BongoMovie - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 21 Nov 2022 08:09:54 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg BongoMovie - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Tesa aanza kumgeuka Nicole https://www.greensports.co.tz/2022/11/21/tesa-aanza-kumgeuka-nicole/ https://www.greensports.co.tz/2022/11/21/tesa-aanza-kumgeuka-nicole/#respond Mon, 21 Nov 2022 08:09:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3864 Na Jonathan HauleKatika Filamu ya Huba juma lililopita tuliona jinsi, Tesa alivyoanza kumgeuka na kuwa mkali kwa Nicole, ambaye kimsingi ni rafiki yake wa ‘dharura’, rafiki aliyekuwa akimtumia ili kuvuruga penzi ya Happy kwa JB, tajiri anayejua kupenda na kutumia pesa.Tukio la mwisho juma lililopita lilidhihirisha hali hiyo baada ya Tesa kumkoromea Nicole ambaye alifika […]

The post Tesa aanza kumgeuka Nicole first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule
Katika Filamu ya Huba juma lililopita tuliona jinsi, Tesa alivyoanza kumgeuka na kuwa mkali kwa Nicole, ambaye kimsingi ni rafiki yake wa ‘dharura’, rafiki aliyekuwa akimtumia ili kuvuruga penzi ya Happy kwa JB, tajiri anayejua kupenda na kutumia pesa.
Tukio la mwisho juma lililopita lilidhihirisha hali hiyo baada ya Tesa kumkoromea Nicole ambaye alifika nyumbani kwake alale ili wakiwa pamoja waangalie namna ya kuyajenga kwa lengo la kumalizia kazi ya kumuondoa Happy kwa JB lakini Tesa akawa amebadilika na kuwa mkali.
Kitendo cha Tesa kumtimua Nicole kinaanza kujibu swali la muda mrefu na la msingi kuhusu urafiki wa wa wawili hawa ambao uliunganiswa na mkakati haramu wa kumtoa Happy kwa JB, mkakati ulioanzia kwa kufanikisha zoezi la kumtorosha Chidi, mume wa Happy kwenye kambi ya shamba la mananasi, ukafuatiwa na mkakati wa kumpeleka Chidi kwa Happy ili Happy aachane na JB.
Yote hayo yamefanyika lakini Happy bado hajatoka kwa JB, je kitendo cha Tesa kumkoromea Nicole na kumfukuza kwake kinaashiria kukata tamaa kwamba mpango umeshafeli na hivyo Nicole hana tena umuhimu kwake au Tesa kashanza kuona dalili za kufanikisha kumtoa Happy na hivyo hahitaji tena ushoga na Nicole.
Yote kwa yote kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kadhaa, urafiki wa Nicole na Tesa ni sawa na tukio la dharura, kila mmoja ana ugomvi moyoni mwake dhidi ya mwenzake, kiini cha ugomvi huo ulioko mioyoni mwa kila mmoja wao ni tajiri JB ambaye amewahi kuwaonjesha wote jeuri yake ya pesa kabla ya Happy kuingilia kati na kugeuka adui yao wote.
Swali ambalo pengine linaweza kuanza kupata jibu Jumatatu hii ni hatma ya ushoga wa wawili hawa hasa baada ya mkakati wa kumtoa Happy kwa JB kuonekana kuwa mgumu. Je kila mtu atashika lake au Tesa atabaini kwamba bado anamhitaji Nicole kama ambavyo bado anamhitaji JB.
Tima naye licha ya kuandamwa na jinamizi la huba kati ya Dev na Jude, kabla hajamaliza yake kaamua kuingilia sakata la Happy na Chidi, anaamua kumsaidia Chidi ili waweze kumtoa Happy kwa JB, safari yake kwa JB inafanikiwa baada ya kuingia ndani na kumkuta Happy ambaye bila aibu anamdhihirishia namna alivyonogewa na huba la JB. Kwa alichokishuhudia, Tima anajiaminisha kwamba Happy kwa JB kafika, ni vigumu kutoka kwa ajili ya Chidi.
Hapo hapo mtoto wa pekee wa JB, Nelly naye hafurahii uhusiano wa baba yake na Happy, anaamua kumdhihirishia Happy namna asivyompenda na asivyomkubali kwa kumtolea kauli za dharau, hapo hapo anamtuhumu kwa kuhusika kuondoka kwa Habiba.
Ugomvi wa wawili hawa ni tukio jingine la mfano wa mtoto na ‘mama yake wa kambo’ ambalo linainogesha Filamu ya Huba na kuacha maswali ya je Nelly ataweza kumheshimu Happy ambaye licha ya kuwa ni mpenzi wa baba yake lakini kwake anamuona kuwa ni kero iliyoletwa na baba yake katika nyumba yao.
Roy na Doris nao huba lao limechukua sura mpya, Roy anagundua ushirikina aliofanyiwa na mkwewe Bi Sikitu kwa kuwekwa kwenye chupa, anakuwa mnyonge baada ya kubaini hilo, hapo hapo bado anateswa na kitendo cha mkewe kwenda Pemba bila ruhusa yake. Yote hayo yanaendelea wakati Nandi tayari ana mtoto jambo ambalo halijamfurahisha Doris, mke mwenza wa Nandi.
Nini hatma ya familia hii ambayo nayo imevurugwa na mahaba huku ushirikina ukionekana kupewa nafasi kubwa? Kuanzia Jumatatu hii mengi yatajulikana.
Kibibi, mwanamke mwingine aliyefanikiwa kwa namna ya kipekee kuubeba uhusika wa ujasiri, ukatili na ujeuri katika Filamu ya Huba, anafanikisha mpango wa kumtoa jela Fabrizo, mlinzi na msaidizi wake mwenye kujua siri nyingi za Kibibi na ambaye baadaye uhusiano wao haukuwa mzuri.
Katika tukio hili Kibibi anadhihirisha nguvu ya mwanamke katika huba, anafanikiwa kumpeleka Fabrizo hotelini na kukaa naye pamoja usiku kucha, asubuhi anaamka na kujikagua, jibu analipata kwamba kuna kosa amelifanya, anajuta lakini anaamua kujipa matumaini kwa imani kwamba azma yake ya kumtuliza Fabrizo inaanza kutimia.
Tukio zima la Kibibi na Fabrizo nalo linaacha maswali kwamba nini kitaendelea baina yao hasa kwa kuwa tayari Fabrizo alionyesha kuchukizwa na baadhi ya mambo ya Kibibi, je tayari amelainika na kusahau yote yaliyopita na kuwa mtiifu kwa Kibibi ambaye kuna kila dalili kwamba kumtoa Fabrizo jela hajakufanya hivi hivi tu bali kuna kitu anataka.
Dev, mpenzi wa Kibi naye anahaha kumtuliza Kibibi, anafanya kila analodhani kuwa ni sahihi ili kufanikisha hilo lakini Kibibi bado anaendelea kumfanya kama mtumishi wake wa ndani, anampa hadhi na heshima kwa muda mfupi hasa anapokuwa na matatizo, baada ya hapo anamuonyesha jinsi alivyo katili na jeuri.
Kupotea kwa Carlos nalo ni tukio jingine lenye utata na linaloacha maswali, nini kitamkuta Carlos? ataangamizwa kama walivyofanywa walinzi wengine wa JB na vipi kuhusu JB na mizimu, nani atakayeangamizwa au kutolewa kafara ili awe sadaka kwa mizimu? Majibu yote haya yataanza kupatikana kuanzia Jumatatu hii.

