Burudani - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 06 Dec 2024 08:40:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Burudani - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Albamu ya Bellinger mastaa kibao https://www.greensports.co.tz/2024/12/06/albamu-ya-bellinger-mastaa-kibao/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/06/albamu-ya-bellinger-mastaa-kibao/#respond Fri, 06 Dec 2024 06:28:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12349 Na joseph shaluwaAlbamu mpya ya ‘It’ll All ya Make Sense Later’ ya staa wa muziki nchini Nigeria, Eric Bellinger (pichani) imewashirikisha mastaa kibao akiwemo Burna Boy ambaye anzo ya Muziki ya Grammy.Mastaa wengine walioshirikishwa kwenye albamu hiyo ni mkali wa RnB kutoka Ghana, Gyakie na mastaa wengine wa Nigeria ambao wamepata kushinda Tuzo ya Grammy, […]

The post Albamu ya Bellinger mastaa kibao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na joseph shaluwa
Albamu mpya ya ‘It’ll All ya Make Sense Later’ ya staa wa muziki nchini Nigeria, Eric Bellinger (pichani) imewashirikisha mastaa kibao akiwemo Burna Boy ambaye anzo ya Muziki ya Grammy.
Mastaa wengine walioshirikishwa kwenye albamu hiyo ni mkali wa RnB kutoka Ghana, Gyakie na mastaa wengine wa Nigeria ambao wamepata kushinda Tuzo ya Grammy, Reekado, Banks, Oxlade, Tempoe na Taves.
Bellinger ambaye naye pia amewahi kushinda Tuzo ya Grammy, albamu yake hiyo mpya inapatikana katika mifumo mbalimbali ya kidigitali mitandaoni.
Albamu yake hiyo iliyotengenezwa Cape Town, Afrika Kusini, ndani yake ina mikong’osia ya aina yake yenye ladha za Kiafrika katika mitindo ya R&B, Afrobeats na Amapiano.
Akizungumzia albamu hiyo, Eric anasema: “Nilisafiri hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kutengeneza hii albamu. Hii ni moja ya kazi iliyonipa uzoefu mkubwa sana katika utengenezaji wa muziki.
“Ni kazi nzuri hakika. Inanipa nguvu ya kusonga mbele, kujiamini katika kazi zijazo, ndiyo maana nimeiita hii albamu, ‘It’ll All Make Sense Later’ yaani ‘Italeta Maana Baadaye.
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na wasanii walioshirikishwa kwenye mabano ni Pure, Special (feat. Konshens), Feelings Never Die na Shooting Star (feat. Oxlade).
Nyingine ni Precision (feat. Reekado Banks), Backtrack (feat. Taves), Don’t Shut Off The Lights na For The Evening (feat. Burna Boy).
Vibao vingine ni Ms Africa (feat. Gyakie), Desire, Follow Her Lead, No Coincidence (feat. Geko), Top Dolla (feat. Vscript), Don’t Leave na Unfinished Business.
Wanamuziki wengine aliowahi kupiga nao kolabo ni Usher Raymond, Justin Bieber, Ne-Yo, bila kuwasahau Chris Brown na OG Parker.
Bellinger pia amepata kuandika mashairi ya nyimbo na kuwatayarishia wasanii mbalimbali maarufu duniani.

The post Albamu ya Bellinger mastaa kibao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/06/albamu-ya-bellinger-mastaa-kibao/feed/ 0
Yemi Alade agonga kolabo na Ziggy Marley https://www.greensports.co.tz/2024/08/11/yemi-alade-agonga-kolabo-na-ziggy-marley/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/11/yemi-alade-agonga-kolabo-na-ziggy-marley/#respond Sun, 11 Aug 2024 05:19:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11761 Na Joseph ShaluwaStaa wa muziki wa AfroPop, Yemi Alade (pichani) ametoa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Rebel Queen’ ambayo inapatikana kupitia mtandao wa muziki wa Effyzzie Music.Katika albamu hiyo amewashirikisha nyota kadhaa wa muziki duniani, akiwemo Ziggy Marley ambaye ni mtoto wa mkali wa Regger wa muda wote, Bob Marley.Jina la albamu hiyo […]

