson ametangazwa na jarida maarufu duniani la uchumi na biashara, Forbes kuwa bilionea na hivyo kufanya idadi ya wanamichezo mabilionea nchini Marekani kufikia wanne. Kwa kufikia hadhi hiyo, Magic Johnson sasa anakuwa katika kundi moja na wanamichezo wengine, Michael Jordan na LeBron James ambao ni wa mpira wa kikapu na Tiger Woods wa golfu. Tathmini ya Forbes inaonesha kuwa Magic Johnson ambaye amewekeza katika timu ya mpira wa kikapu na biashara nyinginezo ikiwamo viwanda ana utajiri unaofikia Dola bilioni 1.2. Katika misimu 13 aliyocheza mpira wa kikapu akiwa na timu ya Los Angeles Lakers katika ligi ya NBA nchini Marekani, Magic Johnson aliingiza dola 40 milioni lakini mambo yalianza kumbadilikia taratibu alipokutana na watu wa biashara na pato lake kuongezeka. Miongoni mwa utajiri wa Magic Johnson ni umiliki wake wa asilimia 60 katika kampuni ya bima ya maisha ambapo pato lake la mwaka kwa mujibu wa Forbes linatajwa kufikia takriban dola bilioni 2.6.

The post Magic Johnson naye ni bilionea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/01/magic-johnson-naye-ni-bilionea/feed/ 0
MwanaFA aipa neno Pazi https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/mwanafa-aipa-neno-pazi/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/mwanafa-aipa-neno-pazi/#respond Thu, 26 Oct 2023 20:18:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8244 Na mwandishi wetuNaibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ameihimiza klabu ya mpira wa kikapu ya Pazi kujitahidi katika michuano ya Afrika kwa kufanya vizuri ikijua wazi kuwa imebeba jukumu la kitaifa.Pazi imefuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Kikapu Afrika itakayofanyika Afrika Kusini kuanzia Novemba 14 hadi 19, mwaka huu baada ya […]

The post MwanaFA aipa neno Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ameihimiza klabu ya mpira wa kikapu ya Pazi kujitahidi katika michuano ya Afrika kwa kufanya vizuri ikijua wazi kuwa imebeba jukumu la kitaifa.
Pazi imefuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Kikapu Afrika itakayofanyika Afrika Kusini kuanzia Novemba 14 hadi 19, mwaka huu baada ya kufanya vizuri katika michezo ya Kanda ya Afrika Mashariki hivi karibuni.

“Nilihudhuria katika mashindano hivi karibuni na kuona Pazi inacheza kama timu, niwatie moyo waendelee kufanya hivyo, wafahamu wana bendera ya nchi, na sisi tuna sababu ya kuishabikia kwa sababu ni timu bora,” alisema MwanaFA.


Alisema kinachohitajika kwa sasa ni mashabiki wa kikapu kurudisha mioyo yao katika mchezo huo kwa kujitokeza pindi yanapokuwepo mashindano ili kuwatia hamasa wachezaji.
MwanaFA alisema wao kama serikali wana maagizo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga viwanja viwili vya ndani Dar es Salaam na Dodoma kwa ajili ya kutoa nafasi ya kuandaa mashindano makubwa.

The post MwanaFA aipa neno Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/26/mwanafa-aipa-neno-pazi/feed/ 0
Pazi kufungua pazia East Division https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/pazi-kufungua-pazi-east-division/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/pazi-kufungua-pazi-east-division/#respond Wed, 18 Oct 2023 18:50:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8147 Na mwandishi wetuTimu ya Pazi inatarajiwa kufungua pazia la mashindano ya kikapu ya East Division ya BAL kwa kucheza na Elan Cotton BBC ya Benin katika Uwanja wa Ndani wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa (IST), Dar es Salaam.Mashindano hayo ambayo yanaanza kesho Alhamisi na kumalizika Oktoba 21, yanashirikisha timu nne kutoka Burundi, Kenya, Benin […]

The post Pazi kufungua pazia East Division first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Pazi inatarajiwa kufungua pazia la mashindano ya kikapu ya East Division ya BAL kwa kucheza na Elan Cotton BBC ya Benin katika Uwanja wa Ndani wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa (IST), Dar es Salaam.
Mashindano hayo ambayo yanaanza kesho Alhamisi na kumalizika Oktoba 21, yanashirikisha timu nne kutoka Burundi, Kenya, Benin na Tanzania ambazo zinapambana kupata nafasi moja ya kuwakilisha Kundi C – East Division kwenye Michuano ya Elite 16 ya BAL mwakani.
Timu hizo ni Dynamo (Burundi), KPA (Kenya), Elan Cotton na Pazi ambayo ni mwenyeji wa mashindano hayo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Kadebe alitoa hamasa kwa mashabiki wa Tanzania kwenda kuishangilia Pazi ambao ni mabingwa wa taifa huku ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.
“Njooni mashabiki muishabikie Pazi ikiwa ni timu pekee inayoipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya BAL. Pazi ikishinda, Tanzania imeshinda,” alisema.

