reddeath - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 May 2024 19:26:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.7 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg reddeath - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Man Utd haitarajii kumuuza Rashford https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/man-utd-haitarajii-kumuuza-rashford/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/man-utd-haitarajii-kumuuza-rashford/#respond Wed, 01 May 2024 19:26:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10805 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United haitarajii kupata ofa yoyote ya kumuuza mshambuliaji wake, Harry Kane ikiamini kwamba hakuna klabu ambayo itakuwa tayari kumpandia dau mshambuliaji huyo.Katika siku za karibuni zimekuwapo habari kwamba klabu hiyo ina mpango wa kuwapiga bei baadhi ya mastaa wake huku Rashford naye akitajwa katika mpango huo lakini habari mpya ni kwamba […]

The post Man Utd haitarajii kumuuza Rashford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United haitarajii kupata ofa yoyote ya kumuuza mshambuliaji wake, Harry Kane ikiamini kwamba hakuna klabu ambayo itakuwa tayari kumpandia dau mshambuliaji huyo.
Katika siku za karibuni zimekuwapo habari kwamba klabu hiyo ina mpango wa kuwapiga bei baadhi ya mastaa wake huku Rashford naye akitajwa katika mpango huo lakini habari mpya ni kwamba klabu hiyo haioni sababu ya kumpunguza mshambuliaji huyo.
Man United inaamini na inatambua kwamba ni klabu ya PSG ya Ufaransa pekee inayoweza kuwasilisha ofa ya kumtaka Rashford lakini haitokuwa tayari kulipa kiwango cha mshahara wa mchezaji huyo.
Zaidi ya hilo, Man United pia inatambua kwamba japo PSG imekuwa ikimtaka mshambuliaji huyo lakini haiamini kwamba anaweza kuwa mbadala wa Kylian Mbappe ambaye zipo habari kwamba anajiandaa kujiunga na Real Madrid baada ya msimu huu.
Msimu huu umekuwa mgumu kwa Rashford akiwa hadi sasa amefunga mabao tisa tu katika mashindano yote lakini Man United haipo tayari kuona akiondoka kwa dau kupunguzwa badala yake inaona bora aendelee kubaki katika timu hiyo.
Mchezaji mwengine ambaye majaliwa yake Man United hayajawekwa sawa ni Mason Greenwood ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo Getafe ya Hispania akiwa akiwa katika msimu wake wa kwanza na tayari ameifungia mabao 10.
Greenwood, 22, ambaye alikuwa akiandamwa na kesi ya udhalilishaji ambayo hata hivyo ilifutwa Februari mwaka jana kwa kukosekana ushahidi na baadhi ya mashahidi kujitoa, huenda naye akauzwa jumla au kurudishwa kikosini.

The post Man Utd haitarajii kumuuza Rashford first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/01/man-utd-haitarajii-kumuuza-rashford/feed/ 0
Kesi za ubakaji zamuandama Mendy https://www.greensports.co.tz/2021/11/17/kesi-za-ubakaji-zamuandama-mendy/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/17/kesi-za-ubakaji-zamuandama-mendy/#respond Wed, 17 Nov 2021 11:41:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=469 Manchester, England Beki wa Manchester City, Benjamin Mendy amehusishwa na makosa mengine mawili ya ubakaji na moja ya udhalilishaji kijinsia.Mendy mwenye umri wa miaka 27 anatarajia kuripoti katika mahakama ya Stockport leo Jumatano na sasa atakuwa akikabiliwa na makosa sita ya ubakaji baada ya manne ya awali sambamba na moja la udhalilishaji kijinsia.Mashtaka hayo yanatokana […]

The post Kesi za ubakaji zamuandama Mendy first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England

Beki wa Manchester City, Benjamin Mendy amehusishwa na makosa mengine mawili ya ubakaji na moja ya udhalilishaji kijinsia.
Mendy mwenye umri wa miaka 27 anatarajia kuripoti katika mahakama ya Stockport leo Jumatano na sasa atakuwa akikabiliwa na makosa sita ya ubakaji baada ya manne ya awali sambamba na moja la udhalilishaji kijinsia.
Mashtaka hayo yanatokana na matukio ambayo yanadaiwa kufanywa na mchezaji huyo kati ya Oktoba 2020 na Agosti mwaka huu yakihusisha wanawake wawili tofauti wa umri unaozidi miaka 16 na msichana mmoja wa umri chini ya miaka 18.
Mendy ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, amekuwa akiiwakilisha vyema Man City tangu mwaka 2017 alipojiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Msimu ulioipita Mendy alishiriki vyema katika mafanikio ya timu hiyo hadi kutwaa taji la Ligi Kuu England lakini tangu ahusishwe na tuhuma hizo klabu yake imemsimamisha ikisubiri upelelezi wa polisi ukamilike.