The post Yemi Alade agonga kolabo na Ziggy Marley first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Joseph Shaluwa
Staa wa muziki wa AfroPop, Yemi Alade (pichani) ametoa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Rebel Queen’ ambayo inapatikana kupitia mtandao wa muziki wa Effyzzie Music.
Katika albamu hiyo amewashirikisha nyota kadhaa wa muziki duniani, akiwemo Ziggy Marley ambaye ni mtoto wa mkali wa Regger wa muda wote, Bob Marley.
Jina la albamu hiyo ‘Rebel Queen’ ni ushuhuda wa utawala wa Yemi kama Malkia wa Afrika wa AfroPop, mwenye upendo wa dhati kwa bara la Afrika.
“Kuwa mpinzani ni kusafiri katika njia ngumu. Ni kuendelea kuwa mwaminifu kwako mwenyewe hata wakati wa kufanya chaguzi binafsi, bila kujali watu watasemaje,” anasema Yemi.
Wimbo “Peace & Love” aliomshirikisha mwanamuziki wa Jamaica, Ziggy Marley ambaye ni mshindi wa mara 8 wa Grammy, unazidisha ladha ya albamu hiyo.
Kibao cha kwanza kabisa kuachiliwa katika albamu hiyo, kiitwacho ‘Tomorrow’ tayari kimeonesha mafanikio kwani kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuachiwa hewani, kimeshatazamwa na watu zaidi ya milioni 7.5.
Albamu hiyo yenye nyimbo 16 imewashirikisha mastaa wengine wakiwemo, Konshens & Femi One katika ‘Baddie Remix’, Angelique Kidjo katika ‘African Woman’ na Innoss’B katika ‘Lipeka’.
Yemi Alade anasema, “Nilitiwa moyo na muziki wa hadhi ya juu ya Kiafrika… nimetoa albamu hii kwa nia moja tu ya kutengeneza muziki ambao nilikuwa nikiupenda na aina ambayo ninaipenda mpaka sasa.”

The post Yemi Alade agonga kolabo na Ziggy Marley first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/11/yemi-alade-agonga-kolabo-na-ziggy-marley/feed/ 0
Idris Sultan aing’arisha Bridgerton https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/idris-sultan-aingarisha-bridgerton/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/idris-sultan-aingarisha-bridgerton/#respond Wed, 22 May 2024 07:47:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11066 Na Joseph ShaluwaStaa wa burudani kutoka Tanzania, Idris Sultan (pichani) ameng’arisha ujio mpya wa tamthiliya ya Bridgerton, katika onesho kabambe lililowakusanya nyota daraja la kwanza kutoka Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla.Onesho hilo lilifanyika mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini, ambapo Netflix, waandaaji wa series hiyo, walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton.Msimu wa […]

The post Idris Sultan aing’arisha Bridgerton first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Joseph Shaluwa
Staa wa burudani kutoka Tanzania, Idris Sultan (pichani) ameng’arisha ujio mpya wa tamthiliya ya Bridgerton, katika onesho kabambe lililowakusanya nyota daraja la kwanza kutoka Afrika Mashariki na bara la Afrika kwa ujumla.
Onesho hilo lilifanyika mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini, ambapo Netflix, waandaaji wa series hiyo, walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton.
Msimu wa tatu wa Bridgerton unatarajiwa kurushwa na Netflix na kushuhudiwa na ulimwengu mzima ambapo tayari sehemu ya kwanza imeshaoneshwa na sehemu ya pili itaoneshwa Juni 13, mwaka huu.
Katika onesho hilo, walihudhuria mastaa wakubwa kutoka nchi za Kenya, Tanzania (Idris), Nigeria, Ghana, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini, wakiongozwa na Adjoa Andoh (ambaye amecheza kama Lady Aga kwenye Bridgerton) akiwa kama mgeni wa heshima.
Mkali wa kurapu free style, kutoka Afrika Kusini ambaye amependekezwa kwenye Tuzo za Grammy, Musa Keys naye aliungana na mastaa wenzake katika hafla hiyo.
Mbali na Idris mastaa wengine kutoka Afrika Mashariki walioalikwa katika onesho hilo la kijanja ni pamoja na komediani na mtayarishaji maudhui, Elsa Majimbo.
Wengine kutoka Kenya ni staa wa filamu Catherine Kamau (Kate), Amina Abdi Rabar na waigizaji mahiri Manasseh Nyagah na Jackie Matubia.
Wanamitindo maarufu wa Nairobi: Brian Babu na Lady Mandy pia walihudhuria, ambapo kwa pamoja walihusika katika kubuni na kutengeneza mavazi ya mastaa waliohudhuria.