The post Pazi kufungua pazia East Division first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/18/pazi-kufungua-pazi-east-division/feed/ 0
Hasheem Thabit arejea Dar kuichezea Pazi https://www.greensports.co.tz/2023/09/26/hasheem-thabit-arejea-dar-kuichezea-pazi/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/26/hasheem-thabit-arejea-dar-kuichezea-pazi/#respond Tue, 26 Sep 2023 12:59:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7853 Na mwandishi wetuMchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabit amerejea nchini Tanzania na kujiunga na timu ya Pazi kwa ajili ya michezo ya hatua za awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (BAL) inayotarajiwa kuchezwa Dar es Salaam kuanzia Oktoba 10 hadi 15, mwaka huu.Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya pili, hatua […]

The post Hasheem Thabit arejea Dar kuichezea Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabit amerejea nchini Tanzania na kujiunga na timu ya Pazi kwa ajili ya michezo ya hatua za awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (BAL) inayotarajiwa kuchezwa Dar es Salaam kuanzia Oktoba 10 hadi 15, mwaka huu.
Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya pili, hatua ya makundi ikiwakilishwa na bingwa wa taifa, Pazi watakaoungana na mabingwa wengine kuwania kucheza hatua ya mtoano katika Kundi D pamoja na Dynamo BC ya Burundi, K.P.A ya Kenya na Sebeta City ya Ethiopia.
Akizungumzia ujio wake Thabiti alisema: “Si mimi pekee, na timu ya Pazi kwa ujumla, lengo langu kubwa kurudi nyumbani ni kuja kufanya kikapu katika kiwango ambacho Tanzania inatakiwa icheze.”
Alisema mashabiki wategemee mabadiliko katika mchezo wa kikapu kwani kwa miaka mingi wanashiriki ila hawafiki mbali na sasa muda umewadia kuonesha kikapu katika kiwango kingine.
Thabit (pichani juu) kabla ya kuanza kucheza kikapu kimataifa na kuwa mchezaji wa kulipwa aliwahi kuzichezea timu za Outsiders na Makongo Sekondari na mwaka 2009 aliingia kwenye Ligi ya Kikapu ya Marekani (NBA) akichezea Memphis Grizzlies.
Thabit alidumu NBA hadi mwaka 2015 akicheza klabu tofauti na mwaka 2017 akajiunga na Yokohama B-Corsairs ya Japan kabla ya baadaye kurejea Marekani kwa mwaka mmoja na kisha akaenda China na sasa yupo The TaiwanBeer HeroBears ya Taiwan.
Wakati huo huo, timu za wanawake za Vijana Queens na JKT Stars zimefuzu kushiriki Ligi ya Wanawake Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Afrika.
Hatua ya awali ya mashindano hayo itachezwa jijini Kigali, Rwanda kuanzia Oktoba 21 mpaka 28 na fainali zitachezwa nchini Misri, Desemba, mwaka huu. Timu hizo zimefuzu moja kwa moja baada ya kufikia hatua ya fainali katika Ligi ya Taifa (NBL 2022).
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linazitakia timu hizo kila la heri kwenye uwakilishi wa kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano hayo.

The post Hasheem Thabit arejea Dar kuichezea Pazi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/26/hasheem-thabit-arejea-dar-kuichezea-pazi/feed/ 0
Ligi ya kikapu Dar kuanza Mei 6 https://www.greensports.co.tz/2023/04/15/ligi-ya-kikapu-dar-kuanza-mei-6/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/15/ligi-ya-kikapu-dar-kuanza-mei-6/#respond Sat, 15 Apr 2023 13:41:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5828 Na mwandishi wetuLigi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL) inatarajiwa kuanza kuunguruma Mei 6, mwaka huu ambapo itashirikisha timu za wanaume na za wanawake ambazo safari hii zitakuwa 12.Akizungumza leo Jumamosi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kamisheni ya Mipango, Maendeleo na Masoko wa Chama cha Kikapu Dar, Terence Mhumbira alisema […]

The post Ligi ya kikapu Dar kuanza Mei 6 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL) inatarajiwa kuanza kuunguruma Mei 6, mwaka huu ambapo itashirikisha timu za wanaume na za wanawake ambazo safari hii zitakuwa 12.
Akizungumza leo Jumamosi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kamisheni ya Mipango, Maendeleo na Masoko wa Chama cha Kikapu Dar, Terence Mhumbira alisema kuwa msimu huu kuna timu mbili za wanawake zimeongezeka na kwamba tayari maandalizi yameshaanza.
Ameeleza kuwa jina la ligi hiyo litabadilika kutoka RBA hadi BDL akisema wameangalia sababu za kibiashara huku wakitarajia ushindani mkubwa kutokana na aina na timu zilizopo na usajili wao.

“Tuko kwenye maandalizi ya ligi ya mkoa wa Dar es Salaam tukitarajia itakuwa ya kiwango cha juu kutokana na timu zilizopo, washiriki wanatakiwa waanze maandalizi ili kuleta ushindani na mwisho wa siku kupata wawakilishi bora wa kushiriki ligi ya taifa,” alisema Mhumbira.


Timu za wanawake zitakazoshiriki ni DB Lioness, JKT Stars, Jeshi Stars, Kurasini Dibas, Mchenga Queens, Pazi Queens, Ukonga Queens, Vijana Queens, UDSM Queens, Polisi Queens, Oilers Princess na Magereza.
Kwa upande wa timu za wanaume ni ABC, Chui, Dar City, DB Oratory, JKT, Jogoo, Mchenga, Mgulani, Oilers, Pazi, Polisi, Savio, UDSM Outsiders, Ukonga Kings, Ukonga Warriors na Vijana City Bulls.

The post Ligi ya kikapu Dar kuanza Mei 6 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/15/ligi-ya-kikapu-dar-kuanza-mei-6/feed/ 0