The post Kesi za ubakaji zamuandama Mendy first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/17/kesi-za-ubakaji-zamuandama-mendy/feed/ 0
Stars yashindwa kutamba nyumbani https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/stars-yashindwa-kutamba-nyumban/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/stars-yashindwa-kutamba-nyumban/#respond Thu, 11 Nov 2021 15:59:22 +0000 https://greensports.co.tz/?p=443 i Na mwandishi wetuMabao matatu ya DR Congo yameiwezesha timu hiyo kutoka kifua mbele kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Taifa Stars katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Taifa Stars.Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Stars iliuanza mchezo kwa kasi na kuisumbua DR […]

The post Stars yashindwa kutamba nyumbani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
i

Na mwandishi wetu
Mabao matatu ya DR Congo yameiwezesha timu hiyo kutoka kifua mbele kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Taifa Stars katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Taifa Stars.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Stars iliuanza mchezo kwa kasi na kuisumbua DR Congo ambao katika kipindi cha kwanza walicheza wakionekana kama wanausoma mchezo wa Stars.
Pamoja na Stars kuanza kwa kasi lakini walikuwa ni DRC waliofanya shambulizi la maana na kupata bao katika dakika ya tano lililofungwa na nyota wa klabu ya Lens ya Ufaransa, Gael Kakota aliyefumua shuti lililomshinda kipa Aishi Manula.
Bao hilo halikuwatoa mchezoni Stars kwani wakiongozwa na nahodha wao, Mbwana Samatta na Simon Msuva waliendelea kuisumbua ngome ya DRC lakini hadi mapumziko DRC walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Juhudi za Stars kusaka bao zilikatishwa tamaa katika dakika ya 65 baada ya Idumba Fasika anayekipiga Afrika Kusini katika klabu Cape Town City kuandika bao la pili ambalo lilizidi kupoteza matumaini ya Stars kutoka nyumbani na ushindi.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Stars ambayo katika mechi ya kwanza na DRC ugenini ilitoka sare ya bao 1-1 ilijikuta ikilala kwa bao la tatu katika dakika ya 85 lililofungwa na Ben Maiango anayeichezea Raja Casablanca ya Morocco.
Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwachanganya hadi mashabiki ambao baadhi walianza kutoka nje ya uwanja huku DRC ambao sasa wanaongoza kundi J wakiwa na pointi nane wakicheza taratibu na kupoteza muda.
Stars inabaki na pointi zake saba wakati mechi nyingine ya kundi hilo itachezwa baadaye leo kati ya Benin na Madagascar.
Katika mechi nyingine ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia, mahasimu wa Afrika Mashariki, Kenya na Uganda waliumana na kutoka sare ya bao 1-1.

The post Stars yashindwa kutamba nyumbani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/stars-yashindwa-kutamba-nyumban/feed/ 0
Sugu akumbuka alivyopigania hakimiliki https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/sugu-akumbuka-alivyopigania-hakimiliki/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/sugu-akumbuka-alivyopigania-hakimiliki/#respond Thu, 11 Nov 2021 11:00:39 +0000 https://greensports.co.tz/?p=422 Na mwandishi wetu Msanii wa miondoko ya Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuna wakati alilazimika kuzunguka mitaani kukamata wezi wa kazi zake za muziki waliokua wakizidurufu na kuziua bila ya ridhaa yake jambo ambalo ni kinyume na sheria ya hakimiliki. Sugu ambaye pia amekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia mwaka […]

The post Sugu akumbuka alivyopigania hakimiliki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu

Msanii wa miondoko ya Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuna wakati alilazimika kuzunguka mitaani kukamata wezi wa kazi zake za muziki waliokua wakizidurufu na kuziua bila ya ridhaa yake jambo ambalo ni kinyume na sheria ya hakimiliki.

Sugu ambaye pia amekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 alisema kwamba hali hiyo ilitokana na mazingira ya wakati huo na nia ya kulinda kilicho chake.

Katika tukio moja, Sugu alimkamata machinga jijini Dar es Salaam akiuza kaseti zilizokuwa na wimbo wake wa Day Worker lakini baada ya kutafakari alisita kumpeleka polisi kwa alichodai kuwa mtu huyo ni Day Worker yaani anayefanya kazi za kawaida ikiwamo vibarua.

“Achana na hiyo ya chinga, mimi nilishakwenda kwenye duka la mtu mmoja nikamkuta anauza kazi zangu kumuuliza akaniambia yeye ni mfanyabiashara analetewa bidhaa na kuziuza, akanitolea mfano wa mtu anayeuza suruali kwamba analetewa tu na watu aziuze hajui wanaomuuzia bidhaa hizo wanazitoa wapi,’’ alisema Sugu.