The post Idris Sultan aing’arisha Bridgerton first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/idris-sultan-aingarisha-bridgerton/feed/ 0
Pogba ageukia uigizaji filamu https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/pogba-ageukia-uigizaji-filamu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/pogba-ageukia-uigizaji-filamu/#respond Mon, 06 May 2024 06:17:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10856 Paris, UfaransaKiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba yuko katika harakati za uigizaji wa filamu iliyopewa jina la 4 Zeros ambayo inatarajia kutolewa Aprili mwakani.Pogba, nyota aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya Ufaransa kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne kwa kosa […]

The post Pogba ageukia uigizaji filamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba yuko katika harakati za uigizaji wa filamu iliyopewa jina la 4 Zeros ambayo inatarajia kutolewa Aprili mwakani.
Pogba, nyota aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya Ufaransa kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli.
Filamu anayoigiza Pogba ni mwendelezo wa filamu ya awali y 3 Zeros ambayo ilitolewa mara ya kwanza mwaka 2002 na habari zaidi zinadai kwamba sehemu ambayo inahusika kuigiza filamu hiyo ni katika jiji la Paris.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Pogba ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31, katika filamu hiyo anaigiza kama kocha wa timu ya soka ya vijana,
Kuhusu sakata la dawa za kusisimua misuli, mchezaji huyo alisema kwamba hajawahi kutumia dawa hizo kwa makusudi na ameikatia rufaa adhabu hiyo ambayo alipewa Februari mwaka huu.
Rufaa ya Pogba itasikilizwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) na kama atafanikiwa katika rufaa hiyo huenda adhabu aliyopewa ya miaka minne ikapunguzwa.

The post Pogba ageukia uigizaji filamu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/06/pogba-ageukia-uigizaji-filamu/feed/ 0
Msiba wa Gardner wamgusa Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2024/04/22/msiba-wa-gardner-wamgusa-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/22/msiba-wa-gardner-wamgusa-rais-samia/#respond Mon, 22 Apr 2024 07:37:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10697 Na mwandishi wetuRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wafanyakazi wa Clouds Media kutokana na kifo cha mtangazaji mahiri, Gardner G Habash.Gardner, 50, aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media alifariki duniani Jumamosi akiwa anapatiwa matibabu ya shinikizo la damu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete […]

The post Msiba wa Gardner wamgusa Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wafanyakazi wa Clouds Media kutokana na kifo cha mtangazaji mahiri, Gardner G Habash.
Gardner, 50, aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media alifariki duniani Jumamosi akiwa anapatiwa matibabu ya shinikizo la damu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Katika salamu zake, Rais Samia alimtaja Gardner kuwa ni mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye ustawi wa sekta ya habari nchini na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema.
Gardner ambaye pia ni baba mzazi wa msanii wa bongofleva, Malkia Karen, habari za kuugua kwake ziliwahi kuzungumzwa mapema mwezi huu ingawa haikuwekwa wazi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani.
Wakati wa uhai wake, Gardner alijipatia umaarufu zaidi kupitia kipindi cha Jahazi ambacho alikiongoza vyema na kubatizwa jina la Captain, jina ambalo lilizoeleka zaidi miongoni mwa mashabiki wa kipindi hicho.
Akiwa na George Bantu, Mussa Hussein na kabla ya hapo Epharim Kibonde ambaye pia alifariki dunia, kwa pamoja wamekifanya kipindi cha Jahazi kinachorushwa kuanzia saa 12 jioni kuwa kimbilio la wasikilizaji wengi wa redio nchini Tanzania.
Kipindi cha Jahazi kimeendelea kuwa maarufu kwa namna ambavyo watangazaji wake wamekuwa wakionesha umahiri na weledi katika utangazaji pamoja na umakini katika kuchambua mikasa na matukio mbalimbali ya kijamii ya ndani na nje ya nchi.
Gardner anaagwa leo Jumatatu na wakati wa jiji la Dar es Salaam kwenye viwanja wa Leaders Club na kuzikwa kesho Jumanne, Tarakea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