The post Tesa aanza kumgeuka Nicole first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/11/21/tesa-aanza-kumgeuka-nicole/feed/ 0
JB ahisi Happy anamsaliti https://www.greensports.co.tz/2022/11/13/jb-ahisi-happy-anamsaliti/ https://www.greensports.co.tz/2022/11/13/jb-ahisi-happy-anamsaliti/#respond Sun, 13 Nov 2022 18:18:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3719 Na Jonathan HauleKatika Filamu ya Huba wiki hii, tumeona jinsi JB, tajiri katili asiyevumilia usaliti alivyoanza kutilia shaka mahaba ya Happy kwake, anahisi kuna kitu kibaya kinaendelea, hapo hapo anaamua kumpa tahadhari Happy kwamba kwake kusalitiwa ni jambo lisilokubalika.Hisia za kwamba anasalitiwa zinamjia JB wakati akiwa kwenye mjengo wake wa kifahari, anamwita Happy katika namna […]

The post JB ahisi Happy anamsaliti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule
Katika Filamu ya Huba wiki hii, tumeona jinsi JB, tajiri katili asiyevumilia usaliti alivyoanza kutilia shaka mahaba ya Happy kwake, anahisi kuna kitu kibaya kinaendelea, hapo hapo anaamua kumpa tahadhari Happy kwamba kwake kusalitiwa ni jambo lisilokubalika.
Hisia za kwamba anasalitiwa zinamjia JB wakati akiwa kwenye mjengo wake wa kifahari, anamwita Happy katika namna ya kimahaba lakini katika hali ya kushangaza Happy hajibu chochote, JB anaamua kumfuata juu ghorofani na ghafla wanakutana ana kwa ana.
Happy anaonesha hali ya wasiwasi ambayo JB anaishtukia na kumuuliza kulikoni, Happy anababaika na ghafla anapata jibu la kumlainisha JB kwamba alikuwa anataka kumfanyia ‘suprise’ lakini kwa sababu ametokea mpango huo umekwama, JB bado anahisi kitu lakini hatimaye anakubali shingo upande.
Wakati yote hayo yakiendelea, Carlos na Chidi mume wa Happy wameamua kumfuata Happy kwenye makazi ya JB, Carlos tayari ameingia ndani na Happy anafanikiwa kumlaghai JB amsuburi chumbani ili amfanyie suprise.
Happy anatumia mwanya huo kuzungumza na Carlos ili aweze kutoka nje ya mjengo wa JB huku akimtadharisha kwamba anaweza akapoteza uhai, Carlos anakubaliana na Happy, anaondoka na kukutana na Chidi aliyekuwa nje akimsubiri.
Kwa sehemu ambayo Filamu ya Huba imeishia ni wazi kwamba kila mfuatiliaji atataka kujua nini hatma ya mapenzi kati ya Happy na JB baada ya JB kuanza kumtilia shaka, je JB hajamuona Carlos ndani ya mjengo wake ambao una ulinzi? Nini hasa kimemfanya JB aanze kujiwa na hisia za kusalitiwa na Happy? Ni wasiwasi ule ule aliouonyesha Happy au kuna kingine ambacho JB amekigundua?
Na vipi kuhusu ‘suprise’ ambalo Happy amedai kupanga kumfanyia JB, Je atakuja na mpango wowote unaoeleweka katika hilo au atashindwa kuja na kitu kipya na kujikuta akimfanya JB aamini alichokuwa akikihisi kuhusu kusalitiwa?
Katika matukio yote ya Filamu ya Huba kwa wiki iliyopita, JB pamoja na kula maraha akiwa na Happy kwenye hoteli ya kifahari lakini mara kadhaa alionekana akiwa mnyonge na mwenye kuwaza japo kwa muda mfupi, bila shaka aliwaachia watazamaji swali kwamba nini kilikuwa kikimtatiza hadi kuwa mnyonge katikati ya maraha yake na Happy.
Jibu la kilichokuwa kikimtatiza JB pengine kilipatikana baada ya kumuua kikatili mlinzi wake kwa kummwagia mafuta na kumchoma. Kitendo hicho kinaendelea kudhihirisha ukatili wa JB kwenye Filamu ya Huba, licha ya kufikisha ujumbe wa tajiri mwenye kupenda starehe lakini sehemu ya moyo pia kumejaa dhambi ya ukatili kwani huyo si mlinzi wa kwanza kumuua.
Matukio yote hayo yanaweza kumfanya mtazamaji wa filamu hii kuanza kujiuliza nini kitamkuta Happy iwapo JB atajiridhisha kwamba anamsaliti na vipi akigundua kwamba Carlos aliingia nyumbani kwake na kupata muda wa kuzungumza na Happy na kama hiyo haitoshi akafikia hatua ya kumchungulia binti wa JB Nelly akiwa chumbani kwake. Je jumba la tajiri linaweza kukosa CCTV Camera?
Pengine maswali hayo yote na mengineyo yanaweza kupata majibu kuanzia Jumatatu hii kwenye mfululizo wa Filamu ya Huba.
Katika sakata hilo hilo la JB, mwanamke katili Tesa bado haamini kama ameachwa na JB na chanzo cha yote hayo ni Happy, anaendelea na harakati za kuhakikisha anavuruga mahusiano ya Happy na JB kwa kumtumia Chidi na Carlos. Nini atakifanya baada ya mpango wa kwanza kufeli huku Chidi akionyesha dalili kama vile ameshaanza kukata tamaa?
Hapo hapo swali la msingi na la muda mrefu linabaki pale pale kwamba iwapo JB ataachana na Happy, Tesa ataingia mjengoni? Na vipi kuhusu Nicole, je yeye hataki kuwa mpenzi wa tajiri JB? Swali hilo kwa mtazamaji huenda linaibua dalili za ugomvi mkubwa kati ya Nicole na Tesa siku zijazo.
Mwanamke mwengine katili, Kibibi naye anaendelea kuivuruga akili ya mpenzi wake Dev, ukatili wa Kibibi unampa wakati mgumu Dev ambaye anamhoji mtumishi wa ndani wa Kibibi kuhusu namna mtu aliyetaka kumbaka mtumishi huyo alivyouawa kikatili na Kibibi.
Ukali ambao Kibibi anamuonyesha Dev unatoa dalili zote kwamba huenda wawili hao wakatengana, na ikitokea hivyo Dev atakwenda wapi, atarudi kwa Roy ingawa mke wa Roy, Doris hamtaki au ataamua kujisalimisha kwa Tima ambaye alimfukuza, vipi kuhusu kurudi kwa Tesa ambaye ni mama yake japo haonekani kumkubali?
Roy naye bado mambo yake hayaeleweki kwa Doris, ameonyesha udhaifu kwa kushindwa kumzuia mkewe asiende Pemba lakini hapo hapo mama mkwe Bi Sikitu naye anamuonyesha Roy ukali baada ya Roy kuzidi kuhoji kitendo cha mkewe kwenda Pemba. Nini hatma ya Doris ambaye tayari amefika Pemba na vipi kuhusu Roy, nini atakifanya baada ya mkewe kwenda Pemba? Je atakubali yaishe?