Alisema kwamba ni muhimu kwa wasanii kupambana katika kulinda kazi zao na kutolea mfano wa mtu aliyejenga nyumba mahali ambapo kituo cha polisi kiko mbali akisema kwamba mtu huyo ni lazima ajipe jukumu la kulinda mali zake kabla ya kulalamika kwamba polisi wako mbali.

Akizungumzia wingi wa wasanii kwa sasa, Sugu alisema kwamba pamoja na wingi huo lakini kuna tatizo la kukosekana umoja, “tatizo ninaloliona sasa ni ukosefu wa umoja, wasanii hawana umoja.”

Akifafanua kuhusu umoja, Sugu alisema kwamba akiwa bungeni aliwahi kuwasilisha hoja ya kutaka wasanii wa muziki walipwe na vituo vya redio na televisheni kwa kutumia kazi zao lakini hapo hapo akatokea msanii mwingine mkubwa na kumpinga.

 Sugu pia aliizungumzia sheria ya Hakimiliki akishangaa na kuhoji ni  kwa nini masuala yanayohusu hakimiliki yapo Wizara ya Viwanda na BIashara wakati wasanii walio wengi ndio wahusika katika sheria hiyo.

“Hii sheria ilitakiwa kuwa wizara inayohusika na sanaa kwani huko kuna wahusika walio wengi wanaoguswa na mambo ya hakimiliki,’’ alisema Sugu.

The post Sugu akumbuka alivyopigania hakimiliki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/sugu-akumbuka-alivyopigania-hakimiliki/feed/ 0
Kim ataja siri ya Redondo Stars https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/kim-ataja-siri-ya-redondo-stars/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/kim-ataja-siri-ya-redondo-stars/#respond Thu, 11 Nov 2021 10:35:24 +0000 https://greensports.co.tz/?p=415 Na mwandishi wetuKocha wa Taifa Stars, Kim Paulsen amempa nafasi Ramadhan Chombo ‘Redondo’ katika timu ya Taifa kutokana na juhudi za mchezaji huyo na mchango anaoutoa katika timu yake ya Biashara kwenye mechi za Ligi Kuu. Paulsen alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu nafasi ya mchezaji huyo ambaye kabla ya kuitwa Stars baadhi ya mashabiki walikuwa […]

The post Kim ataja siri ya Redondo Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa Taifa Stars, Kim Paulsen amempa nafasi Ramadhan Chombo ‘Redondo’ katika timu ya Taifa kutokana na juhudi za mchezaji huyo na mchango anaoutoa katika timu yake ya Biashara kwenye mechi za Ligi Kuu.

Paulsen alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu nafasi ya mchezaji huyo ambaye kabla ya kuitwa Stars baadhi ya mashabiki walikuwa wakimzungumzia na kutaka apewe nafasi katika timu hiyo ambayo leo (Novemba 11, 2021) inaumana na timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika mechi ya Kundi J kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022.
Akifafanua zaidi Paulsen alisema kwamba ni wachezaji wengi wanaofikiriwa katika timu ya Taifa lakini ni wachache wanaoitwa kujiunga na timu hiyo na kwa Redondo ameonyesha umuhimu wa uzoefu wake katika timu yake lakini zaidi ya hayo ni mchezaji mbunifu.
“Redondo ni mbunifu lakini pia ameonyesha faida ya kuwa mzoefu, kwa kawaida mchezaji anayefanya vizuri akiwa na timu yake katika Ligi Kuu ndiye anayeitwa Stars na kwa Redondo hilo limeonekana wazi,’’ alisema Paulsen.
Akiizungumzia Stars kwa ujumla kabla ya mechi na DRC, Paulsen alisema kwamba wachezaji wote wana ari na wanafurahia kuwa katika familia ya Taifa Stars na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Alisema kwamba wanatambua kuwa wapinzani wao ni timu nzuri yenye wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi na wako katika nafasi ya 65 kwenye viwango vya FIFA lakini dhamira yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri na kuongoza katika kundi lao.
“Tumecheza nao tukapata sare ya bao 1-1, lakini mechi hiyo ya ugenini inabaki kuwa somo ambalo tutalitumia katika mechi ya nyumbani, tunajiamini na tunataka kuwa namba moja katika kundi letu na kuendelea katika hatua nyingine,’’ alisema.
Stars inaongoza kundi lake ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Benin ambayo pia ina pointi saba lakini zinatofautana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, DRC ni ya tatu ikiwa na pointi tano wakati Madagascar inashika mkia ikiwa na pointi tatu huku timu zote zikiwa zimecheza mechi nne.
Paulsen pia alikataa kuzungumzia mbinu ambazo anatarajia kuzitumia katika mechi na DRC baada ya kuulizwa na mwandishi mmoja wa DRC aliyesema kwamba katika mechi ya kwanza Stars walicheza kwa kuwasoma zaidi DRC na kujihami, akitaka kujua kama Paulsen leo atatumia mbinu hiyo au la
“Kila mechi ina mbinu zake lakini kwa sasa sitoweza kukwambia mbinu nitakayoitumia, nitaweza kufanya hivyo baada ya mechi,’’ alisema Paulsen.
Paulsen pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadhamini wa Stars, serikali na mashabiki ambao aliwataka waendelee kuwaunga mkono katika mechi ya leo.
Naye nahodha wa Stars, John Bocco alisema wako tayari kwa ajili ya mechi ya leo, wanawaheshimu DRC na akawataka mashabiki kuwaombea ili wafanye vizuri.