The post Msiba wa Gardner wamgusa Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/22/msiba-wa-gardner-wamgusa-rais-samia/feed/ 0
Cobhams agonga kolabo na Sauti Sol https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/cobhams-agonga-kolabo-na-sauti-sol/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/cobhams-agonga-kolabo-na-sauti-sol/#respond Sat, 17 Feb 2024 18:30:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9775 Na Joseph ShaluwaMsanii maarufu nchini Nigeria, Cobhams Asuquo (pichani) ameshirikiana na kundi maarufu nchini Kenya la Sauti Sol kwenye video inayokwenda kwa jina la ‘Lady Fiona’.Cobhams ambaye pia ni mwandishi wa mashairi na mtayarishaji muziki, ameunganisha nguvu na miamba ya muziki nchini Kenya, Sauti Sol ambao wameshikilia tuzo ya kundi bora la muziki wa Afro-Pop, […]

The post Cobhams agonga kolabo na Sauti Sol first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Joseph Shaluwa
Msanii maarufu nchini Nigeria, Cobhams Asuquo (pichani) ameshirikiana na kundi maarufu nchini Kenya la Sauti Sol kwenye video inayokwenda kwa jina la ‘Lady Fiona’.
Cobhams ambaye pia ni mwandishi wa mashairi na mtayarishaji muziki, ameunganisha nguvu na miamba ya muziki nchini Kenya, Sauti Sol ambao wameshikilia tuzo ya kundi bora la muziki wa Afro-Pop, Kenya.
Huu ni ushirikiano mzuri wa kimataifa unaowakutanisha miamba ya muziki barani Afrika na kuunganisha pamoja sauti zao tamu zinazotoa burudani ya aina yake kwa hadhira.
“Lady Fiona” ni wimbo wa aina yake wenye mahadhi ya Afro-pop, unaotoa nafasi ya ubunifu wa wasanii hawa – Cobhams Asuquo na Sauti Sol,” inaeleza sehemu ya taarifa kwa vyombo vya habari.
Ni wimbo unaowafanya wasikilizaji wazame katika ulimwengu wa mahaba na kuibua hisia zinazoweza kumpata mtu yeyote ambaye amepitia furaha au magumu katika mahusiano ya kimapenzi.
“Ombi letu kubwa kwa mashabiki wa muziki ni kuitazama video hiyo ambayo tayari inapatikana mitandaoni. Hapo ukweli wa haya tunayosema utathibitika,” ilihitimisha taarifa hiyo.

The post Cobhams agonga kolabo na Sauti Sol first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/17/cobhams-agonga-kolabo-na-sauti-sol/feed/ 0
Olori aachia albamu chini ya Davido https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/olori-aachia-albamu-chini-ya-davido/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/olori-aachia-albamu-chini-ya-davido/#respond Tue, 13 Feb 2024 19:36:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9713 Na Joseph ShaluwaStaa wa muziki nchini Nigeria, Logos Olori ametoa albamu yake fupi (EP) akiwa chini ya lebo ya mwanamuziki nyota nchini humo, Davido.EP hiyo inaonesha jinsi ambavyo Olori ameamua kuja kwa makali zaidi baada ya panda shuka katika gemu, mwaka uliopita wa 2023.Katika kunogesha utamu zaidi kwenye EP hiyo, Olori amepiga kolabo na Davido […]