The post JB ahisi Happy anamsaliti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/11/13/jb-ahisi-happy-anamsaliti/feed/ 0
Penzi la JB, Happy mtegoni https://www.greensports.co.tz/2022/11/06/penzi-la-jb-happy-mtegoni/ https://www.greensports.co.tz/2022/11/06/penzi-la-jb-happy-mtegoni/#respond Sun, 06 Nov 2022 18:39:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3609 Na Jonathan Haule, Katika Filamu ya Huba juma hili tumeona jinsi mtego wa Tesa ulivyofanikiwa, hatimaye Chidi anakutana na mkewe Happy ana kwa ana nyumbani kwa JB.Chidi anaonyeha hali ya kuchanganyikiwa baada ya kumuona Happy na kujaribu kuwa mkali akisaidiwa na Carlos katika kuwatisha Happy na JB lakini muda mfupi baadaye Chidi ananywea na kuwa […]

The post Penzi la JB, Happy mtegoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule,

Katika Filamu ya Huba juma hili tumeona jinsi mtego wa Tesa ulivyofanikiwa, hatimaye Chidi anakutana na mkewe Happy ana kwa ana nyumbani kwa JB.
Chidi anaonyeha hali ya kuchanganyikiwa baada ya kumuona Happy na kujaribu kuwa mkali akisaidiwa na Carlos katika kuwatisha Happy na JB lakini muda mfupi baadaye Chidi ananywea na kuwa mnyonge, anaanza kumbembeleza Happy ili aachane na JB.
Wakati yote hayo yakiendelea, Tesa anaonyesha furaha yake na kuanza kumsakama JB kwa maneno ya dhihaka akimshangaa mtu mzima kuingilia ndoa za watoto wadogo.
Cheko la Tesa linamuibua Nelly, binti wa pekee wa tajiri JB, Nelly anamshangaa Tesa kwa kicheko cha dharau na kuhoji nini hasa kilichomfanya acheke namna hiyo, kauli ya Nelly inamuibua Nicole ambaye anamtetea Tesa kwa namna alivyocheka na kumtaka Nelly anyamaze kama haoni cha kucheka.
Wakati yote hayo yakiendelea JB anaonekana kuwa kimya wakati Happy akijisogeza mithili ya mtoto wa swala mwenye hofu ya kuvamiwa na fisi, anajiweka karibu zaidi na JB ambaye wakati yote hayo yakiendelea amekuwa kimya.
Kimya cha JB kinaacha maswali, ni kama vile yupo mtegoni, anasoma mazingira kabla ya kuchukua maamuzi. Je nini atakifanya kwa Happy, na nini atakifanya kwa Chidi na Carlos, na nini atakifanya kwa Nicole na Tesa ambao wote ni kama wavamizi waliovamia nyumbani kwake?
Sehemu ya utamu wa Filamu ya Huba itaanzia hapo, maswal yote hayo au baadhi yake hapana shaka majibu yake yatapatikana Jumatatu hii usiku.
Hapo hapo bado kuna swali kuhusu Nicole na Tesa, wote wanajua raha ya kuwa na JB, mpenzi tajiri, tena tajiri anayejua kudhihirisha jeuri ya fedha zake pale anapopenda, hakuna kati yao anayefurahia kulikosa penzi la aina hiyo ambalo Happy mtu wanayemuona hana hadhi hiyo ndiye aliyechaguliwa na JB kulifurahia penzi la aina hiyo.
Katika mazingira yote hayo swali ambalo halijapata jibu juma lililopita linaendelea kubaki vile vile, swali hilo ni je urafiki wa Tesa na Nicole ambao kimsingi unaweza kusema ni urafiki wa dharura, utadumu iwapo JB ataamua kuachana na Happy? Au wataingia katika vita mpya ya kumtaka JB?
Dave naye bado yuko njia panda kama ndugu yake Roy, uamuzi wake wa kwenda kujituliza kwa Kibibi umekuwa mgumu, Kibibi anamapenzi yasiyoeleweka lakini kubwa ni ukali na ukatili ambao amekuwa akiudhihirisha kwa Dave, licha ya kulala chumba kimoja na kuonekana akiji-baby-isha kwa Dave lakini hakuchelewa kumgeuka na kumdhihirishia alivyo mwanamke mbabe asiyechezewa.
Mazingira hayo yanamfanya Dave azidi kuchanganyikiwa na hatimaye anaamua kumrudia Tima lakini hapo hapo anakutana na mtihani mwingine, Nelly hatimaye anaamua kutumia ushirikina pengine kwa lengo la kumtoa Dave kwa Tima, anachinja kuku wa kienyeji mwenye madoadoa na kumuweka kwenye geti la kuingia nyumbani kwa Tima, pengine ni kwa maelekezo ya mganga wa kienyeji.
Katika hali ambayo haikutarajiwa Dave anakutwa eneo hilo hilo akiwa amemshika kuku huyo katika hali ya mshangao, ghafla Tima naye anafungua geti lake na kumkuta Dave akiwa amemshika kuku huyo na moja kwa moja anaamini Dave ndiye aliyemuweka kuku eneo hilo.
Dave anafukuzwa kama mwizi nyumbani kwa Tima, anaamua kuondoka akiwa katika hali ya unyonge na aliyevurugwa kwa kuhusishwa na ushirikina ambao hakuufanya.
Nini hatma ya Dave na Tima? Je Tima atamsamehe kwa sababu tusisahau ukweli kwamba anampenda, na je Dave atafanya nini baada ya Tima kumfukuza, ataendelea kujishikiza kwa Kibibi au ataamua aende kwa Nelly ambaye pia anampenda sana Dave na haoni wala hasikii.
Dave katika Filamu ya Huba amefanikiwa kufikisha ujumbe wa mwanaume aliyevurugwa na wapenzi na ambaye pia amekosa msimamo.
Kwa Doris na mama yake Bi Sikitu nako hali inazidi kuwa tete, Doris bado hana amani baada ya kusikia mke mwenzake Nandi ana mtoto, anatangaza azma yake ya kwenda Pemba jambo ambalo Bi Sikitu licha ya kubobea katika ushirikina lakini anamuonya kwamba Pemba si mchezo, anamtaka asijaribu kwenda kwa sababu waganga wa Pemba si mchezo.
Dorisi anaamua kumpuuza mama yake na kusisitiza kwamba lazima aende Pemba, mumewe Roy naye ni kama vile ameshindwa kumzuia mkewe asiende Pemba. Je nini kitatokea kuhusu mpango wa Doris, na je mumewe Roy atafanya nini? Ni majibu ambayo yataanza kupatikana kuanzia Jumatatu hii.