The post Kim ataja siri ya Redondo Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/11/kim-ataja-siri-ya-redondo-stars/feed/ 0
Kardashians, warembo wanaopiga pesa kwenye urembo https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/familia-ya-warembo-inayopiga-pesa-kwenye-urembo/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/familia-ya-warembo-inayopiga-pesa-kwenye-urembo/#respond Wed, 10 Nov 2021 15:00:51 +0000 https://greensports.co.tz/?p=392 New York, MarekaniMwaka 1978, mwanasheria Robert Kardashian alifunga ndoa na Kris au Jenner na kupata watoto wanne; Kourtney, Kimberly au Kim, Khloe na Rob. Ndoa hiyo ilivunjika mwaka 1991 na Robert alifariki mwaka 2003.Robert alipata umaarufu mwaka 1994 na 1995 alipomtetea, O.J Simpson hadi kushinda kesi ya mauaji iliyokuwa mjadala sehemu mbalimbali duniani. Simpson, Mmarekani […]

The post Kardashians, warembo wanaopiga pesa kwenye urembo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Mwaka 1978, mwanasheria Robert Kardashian alifunga ndoa na Kris au Jenner na kupata watoto wanne; Kourtney, Kimberly au Kim, Khloe na Rob. Ndoa hiyo ilivunjika mwaka 1991 na Robert alifariki mwaka 2003.
Robert alipata umaarufu mwaka 1994 na 1995 alipomtetea, O.J Simpson hadi kushinda kesi ya mauaji iliyokuwa mjadala sehemu mbalimbali duniani. Simpson, Mmarekani mwenye asili ya Afrika alidaiwa kumuua aliyekuwa mkewe, Nicole Brown ambaye ni mzungu miaka miwili baada ya kutalikiana.
Leo hii ukiizungumzia familia ya Kardashian huhitaji tena kumtaja Robert, utawazungumzia wanadada warembo wafanyabiashara matajiri ambao wameutumia vizuri urembo wao kupiga pesa kupitia uanamitindo, mauzo na maonyesho ya mavazi, vipindi vya televisheni hadi kutoa kitabu cha Kardashian Konfidential cha mwaka 2010.

Kourtney (42)
Kourtney ni mwanamitindo na mshiriki wa vipindi vya televisheni akishiriki kipindi maarufu cha familia hiyo cha Keeping Up with Kardashians na vipindi vingine vya Kourtney and Khloe Take Miami na Kourtney and Kim Take New York ambavyo ni kama mwendelezo wa Keeping Up with Kardashians.
Kourtney na ndugu zake pia wamekuwa wakiuza mavazi ya aina mbalimbali pamoja na manukato huku wakinufaika kupitia mitandao ya Facebook, Twitter na Instagram kwa kujiingizia pesa kwa kila ‘post’. Kourtney aliwahi kutajwa kupata dola 75,000 hadi 200,000 kupitia mitandao ya Facebook na Twitter.
Kwenye mahusiano, Kourtney aliwahi kuwa mpenzi wa Scott Disick kati ya mwaka 2005 hadi 2015 na a kupata watoto watatu, baada ya hapo akawa na mwanamitindo, Younes Bendjima kati ya mwaka 2017 na 2018.
Mapema mwaka huu zimekuwapo habari kwamba Kourtney anatoka na mwanamuziki Travis Barker na wawili hao inadaiwa huenda wakafunga ndoa wakati wowote.