The post Olori aachia albamu chini ya Davido first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Joseph Shaluwa
Staa wa muziki nchini Nigeria, Logos Olori ametoa albamu yake fupi (EP) akiwa chini ya lebo ya mwanamuziki nyota nchini humo, Davido.
EP hiyo inaonesha jinsi ambavyo Olori ameamua kuja kwa makali zaidi baada ya panda shuka katika gemu, mwaka uliopita wa 2023.
Katika kunogesha utamu zaidi kwenye EP hiyo, Olori amepiga kolabo na Davido katika wimbo “Easy On Me” na Musa Keys kwenye “Hmm Hmm”.
Mbali na nyimbo hizo alizowashirikisha Davido na Musa Keys, nyimbo nyingine ni Olori, Push It, My Darling, Apapa na Murder zinazokamilisha nyimbo saba.
Akizungumzia project hiyo, Olori anasema: “Jiunge nami katika safari hii, tunaposafiri huku tukiwa na furaha ya ala na mitikisiko ya kila namna ya burudani. Kuanzia ngoma za Apapa hadi nyimbo tamu za Olori, kila wimbo una tukio lake mahususi.
“Huyu ndiye Logos Olori, msanii huru, anayebadilika kulingana na kila ngoma. Ni kama maji yatiririkayo, huwa yanabadilika kila wakati yanapochukua maumbo na hali tofauti katika safari. Tuko huru na lengo ni kuwa huru siku zote.”

The post Olori aachia albamu chini ya Davido first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/13/olori-aachia-albamu-chini-ya-davido/feed/ 0
Mr Eazi akamilisha ‘Evil Genius’ https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/mr-eazi-akamilisha-evil-genius/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/mr-eazi-akamilisha-evil-genius/#respond Wed, 22 Nov 2023 07:44:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8572 Na Joseph ShaluwaMsanii nyota wa Afropop, Mr Eazi, ameachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.Video za albamu hiyo imechukuliwa katika maeneo ya miji ya nchi tofauti kama, Ouidah na Cotonou nchini Benin, Kigali, Rwanda, Accra na Kokrobite, Ghana, Lagos, Nigeria, London, Uingereza na Los Angeles […]

The post Mr Eazi akamilisha ‘Evil Genius’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Joseph Shaluwa
Msanii nyota wa Afropop, Mr Eazi, ameachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.
Video za albamu hiyo imechukuliwa katika maeneo ya miji ya nchi tofauti kama, Ouidah na Cotonou nchini Benin, Kigali, Rwanda, Accra na Kokrobite, Ghana, Lagos, Nigeria, London, Uingereza na Los Angeles na New York, Marekani.
Albamu hiyo ‘The Evil Genius’ huangazia baadhi ya kazi za kibinafsi za Mr Eazi, anapozama kwa kina katika mada kama vile mapenzi, usaliti, upweke na familia, zinazoonyeshwa kupitia vitendo vitatu tofauti.
Washiriki katika kazi hiyo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Angelique Kidjo (Benin), Tekno (Nigeria), Efya (Ghana), Whoisakin (Nigeria), Joeboy (Nigeria), na washindi mara tatu wa Grammy Soweto Gospel Choir (Afrika Kusini).
Kwa upande wa watayarishaji, walikuwa pamoja na Kel-P (Nigeria), Knucks (U.K.), Michael Brun (Haiti), Andre Vibez (Nigeria), Yung Willis (Nigeria), Nonso Amadi (Nigeria/Canada), KillBeatz (Ghana), M.O.G Beatz (Ghana), E Kelly (Nigeria), Type A (Nigeria), Stikmatik (U.K.), Phantom (Nigeria), Beat Butcha (U.K.), Venna (U.K.), KDream (Nigeria) na Mr Eazi mwenyewe.
Katika kuonyesha Mr Eazi ni mwamba wa kuchanganya ladha, ndani yake yupo staa kutoka Afrika Mashariki nchini Kenya, Alphonce Odhiambo maarufu Alpha ODH ambaye amemshirikisha kwenye kibao ‘Advice’.
Kwa upande wa usanifu wa jalada la albamu hiyo, Mr Eazi alishirikiana na mwanamitindo maarufu wa Nigeria, mbunifu na mpiga picha Daniel Obasi, anayejulikana kwa kazi nzuri alizowafanyia mastaa Beyoncé na Louis Vuitton.