The post Penzi la JB, Happy mtegoni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/11/06/penzi-la-jb-happy-mtegoni/feed/ 0
Happy aibiwa, ahongwa simu kali https://www.greensports.co.tz/2022/10/30/happy-aibiwa-ahongwa-simu-kali/ https://www.greensports.co.tz/2022/10/30/happy-aibiwa-ahongwa-simu-kali/#respond Sun, 30 Oct 2022 14:36:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3503 Na Jonathan HauleFilamu ya Huba inazidi kunoga, Happy anaendelea kufurahia huba la JB, ameshaonyeshwa jinsi wenye pesa zao wanavyokula raha, ameingizwa katika ‘mjengo’ wa hadhi, amelalia kitanda cha hadhi, amepelekwa hoteli ya hadhi lakini hapo hapo anaibiwa simu yake na kuhongwa simu ya bei kali. …Kwa Happy, JB anafanya kila awezalo kumthibitishia mambo mawili muhimu, […]

The post Happy aibiwa, ahongwa simu kali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule
Filamu ya Huba inazidi kunoga, Happy anaendelea kufurahia huba la JB, ameshaonyeshwa jinsi wenye pesa zao wanavyokula raha, ameingizwa katika ‘mjengo’ wa hadhi, amelalia kitanda cha hadhi, amepelekwa hoteli ya hadhi lakini hapo hapo anaibiwa simu yake na kuhongwa simu ya bei kali. …
Kwa Happy, JB anafanya kila awezalo kumthibitishia mambo mawili muhimu, moja kumthibitishia kuwa yeye ni tajiri mwenye pesa lakini pili ni namna anavyompenda, hapo hapo kete yake kuu anayoitumia kudhihirisha mapenzi yake kwa Happy ni uwezo wake kifedha. Happy, kama lilivyo jina lake anafurahia kuwa mpenzi wa mtu mwenye pesa zake.
Katika jeuri ya fedha, JB anam-suprise Happy kwa simu mpya ya bei mbaya, Happy anaipokea simu lakini anakuwa na maswali kuhusu kupotea kwa simu yake, hapo hapo JB anampa jibu kwamba ameitupa na ndio maana kamnunulia mpya ya hadhi, jambo ambalo halijamfurahisha Happy lakini anaipokea simu mpya ya hadhi.
Baadaye inabainika kwamba JB aliichukua simu ya Happy na kuanza kuikagua, ni dhahiri kwamba anaweza kukutana na ujumbe wa Chidi au Tesa au Nicole ambao kimsingi wote hao kwa sasa ni maadui zake, je nini atakifanya iwapo atakutana na kitu kisichomfurahisha kwenye simu ya Happy.
Yote hayo yanaendelea huku waliokimbiwa na JB wakizidi kupamba moto katika kutaka kulipa kisasi au kumtoa Happy kwa JB, wakati Happy akifurahi kama lilivyo jina lake. Tesa naye anateseka kama lilivyo jina lake, hataki kuamini kama yeye na JB wamefika mwisho.
Tesa amefanikiwa kumtoa Chidi kambini kwenye mashamba ya mananasi na tayari Chidi ameshaambiwa kwamba mkewe Happy yuko na JB.
Nini Chidi atafanya, bado ni swali gumu lililojificha kwenye Filamu ya Huba, swali ambalo huenda jibu lake likaanza kupatikana Jumatatu lakini hapo hapo kuna swali kuhusu Tesa, nini atakifanya iwapo mpango wa kumtoa Chidi kambini utashindwa kuja na majibu aliyoyakusudia. Je atakubali mambo yaishe au ataanzisha vita nyingine.
Kwa namna Tesa alivyoigiza katika Filamu ya Huba ni dhahiri kwamba hatokuwa mtu wa kukata tamaa, atafanya kila liwezekanalo kumtoa Happy kwa JB, Je atakuja na mbinu gani? Je atamtoa Happy duniani kama alivyomfanya Kashaulo, mtu ambaye aliingia katika anga zake? Nini hatma ya Happy.
Kwa upande mwingine Kibibi anaendelea kudhihirisha ukatili wake, anaua mtu aliyetaka kumuiba mtoto wake na bila ajizi anamwambia Dave kuhusu tukio hilo, Dave anashtuka na kujawa hofu lakini baadaye anaamua kumdadidi mtumishi wa ndani wa Kibibi ambaye alikwenda na Kibibi kuwasaka waliotaka kumuiba mtoto wa Kibibi.
Hapo hapo Dave na mtu wake wa karibu, Roy, wote wana matatizo na wapenzi wao lakini kila mmoja anamuonea huruma mwenzake na kumuona ndiye mwenye hali mbaya zaidi, Roy anamsikitia Dave kwa jinsi anavyohaha na kushindwa kuwa na msimamo, akiyumba mbele ya Kibibi, Tima na Nelly. Dave naye anamsikitikia Roy anavyoyumbishwa na Doris na Bi Sikitu ambaye ni mama mkwe wake.
Taarifa za Nandi, mpenzi mwingine wa Roy kupata mtoto zinamvuruga Doris ambaye ametengeneza huba zito kwa Roy akitumia nguvu za giza kumfanya Roy asiwe na la kusema mbele yake. Nini hatma ya watu watatu hawa yaani Bi Sikitu, Roy na Doris hasa baada ya Nandi kupata mtoto?
Dave naye akiwa bado amehifadhiwa nyumbani kwa Kibibi, anajikuta akipata mgeni ambaye ni Tima, mpenzi wake waliyetengana na kumfanya ahamie kwa Kibibi. Tima kaamua liwalo na liwe, licha ya kusumbuliwa na mumewe Jude aliye gerezani lakini akili yake ipo kwa Dave, anachukua uamuzi mgumu wa kumfuata Dave nyumbani kwa Kibibi.
Wakati Tima amechukua uamuzi huo, mauaji anayodaiwa kufanya Kibibi yanamtesa Dave, ameanza harakati za kutaka kujua ni kweli Kibibi ameua mtu aliyetaka kuiba mtoto wake? Mauaji hayo yanamuogopesha Dave lakini Kibibi anaoanyesha jinsi alivyo mwanamke katili na asiyejali.
Wakati Dave akimhoji mtumishi wa Kibibi ghafla kengele inaita, wote wanashtuka kwa kudhani ni Kibibi aliyepiga kengele lakini kumbe aliyepiga kengele ni Tima.
Je nini atakifanya Kibibi iwapo ikitokea akamkuta Tima nyumbani kwake? Ataanza kumkabili Tima au Dave na kisha kumfukuza au atawafukuza wote jambo ambalo bila shaka Tima atalifurahia? Na vipi kuhusu Nelly ambaye naye hajakata na haonekani kukata tamaa kwa Dave?