Kim (40)
Kama dada yake Kourtney, Kim alianza kupata umaarufu akiwa rafiki wa mwanamitindo Paris Hilton, baadaye akawa gumzo zaidi baada ya mkanda wake wa ngono na aliyekuwa mpenzi wake, Ray J kuzagaa mitandaoni mwaka 2007. Ni wakati huo huo alishiriki vizuri na kukipa umaarufu zaidi kipindi cha Keeping Up with Kardashians.
Kwa warembo wa familia ya Kardashian, Kim amepiga pesa za maana, mbali na vipindi vya televisheni ana biashara za mavazi na manukato na mwaka 2017 alianzisha kampuni za biashara ya urembo, mitindo na manukato za KKW Beauty na KKW Fragrance hiyo ni mbali na mamilioni ya wafuasi wanaomfuatiia kwenye mitandao hasa ya Twitter na Instagram na kumfanya alipwe fedha kibao.
Mwaka 2015 jarida la Time, lilimtaja katika orodha ya wanawake 100 maarufu huku akitajwa kuwa mshiriki wa kwenye vipindi vya televisheni mwenye malipo makubwa akidaiwa katika mwaka huo pato lake lilifikia Dola 53 milioni.
Kim alifunga ndoa mwaka 2000 na Damon Thomas, msanii wa R&B lakini ndoa ilivunjika mwaka 2004, mwaka 2011 akaolewa na Kris Humphries nyota wa mpira wa kikapu katika ligi ya NBA, Marekani lakini ndoa hiyo ilivunjika mwaka 2013 huku ikidaiwa kuwa ndoa hiyo ilikuwa ni mpango maalum wa Kim kujiongezea umaarufu na kujiimarisha zaidi kibiashara ingawa Kim alipinga.
Mwaka 2014 akaangukia kwa rapa Kanye West, ndoa iliyokuwa maarufu kwa namna vyombo vya habari vilivyokuwa vikiwakifuatiliwa kila kona huku Kim akiitwa kwa jina la Kim Kardashian West. Kim na Kanye wana watoto wanne lakini Septemba mwaka huu ndoa yao kama ile ya Kourtney nayo iliota mbawa.

Khloe (37)
Ni mrembo aliyefuata nyayo za dada zake, kwenye mitindo yumo na hajajiweka kando kwenye televisheni, ushiriki wake katika Keeping Up with Kardashians unachangia kumuweka juu.
Mwaka 2016 alijiongeza zaidi kwa kuanzisha kipindi cha televisheni cha Kocktails with Khloe pamoja na kipindi kingine cha mambo ya afya na mazoezi cha Revenge Body with Khloé Kardashian.
Khloe, pia anafanya biashara ya manukato, mwaka 2011 yeye na aliyekuwa mumewe walitangaza kuuza manukato ya wanawake na wanaume waliyoyapa jina la Unbreakable na mwaka 2012 wakaja na manukato mengine waliyoyapa jina la Unbreakable Joy.
Mwaka 2008, Khloe alitajwa kuwa katika mapenzi na nyota wa mpira wa kikapu wa klabu ya Los Angeles Lakers, Rashad McCants lakini miezi saba baadaye walitengana na akahamia kwa nyota mwingine wa kikapu, Lamar Odom waliyefunga naye ndoa Septemba 2009 na Khloe kuitwa Khloe Kardashian Odom lakini ndoa hiyo nayo iliota mbawa mwaka 2016.


Rob (34)
Kaka pekee mwenye dada watatu, hajajiweka nyuma katika kusafiria nyota ya dada zake, Rob ni mshiriki mzuri wa Keeping Up with Kardashians, jina lake lilikuwa mjadala mitandaoni mwaka 2016 alipoanza mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo, Blac Chyna na kupata mtoto wa kike waliyempa jina la Dreem Renee aliyezaliwa Novemba 2016, lakini mwezi mmoja tu baada Dreem kuzaliwa wawili hao waliachana.
Rob pia ana dada wengine wawili, Kendall na Kylie ambao ni wa baba mwingine, nao wamefuata nyayo za Kardashian Family kwa kuutumia urembo kupiga pesa.


Kendall Jenner (26)
Kendall ni mwanamitindo, mfanyabiashara na mshiriki mzuri wa vipindi vya televisheni, alianza kupata umaarufu kupitia Keeping Up with the Kardashians na kwenye maonyesho ya mitindo ya Paris, Milan na New York.
Mwaka 2017 jarida la Forbes lilimtaja Kendall kuwa ni mwanamitindo anayelipwa fedha nyingi zaidi akimpiku, Gisele Bündchen ambaye amekuwa akitamba kwa zaidi ya miaka 10. Kendall kwa sasa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na nyota wa mpira wa kikapu wa NBA, Devin Booker.