The post Mr Eazi akamilisha ‘Evil Genius’ first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/mr-eazi-akamilisha-evil-genius/feed/ 0
Afro B aachia video ya Wo wo wo https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/afro-b-aachia-video-ya-wo-wo-wo/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/afro-b-aachia-video-ya-wo-wo-wo/#respond Wed, 22 Nov 2023 07:40:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8569 Msanii aliyetambuliwa na ngoma ya Afrowave ‘Drogba’, Afro B, ameachia video yake mpya ya kibao ‘Wo Wo Wo’ ikiwa ni kolabo na Mmarekani, Rich The Kid na msanii wa muziki wa rap nchini Uingereza, Rimzee.Afro B (pichani) ni raia wa Ivory Coast ambaye kwa sasa makazi yake yapo nchini Uingereza katika Jiji la London ametoa […]

The post Afro B aachia video ya Wo wo wo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Msanii aliyetambuliwa na ngoma ya Afrowave ‘Drogba’, Afro B, ameachia video yake mpya ya kibao ‘Wo Wo Wo’ ikiwa ni kolabo na Mmarekani, Rich The Kid na msanii wa muziki wa rap nchini Uingereza, Rimzee.
Afro B (pichani) ni raia wa Ivory Coast ambaye kwa sasa makazi yake yapo nchini Uingereza katika Jiji la London ametoa kolabo hiyo yenye hadhi ya kimataifa kwa kuwa inajumuisha mastaa kutoka mabara tofauti ulimwenguni.
Kabla ya kibao hiki, msanii huyo amepata kufanya kazi na mastaa wengine wa muziki wakiwemo, Wizkid, Slim Jxmmi (Rae Sremmurd), DJ Snake, Sukihana na wengineo.
Tangu wakati huo, amepata kuungwa mkono na Billboard, BET, BBC Radio 1, Capital, Hot 97, Power 105 na The Fader, Rolling Stone & NME.
“Mambo makubwa yanakuja, huu ni mwanzo tu, mashabiki wangu wakae mkao wa kula,” anasema Afro B akizungumzia kazi yake hiyo mpya.

The post Afro B aachia video ya Wo wo wo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/22/afro-b-aachia-video-ya-wo-wo-wo/feed/ 0
MwanaFA amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mwanafa-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mwanafa-amshukuru-rais-samia/#respond Wed, 01 Mar 2023 06:15:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5339 Na mwandishi wetuMbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma au MwanaFA amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuwataka wasanii na wanamichezo kufanya kazi kwa mikono yao.MwanaFA ambaye ni mwanamuziki mkongwe nchini ni miongoni mwa uteuzi uliotangazwa Jumapili hii na Rais Samia kabla ya kula kiapo Jumatatu akichukua […]

The post MwanaFA amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma au MwanaFA amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuwataka wasanii na wanamichezo kufanya kazi kwa mikono yao.
MwanaFA ambaye ni mwanamuziki mkongwe nchini ni miongoni mwa uteuzi uliotangazwa Jumapili hii na Rais Samia kabla ya kula kiapo Jumatatu akichukua nafasi ya Pauline Gekul aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao kijamii wa Instagram, MwanaFA aliweka ujumbe huo wa shukrani kwa Rais sambamba na kuwasihi wadau wa wizara hiyo kwenda kufanya kazi kwa bidii.

“Wanautamaduni,wasanii na wanamichezo wa nchi hii, muda ndio huu jamaa zangu, twendeni tukafanye mambo yetu kwa mikono yetu wenyewe, Mungu ametoa kibali,” alisema MwanaFA


“Namshukuru sana Rais Samia kwa imani hii kubwa aliyonipa kijana wake, ina maana kubwa mno na naahidi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu nisimuangushe.
“Nawashukuru pia wananchi wenzangu wa Muheza kwa imani na ushirikiano mkubwa wanaoendelea kunipatia. Muheza ni ya watu magwiji watupu,” aliandika FA.

The post MwanaFA amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/01/mwanafa-amshukuru-rais-samia/feed/ 0