The post Happy aibiwa, ahongwa simu kali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/10/30/happy-aibiwa-ahongwa-simu-kali/feed/ 0
Huba feki la Nicole lamlainisha Bambo https://www.greensports.co.tz/2022/10/23/huba-feki-la-nicole-lamlainisha-bambo/ https://www.greensports.co.tz/2022/10/23/huba-feki-la-nicole-lamlainisha-bambo/#respond Sun, 23 Oct 2022 12:41:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3396 Na Jonathan HauleKatika Filamu ya Huba wiki hii, Nicole anafanikisha kazi aliyopewa na Tesa ya kuhakikisha anamtoa Chidi katika mashamba ya mananasi baada ya kumlainisha Bambo, lengo ni kumkutanisha Chidi na mkewe Happy ili kumuondoa Happy kwa JB.Katika kulifanikisha hilo, Nicole anajaribu kumdanganya Bambo ambaye ni msimamizi wa mashamba hayo kwamba Carlos amefiwa na mama […]

The post Huba feki la Nicole lamlainisha Bambo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule
Katika Filamu ya Huba wiki hii, Nicole anafanikisha kazi aliyopewa na Tesa ya kuhakikisha anamtoa Chidi katika mashamba ya mananasi baada ya kumlainisha Bambo, lengo ni kumkutanisha Chidi na mkewe Happy ili kumuondoa Happy kwa JB.
Katika kulifanikisha hilo, Nicole anajaribu kumdanganya Bambo ambaye ni msimamizi wa mashamba hayo kwamba Carlos amefiwa na mama yake ili aruhusiwe pamoja na Chidi kuondoka katika mashamba hayo lakini Bambo anahisi kitu na kukataa kuwaruhusu wote wawili.
Bambo pamoja na ugumu aliounyesha lakini hapo hapo anaonyesha ‘udhaifu wa kiume’ anahamasika baada ya kumuona Nicole, anamtamani na hatimaye anakubali lakini anauliza na yeye atafaidika na nini kwa kutoa ruhusa kwa Chidi na Carlos kuondoka.
Nicole anaubaini udhaifu wa Bambo na hatimaye anaamua kutumia ‘nguvu ya kike’ kumlainisha Bambo kwa huba feki, Bambo anaingia kwenye mtego wa Nicole, anatomaswa na kujikuta akichanganyikiwa na kuanza kucheka hovyo mithili ya mtu aliyewehuka akili, wakati hayo yakiendelea, Nicole anamrekodi kwa simu yake na dakika chache baadaye anamuonyesha picha zake na kumtishia kuzirusha mitandaoni.
Bambo anaingia hofu, kwa shingo upande anajikuta akilazimika kuwaruhusu Chidi na Carlos waondoke katika mashamba hayo ili kuficha aibu ambayo inaweza kumkuta.
Wakati yote hayo yakiendelea, upande wa pili Happy anazidi kunogewa na huba la JB, mjengo wa kifahari wa JB sasa unakuwa kama mali yake na yeye anakuwa kama mama mwenye nyumba, anaonekana kitandani kwa JB akijirusha na kumlalia JB mgongoni.
Mambo yote hayo ya Happy yanazidi kumkera Nelly, mtoto wa pekee wa JB ambaye anafikia hatua ya kumkoromea baba yake, bado haoni kama Happy ni mtu sahihi kuwa mpenzi wa baba yake, anafanya kila anachokifanya lakini wakati wote JB haonyeshi kutetereka na zaidi ya yote anamwambia kweupee kwamba Happy ndio chaguo lake.
Wakati Nelly akikosa raha, Happy ni mwingi wa furaha, anafikiria atakavyopanda ndege kwa mara yake ya kwanza baada ya kupewa ahadi hiyo na JB.
Mwisho wa yote, Happy anaomba ruhusa kwa JB ili aende alipokuwa akiishi, JB hataki aende peke yake, anaamua kumpeleka kwa usafiri wa hadhi ya mpenzi wa tajiri lakini wakati anafika, Chidi na Carlos nao wanawasili kwenye nyumba hiyo hiyo.
Utamu wa Filamu ya Huba unaanzia hapo, nini kitatokea Jumatatu, Happy atakapokutana na Chidi, je atakubali ‘kulikimbia furushi la pesa’ ili tu abaki na Chidi wake ambaye amekuwa na hamu naye kwa muda mrefu huku akimkumbuka mara kwa mara?
Na je iwapo tamaa ya pesa itamfanya Happy aachane na Chidi, nini atakifanya Chidi baada ya kuachwa? Na je Happy akiamua anarudi kwa Chidi wake na kuachana na JB, nini atakachofanya JB ukizingatia ukweli kwamba ni mtu anayeamini katika nguvu ya pesa pamoja na michezo michafu ya ushirikina?
Na vipi kuhusu Tesa na Nicole iwapo watamtenganisha Happy na JB nani kati yao atakayekuwa mpenzi wa JB? Je huo hauwezi kuwa mwanzo mpya wa ugomvi baina yao kwa kugombea furushi la pesa (JB)? Hapana shaka kila mtazamaji wa Filamu ya Huba atakuwa mwenye kusubiri majibu ndani ya filamu hii.
Kingine kinachosubiriwa kuanzia Jumatatu hii ndani ya Filamu ya Huba ni hatma ya Tima na Judi, ni kama vile Tima hataki kusikia habari za mpenzi wake huyo ambaye kwa sasa ni mfungwa lakini Judi hajaacha kumsumbua siku hadi siku.
Hapo hapo kuna suala zima la Kibibi na Dev, wapenzi hawa ambao wamejikuta wakirudiana katika mazingira ya ajabu ajabu baada ya Kibibi kupata matatizo ya kumpoteza mtoto wake na hatimaye akashirikiana na Dev katika kumtafuta mtoto huyo.
Nini hatma ya penzi lao baada ya Kibibi kumpata mtoto wake, ataendelea kuwa na Dev au atarudi nyuma na kukumbuka jinsi Dev alivyomsukuma kwenye bwawa la kuogelea akiwa na nguo zake wakati akijaribu kumtaka warudiane na Dev kutokuwa tayari hasa akikumbuka mateso aliyopewa na Kibibi.
Na vipi kuhusu Roy ambaye inaonekana wazi kwamba mpenzi wake Doris amemuendea kwa Sangoma ili asiwe na sauti kwenye familia yake ingawa kwa mbali Roy anaonekana kama akili zinaanza kumrudia kwa namna ambavyo ameanza kuhoji baadhi ya mambo.
Visa hivyo na vinginevyo ni kati ya mambo yanayoinogesha filamu hii na ndio maana kila anayeifuatilia anajikuta akiwa mwenye shauku ya kutaka kujua nini kitakachofuata.

The post Huba feki la Nicole lamlainisha Bambo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/10/23/huba-feki-la-nicole-lamlainisha-bambo/feed/ 0
Happy afurahia huba la JB, Tesa ateseka https://www.greensports.co.tz/2022/10/17/happy-afurahia-huba-la-jb-tesa-ateseka/ https://www.greensports.co.tz/2022/10/17/happy-afurahia-huba-la-jb-tesa-ateseka/#respond Mon, 17 Oct 2022 10:52:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3285 Na Jonathan HauleKatika Filamu ya Huba, Happy, kama lilivyo jina lake ameanza kufurahia huba la JB baada ya kujawa hofu siku za mwanzo, hapo hapo Tesa mwanamke jasiri anayeamini kuwa ndiye mwenye hadhi ya kuwa na JB akiteseka kama lilivyo jina lake baada ya kuachwa…Ilipofika Filamu ya Huba juma hili ni mwendelezo wa visa vyenye […]