Kylie Jenner (24)
Ni mwanamitindo, mfanyabiashara na mshiriki wa vipindi vya televisheni, alipata umaarufu kupitia kipindi cha E! reality ambacho ni sehemu ya Keeping Up with the Kardashians, pia ni mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, anatajwa kuwa mwanamke mwenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram akiwa na umri mdogo.
Katika mauzo ya mavazi ameshirikiana vyema na dada yake kupitia kampuni yao ya Kendall & Kylie na mwaka 2015 alizindua aina ya vipozozi vyake alivyovipa jina la Kylie Lip Kits na baadaye kubadili jina hilo na kuwa Kylie Cosmetics.
Kati ya mwaka 2014 na 2015, jarida la Time lilimtaja yeye na Kendall kuwa ni wasichana wa umri mdogo maarufu duniani kwa kuangalia nguvu yao kwenye mitandao ya kijamii.
Mwaka 2019 Forbes lilimtaja Kylie kuwa na pato linalofikia dola bilioni 1 na kumfanya awe msichana aliyepambana kufikia hadhi ya ubilionea akiwa mdogo, wakati huo alikuwa na miaka 21.
Hata hivyo hoja ya kwamba amepambana hadi kuwa bilionea imekuwa ikipingwa na wale wanaoamini kuwa utajiri wake umebebwa na umaarufu wa familia huku akilaumiwa kuwa japo ni tajiri mwenye pesa lakini baadhi ya taarifa zake zinakuzwa ili kumpaisha zaidi.
KKylie aliwahi kuwa mpenzi wa rapa Tyga yaani mpenzi wa zamani wa Blac ambaye pia alikuwa mpenzi wa Rob, kaka yake Kylie, aliwahi kuonekana kwenye video za nyimbo za Tyga za Stimulated na aka Dope’d Uppen.
Kuanzia mwaka 2017, Kylie amekuwa akionekana na mwanamuziki Travis Scott na alionekana katika video ya wimbo wa Scott wa Stop Trying to Be God na hadi sasa wana mtoto mmoja wa kike aitwaye, Stormi Webster.

The post Kardashians, warembo wanaopiga pesa kwenye urembo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/familia-ya-warembo-inayopiga-pesa-kwenye-urembo/feed/ 0
J.Lo, Ben Affleck ‘Super Couple’ iliyorudi baada ya miaka 17 https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/j-lo-ben-affleck-super-couple-iliyorudi-baada-ya-miaka-17/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/j-lo-ben-affleck-super-couple-iliyorudi-baada-ya-miaka-17/#respond Wed, 10 Nov 2021 14:43:05 +0000 https://greensports.co.tz/?p=386 NEW YORK, MAREKANIMwaka 2002 staa wa filamu Ben Affleck na mwanamuziki Jeniffer Lopez au J.Lo walikuwa gumzo duniani hadi kubatizwa jina la Super Couple na baadaye Bennifer ikiwa ni ufupisho wa majina yao .Kila walipokwenda, kila walichofanya kilikuwa habari na haikushangaza kuwakuta kila mara wakiwa kwenye vyombo vya habari na kuwa gumzo duniani kote. Ukweli […]

The post J.Lo, Ben Affleck ‘Super Couple’ iliyorudi baada ya miaka 17 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

NEW YORK, MAREKANI
Mwaka 2002 staa wa filamu Ben Affleck na mwanamuziki Jeniffer Lopez au J.Lo walikuwa gumzo duniani hadi kubatizwa jina la Super Couple na baadaye Bennifer ikiwa ni ufupisho wa majina yao .
Kila walipokwenda, kila walichofanya kilikuwa habari na haikushangaza kuwakuta kila mara wakiwa kwenye vyombo vya habari na kuwa gumzo duniani kote. Ukweli ni kwamba wawili hawa walikuwa kivutio na waliteka hisia za wapenzi wa filamu, muziki na wengineo waliopenda kusikia habari zao.
Hata hivyo kumulikwa kwa mambo yao na vyombo vya habari kukageuka kero na ikatosha kuwa sababu ya kuachana kwao na kuwaacha vinywa wazi mashabiki wao waliokuwa wakiisubiri kwa hamu ndoa ya ma-Super Couple hawa ambayo tayari ilianza kunukia.
Ndoa hiyo iliyopangwa kufungwa Septemba 14, 2003 iliota mbawa kwa taarifa iliyotolewa siku nne kabla ya tukio hilo sababu ikielezwa kuwa ni kukerwa na namna ambavyo vyombo vya habari vilikuwa vikiwanyima utulivu kwa kuyashupalia mambo yao na kila sehemu waliyokwenda.