The post Happy afurahia huba la JB, Tesa ateseka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule
Katika Filamu ya Huba, Happy, kama lilivyo jina lake ameanza kufurahia huba la JB baada ya kujawa hofu siku za mwanzo, hapo hapo Tesa mwanamke jasiri anayeamini kuwa ndiye mwenye hadhi ya kuwa na JB akiteseka kama lilivyo jina lake baada ya kuachwa…
Ilipofika Filamu ya Huba juma hili ni mwendelezo wa visa vyenye utata katika mahaba miongoni mwa wahusika wa filamu hii ambao kwa kiasi kikubwa wameendelea kudhihirisha namna wanavyofanikisha kufikisha ujumbe wa visa hivyo kama lilivyo jina la filamu yenyewe.
Wakati Happy akianza kufurahia huba na utajiri wa JB, Tesa anajikuta akiwa mnyonge, anapoteza ujasiri na ubabe wote aliojipamba nao katika filamu hii, chozi linamtoka, anajawa hasira, hatimaye anamalizia hasira zake kwa Mzee Mwinyi na mkewe ambao amewapa hifadhi nyumbani kwake, anawafokea kwa makosa yasiyoeleweka, na kama hiyo haitoshi anaamua kuwatimua akiwataka warudi kijijini.
Happy kwa upande wake ameanza kuonjeshwa jeuri ya pesa za JB, amewekewa watu maalum wa kumpa mavazi ya uhakika ili kumfanya afanane na mwanamke mwenye kuishi maisha ya kifahari, awe na hadhi ya mpenzi wa tajiri JB.
JB hajawa nyuma katika kuonyesha jeuri ya pesa, hataki Happy tena atumie usafiri mwingine zaidi ya usafiri wa hadhi, apelekwe anakotaka na dereva au JB ampeleke mwenyewe. Zaidi ya hilo JB pia anajipanga kwenda naye Dodoma katika shughuli zake za kibiashara.
Tesa hajakubaliana na kinachoendelea kati ya Happy na JB, anaamua kumshirikisha Nicole ambaye kama Tesa naye ameporwa JB, ni wanawake wawili wanaougulia maumivu ya kuporwa bwana, wanajipanga kuunganisha nguvu dhidi ya Happy, msichana ambaye Nicole ndiye aliyemuongoza katika mambo yote ya ukahaba lakini akafikia hatua ya kumpiku kwa JB, tajiri mpenda totoz.
Kuungana kwa Nicole na Tesa ni tukio mojawapo linalomfanya mfuatiliaji wa filamu hii kusubiri kwa hamu kuanzia Jumatatu hii na kuendelea ili kujua nini kitatokea kati ya Tesa na Nicole dhidi ya Happy, na nini atakifanya JB iwapo Nicole na Tesa wataamua kuunganisha nguvu na kumkabili Happy? Na je ni mbinu gani watakayokuja nayo Nicole na Tesa dhidi ya Happy?
Hapo hapo kila mtu atapenda kujua nini hatma ya Happy na Chidi, wapenzi wawili ambao licha ya umaskini wao lakini walikuwa na huba lisilotia shaka kabla Happy hajaingia katika ukahaba na kuangukia kwa JB na taratibu ameanza kumsahau Chidi, mtu wake ambaye awali alikuwa akimuulizia mara kwa mara.
Vipi mpango wa Chidi kutoroka kwenye kambi anakofanya shughuli za kilimo, mpango ambao tayari umevurugwa na Carlos licha ya awali kulipigania suala la kutoroka na kumshirikisha Chidi, lakini kubwa linalomtesa Chidi ni pale zinapomjia kumbukumbu za Happy.
Mwanamama mwingine jeuri na mwenye pesa zake, Kibibi hatimaye anaelekea kusalimu amri kwa Devi licha ya ukali na maneno ya kijeuri aliyokuwa akimtolea wakati Devi akijaribu kurudisha penzi lao la zamani, awali hakukuwa na dalili zozote za Kibibi kumkubali Devi lakini taratibu ameanza kulegea, ama kweli penzi halina jemedari, anamlilia Devi na kumueleza matatizo yaliyomkuta.
Walipofikia Devi na Kibibi ni vigumu kuamini kwamba ni Kibibi huyu huyu aliyekuwa akimuangalia Devi kwa jicho la dharau na kumsikiliza kwa namna ya kutojali nini anasema, kumlaza sebuleni kwenye kochi lakini sasa kinachoonekana ni kama vile ile hadithi ya hakuna mkate mgumu mbele ya chai taratibu inaanza kujidhihirisha. Kuanzia Jumatatu bila shaka tutaona mengi ya wawili hawa. Je Kibibi ataanza kumbadilikia Devi au Devi ataendelea kumtuliza kama ambavyo tayari kafanikiwa kumtuliza?
Nelly, mtoto pekee wa JB naye ni kama amechanganywa kwa kitendo cha baba yake kuingia katika mahusiano na Happy, anajaribu kumdodosa Happy lakini kabla hajafika mbali anakubali ukweli ambao haupendi na haumfurahishi kwamba baba yake haoni hasikii kwa Happy na hivyo kwake hana ujanja zaidi ya kukubali kwamba Happy sasa anakuwa kama mama yake.
Mfungwa Judi pamoja na kuwa jela lakini akili yake bado haijatoka kwa Tima, haachi kumuwaza mara kwa mara licha ya kwamba Tima hana mpango naye, katika matukio ya wawili hao Judi anajawa hasira kwa anachojua kwamba Tima ametoa mimba yake na hivyo anaamua kumfanyia visa vya kila aina huku akiendelea kutumikia kifungo gerezani.
Tima hakubaliani na Judi, anapinga hoja ya kutoa mimba, anaamua kumfuata jela na hapo hapo inatokea tafrani baina ya wawili hao, Judi akishikilia msimamo wake kwamba Tima ametoa mimba yake.
Mbali na kuvurugwa na Judi, Tima pia hana amani baada ya penzi lake na Devi kusambaratika licha ya matumaini makubwa aliyokuwa nayo kwa Devi hasa baada ya Judi kufungwa na Devi kutibuana na Kibibi na hivyo Tima akawa kimbilio pekee la Dvi.
Devi anayepigiwa hesabu na Tima kwa sasa kitu pekee anachofanya ni kupigania kulirudisha penzi lake kwa Kibibi jambo ambalo tayari ameanza kulifanikisha na hivyo nafasi ya Tima haipo.
Visa hivyo na vinginevyo vingi vikiwamo vya kishirikina vinavyohusisha mambo ya mahaba ni kati ya matukio yanayoipamba Filamu ya Huba. Tukutane juma lijalo kwa muendelezo wa uchambuzi wa filamu hii iliyojaa visa vya kusisimua…

The post Happy afurahia huba la JB, Tesa ateseka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/10/17/happy-afurahia-huba-la-jb-tesa-ateseka/feed/ 0
Mahaba yenye utata katika Filamu Huba https://www.greensports.co.tz/2022/10/09/mahaba-yenye-utata-katika-filamu-huba/ https://www.greensports.co.tz/2022/10/09/mahaba-yenye-utata-katika-filamu-huba/#respond Sun, 09 Oct 2022 17:43:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=3169 Na Jonathan HauleKwa anayeitazama Filamu ya Huba kupitia DSTV, bila shaka jambo mojawapo linamlovutia ni namna wahusika wanavyouvaa vyema uhusika pamoja na mpangilio wa matukio hasa visa vyenye utata wa mahaba.Katika filamu hii kwanza JB ameendelea kudhihirisha unguli wake katika tasnia, kila eneo alilohusika amejitahidi kuuvaa uhusika kikamilifu. Kwenye Huba amefanikiwa kuiteka hadhira kwa namna […]