J.Lo ambaye pia ameigiza filamu kadhaa, alikiri kwamba kuachana na Ben Affleck ni tukio la kwanza kubwa lililomuumiza mno moyo.
Baada ya kuachana, Affleck alianza kutoka na rafiki yake wa zamani, Jennifer Garner na kufunga naye ndoa mwaka 2005, ndoa iliyobarikiwa watoto watatu lakini wawili hao waliachana mwaka 2018.
J.Lo naye alirudiana na mpenzi wake wa zamani, Marc Anthony na kufunga naye ndoa Juni 2004 na mwaka 2008, J.Lo alijifungua watoto wawili mapacha, Maximilian David na Emme Maribel lakini ndoa yake na Marc nayo ilivunjika mwaka 2011.
Julai mwaka huu, J.Lo alithibitisha kile alichokisema mwaka 2004 kwamba kuachana na Affleck kulimuumiza mno moyo na hatimaye sasa amekiri kurudiana naye baada ya uvumi kuenea mapema mwaka huu kwamba Super Couple iliyotingisha 2002 hadi 2004 inatudi tena.
Wakati wanaachama mwaka 2004, Affleck ndio kwanza alikuwa mkaka wa miaka 32 wakati J.Lo alikuwa mdada wa miaka, 35 leo hii wanarudiana Affleck ni mtu mzima mwenye miaka 49 wakati J.Lo ni mama wa miaka 52.

The post J.Lo, Ben Affleck ‘Super Couple’ iliyorudi baada ya miaka 17 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/j-lo-ben-affleck-super-couple-iliyorudi-baada-ya-miaka-17/feed/ 0
Abhi & Pragya wanavyoinogesha Twist of Fate https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/abhi-pragy-wanavyoinogesha-twist-of-fate/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/abhi-pragy-wanavyoinogesha-twist-of-fate/#respond Wed, 10 Nov 2021 14:37:12 +0000 https://greensports.co.tz/?p=383 NEW DELHI, INDIAUnaweza kuwa mpenzi wa filamu za Bollywood lakini usijue chochote kuhusu Shabir Ahluwalia lakini ukitajiwa jina la Abhishek Mehra au Abhi hapo akili itaelekea katika filamu mbalimbali ikiwamo Twist of Fate.Ni hivyo hivyo kwa mrembo Sriti Jha si ajabu usimjue lakini ukitajiwa jina la Pragya akili pia itakwenda katika filamu alizoigiza mojawapo ikiwa […]

The post Abhi & Pragya wanavyoinogesha Twist of Fate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

NEW DELHI, INDIA
Unaweza kuwa mpenzi wa filamu za Bollywood lakini usijue chochote kuhusu Shabir Ahluwalia lakini ukitajiwa jina la Abhishek Mehra au Abhi hapo akili itaelekea katika filamu mbalimbali ikiwamo Twist of Fate.
Ni hivyo hivyo kwa mrembo Sriti Jha si ajabu usimjue lakini ukitajiwa jina la Pragya akili pia itakwenda katika filamu alizoigiza mojawapo ikiwa Twist of Fate.
Katika Twist of Fate, Abhi, mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu ameigiza na Sriti au Pragya, mwanamke muungwana asiye na makuu, wameuvaa vizuri uhusika wa wapenzi walioshibana ambao misukosuko ya hapa na pale inafanikiwa kuwavuruga na kuwatenganisha lakini si kwa mmojawapo kumtoa moja kwa moja mwenzake moyoni.
Na hilo linathibitishwa na namna ambavyo kila mmoja anavyojiwa na mawazo ya mwenzake anapokuwa katika tafakari za mambo mbalimbali ya maisha, iwe mchana au hata usiku.
Katika filamu hii, Abhi na Pragya wanaubeba kisawasawa ule usemi wa wahenga kwamba ‘uliyemtia moyoni kumtoa kazi.’
Tukio kubwa la kutengana kwao linawafikisha katika hatua ya kugawana watoto wao wawili wa pekee mapacha wa kike, Prachi na Ria.
Prachi analelewa na mama yake na kuishi maisha ya watu wa kipato cha kawaida yanayoambatana na maadili mema wakati mwenzake Ria akilelewa kama yai na baba yake na kuishi maisha ya kifahari katika jiji la New Delhi, akionekana mtoto pekee wa mwanamuziki maarufu na tajiri.
Watoto hawa baadaye wanajikuta wakiwa pamoja chuo kikuu mjini Delhi ingawa hawajuani, hapo kila mmoja anatoa tafsiri ya aina ya malezi aliyopata, Prachi msichana mwenye maadili na anayeishi maisha ya kawaida wakati ndugu yake Ria anaishi kitajiri, kwenda chuo na gari, kudharau wanafunzi wanaotoka familia za kipato cha kawaida na kuonyesha dalili zote za kuwapo tatizo katika malezi aliyopata.
Kutengana huku na mivutano ya hapa na pale inasababisha Abhi kuchukua uamuzi mgumu wa kuoa mke mwingine, Pragya akiwa naye amehamia jijini Delhi anaumizwa na uamuzi huo, anapambana kuzuia mumewe asifunge ndoa nyingine jambo ambalo linafanikiwa huku Abhi naye akimuunga mkono kudhihirisha namna ambavyo Pragya bado yuko moyoni mwake.
Hapo hapo watoto wao Ria na Prachi wakiwa hawajuani wanajikuta katika mvutano wa kumgombea Ranbir, kijana anayetoka familia ya kitajiri ambayo ni familia rafiki ya Abhi.
Wakati Ria akijiaminisha kwamba yeye ndiye mtu sahihi wa kuwa mpenzi wa Ranbir hasa kwa kuwa ni marafiki wa utotoni, wote wanatoka familia rafiki na za kitajiri, hali ni tofauti kwa Ranbir kwani haoni hasikii kwa Prachi.
Kwa ambao wameifuatilia filamu hii kupitia Zee World wanaweza kudhani kwamba Abhi na Pragya ni wapenzi wa kweli hata nje ya filamu, ukweli ni kwamba Abhi ambaye kwa sasa ana miaka 42 ni mume wa Kanchi Kaul, staa mwingine wa filamu na walifunga ndoa mwaka 2011 na hadi sasa wana watoto wawili wa kiume.