The post Mahaba yenye utata katika Filamu Huba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Jonathan Haule
Kwa anayeitazama Filamu ya Huba kupitia DSTV, bila shaka jambo mojawapo linamlovutia ni namna wahusika wanavyouvaa vyema uhusika pamoja na mpangilio wa matukio hasa visa vyenye utata wa mahaba.
Katika filamu hii kwanza JB ameendelea kudhihirisha unguli wake katika tasnia, kila eneo alilohusika amejitahidi kuuvaa uhusika kikamilifu. Kwenye Huba amefanikiwa kuiteka hadhira kwa namna anavyoigiza tajiri mwenye pesa chafu na ambaye anajua kuzitumia pesa kwa warembo.
Jumba analoishi, nguo anazovaa, fimbo anayotembelea, gari analotumia, aina ya mazungumzo yake, wasaidizi wake kuanzia mlinzi na wasaidizi wengine wa nyumbani, vyote vinakupa picha ya tajiri fulani hivi mwenye pesa chafu na anayejua kuipa roho kitu inataka lakini pia mwenye imani za kishirikina.
Hapo hapo anadhihirisha alivyo tajiri katili asiyetaka kuchezewa na aliye tayari kufanya lolote inapobidi kufanya hivyo, kitendo cha kumuua mlinzi wake na kutoa maagizo ya kutaka maini ya mlinzi huyo yatolewe kinadhihirisha ukatili wa JB katika Filamu Huba.
Nje ya hayo Huba inadhihirisha namna JB anavyojua kupenda na hata kulaghai wanawake, fimbo kubwa inayomuwezesha kufanikisha hayo ni jeuri ya pesa lakini anapomtaka mwanamke haoni tabu kujishusha ili tu azma yake itimie.
Amelidhihirisha hilo kwa Tesa, mwanamke ‘single mother’ mwenye uwezo wake kifedha lakini mwenye sifa ya kiburi na ukatili, Kashaulo aliingia kwenye anga zake, hakumchelewesha, akamuondoa duniani. Ugomvi wake na JB ulitarajiwa kuwa tukio kubwa ndani ya Filamu ya Huba lakini mwisho wa siku Tesa akatulizwa na kuangukia kwenye himaya ya JB.
Baada ya Tesa kuwapangua walinzi na kuingia kibabe kwenye mjengo wa kifahari wa JB, akaanza kumchamba na kumpayukia maneno makali akimtaka aache kuwasakama ma-single mother. Nini alikifanya JB baada ya kumwagiwa maneno ya shombo na mwanamke, ilitarajiwa angejibu mapigo, ilikuwa kama tajiri amedhalilishwa na kushushiwa heshima yake.
JB hakurusha ngumi, hakujibu kwa maneno ya shombo, alichofanya ni kudhihirisha kwamba mwanaume wa kweli hashindwi lolote mbele ya mwanamke hata awe mkali kama simba.
Alitulia, akacheka cheko la kitajiri, kisha akamsifia kwa ujasiri aliouonyesha, akamtaka akae atulie apate kinywaji. Nini kilifuata? Tesa anashtuka asubuhi akiwa kwenye kitanda cha kifahari cha JB, asielewe imekuwajekuwaje, akawa mfano wa mtu aliyekumbwa na mfadhaiko wa akili. Huyo ndiye JB anayejua kuuvaa uhusika kwenye filamu.
Wakati Tesa akijiaminisha kwamba JB ni Tesa na Tesa ni JB, ghafla utata wa kimahaba unaibuka, Tesa anagundua kwamba Nicole naye yupo kwenye himaya ya JB, anakabiliana na Nicole na kuonekana kumaliza utata huo anabaini kwamba Happy, msichana asiye na kipato cha uhakika na wa hadhi ya chini naye kaingia kwenye himaya ya JB.
Kama hilo halitoshi, Tesa anabaini kwamba cheni ya dhahabu aliyojiaminisha kwamba amenunuliwa na JB kwa Sh 950,000 haikuwa yake, badala yake anavalishwa Happy mbele yake.
Hadi hapo Tesa anajiona amepigwa tukio, hasira zinampanda japo anajilazimisha kucheka kinafiki, anajaribu kupambana lakini JB anambadilikia kweupee, tena mbele ya Nelly ambaye ni mtoto wa pekee wa JB na ambaye pia analazimisha penzi kwa Devi, mtoto wa Tesa huku Tesa akishabikia penzi hilo pengine kwa imani kwamba itamrahishia kila kitu kwa JB.
Nini atakifanya Tesa baada ya kumkuta kilichomkuta, bila shaka kila mfuatiliaji anasubiri kwa hamu kujua nini kitatokea Jumatatu kwenye mjengo wa kifahari wa JB katika mfululizo wa Filamu ya Huba.
Ukiachana na Tesa kwenye Filamu ya Huba pia yupo, Kibibi huyu ni mwanamke mwingine ambaye si haba naye kauvaa vyema uhusika, ana kipato cha maana lakini amepambwa na sifa ya ujeuri, kiburi na ukatili na aliye tayari kuua na kufuta ushahidi kwa jeuri ya pesa kama alivyomfanyia Miraji.
Pamoja na yote hayo, Kibibi naye anajikuta katika utata wa mahaba, anasumbuliwa na tukio la kuachwa na Devi, anajaribu kumrudisha Devi kwenye himaya yake, Devi hataki hasa anapokumbuka mateso aliyowahi kupewa na Kibibi, mwishowe anaishia kumsukuma Kibibi kwenye bwawa la kuogelea akiwa na nguo zake.
Devi hata hivyo kwa sasa yamemkuta anaamua kujirudisha kwa Devi baada ya kutendwa na Tima mke wa Judi, anaingia nyumbani kwa Kibibi na kulazwa sebuleni, anamlazimisha Kibibi warudiane si tu ili wawe wapenzi bali pia apate pa kuishi, Nini kitatokea kati ya wawili hawa, ni utata wa kimahaba unaoweza kupata jibu Jumatatu katika mfululizo wa Filamu ya Huba.
Kibibi naye pamoja na ukatili na kiburi chake anapambwa na utata mwingine wa kimahaba, ni vipi alikubali kuwa mpenzi wa Chidi hadi kupata naye mtoto, ni mtu wa hadhi ya chini mno, hana lolote la kujivunia kuwa na hadhi ya kutoka na Kibibi lakini Filamu ya Huba imelitumia vyema tukio hilo pengine kudhihirisha kinachosemwa kwamba penzi halina jemedari.
Kwa ujumla Filamu ya Huba mbali na kuanika mahaba yaliyotawaliwa na utata, pia ni kielelezo kimojawapo cha ukomavu katika Bongomovie, ni filamu ambayo imefuta kasoro nyingi tulizokuwa tukizishuhudia miaka ya nyuma kwenye tasnia ya filamu.
Ukomavu unaonekana kwa waigizaji, mpangilio wa matukio na visa, maeneo yanayotumiwa kuigiza kuanzia nyumba, hoteli na kwingineko na kama hiyo haitoshi hata vingereza tunavyovisikia katika filamu hii si kama ilivyokuwa siku za nyuma, kwenye Huba vingereza havitumiki hovyo hovyo, badala yake vinatumika kuonyesha ‘msisitizo.’

The post Mahaba yenye utata katika Filamu Huba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/10/09/mahaba-yenye-utata-katika-filamu-huba/feed/ 0