The post Abhi & Pragya wanavyoinogesha Twist of Fate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/abhi-pragy-wanavyoinogesha-twist-of-fate/feed/ 0
Bellerin, staa wa Arsenal mwanamazingira https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/bellerin-staa-wa-arsenal-mwanamazingira/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/bellerin-staa-wa-arsenal-mwanamazingira/#respond Wed, 10 Nov 2021 14:17:52 +0000 https://greensports.co.tz/?p=378 Barcelona, HispaniaStaa wa Arsenal, Hector Bellerin anakumbuka vizuri utamaduni wa kutunza mazingira aliojifunza kwa babu yake tangu akiwa mtoto mdogo katika viunga vya jiji la Barcelona. Katika kuuendeleza utamaduni huo, Bellerin ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Real Betis ya Hispania, anaendesha kampeni ya upandaji miti lengo likiwa ni kupendezesha na kusaidia […]

The post Bellerin, staa wa Arsenal mwanamazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Staa wa Arsenal, Hector Bellerin anakumbuka vizuri utamaduni wa kutunza mazingira aliojifunza kwa babu yake tangu akiwa mtoto mdogo katika viunga vya jiji la Barcelona.

Katika kuuendeleza utamaduni huo, Bellerin ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Real Betis ya Hispania, anaendesha kampeni ya upandaji miti lengo likiwa ni kupendezesha na kusaidia utunzaji na uhifadhi wa mazingira duniani.

“Nikiwa mdogo niliishi na babu yangu Barcelona, nilikuwa nakwenda naye kwenye bustani yake na huko tulipanda miti na kucheza kwenye pori dogo, kwa hiyo hili ni jambo linalougusa moyo wangu,” alisema Bellerin katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya.

Wakati Ligi Kuu England msimu wa 2019/20 ikiwa imesimama Machi mwaka jana kutokana na janga la Corona, mbali na juhudi za kujiweka fiti, Bellerin pia alitumia muda huo kuendeleza harakati zake za upandaji miti na utunzaji mazingira jambo ambalo analifanya kutokana na mapenzi aliyonayo katika jambo hilo.

Katika kuifanyia kazi kampeni hiyo, Bellerin aliahidi kupanda miti 3,000 kwa kila mechi ambayo klabu yake ya Arsenal ingeibuka na ushindi katika mechi zilizobaki za msimu huo.

Bellerin pia amekuwa akiwahimiza wachezaji wenzake kusaidia katika kampeni za utunzaji mazingira na upandaji miti, “Ni jambo zuri kujivunia kwa kile tulichonacho, iwe ni magari yetu, saa za bei mbaya lakini pia ni muhimu kuwasilisha ujumbe wenye maana, angalia katika hilo tuko kimya,” alisema Bellerin katika moja ya mahojiano.

Septemba mwaka jana, Bellerín alitangazwa kuwa mwanahisa wa pili kuwa na hisa nyingi katika klabu ya Forest Green Rovers ya England inayoshiriki ligi ya EFL (League II) , aliipongeza klabu hiyo kwa kampeni yake ya kuhimiza ulaji mboga na matunda (veganism) na kampeni za utunzaji mazingira.

Bellerin ambaye mwaka 2017, alianza kuwa mlaji wa mboga na matunda (vegan) jambo ambalo anasema limemsaidia kuimarisha afya yake, moja ya mikakati yake kwa sasa ni kushiriki kupanda miti katika msitu maarufu wa Amazon (Mapafu ya Dunia) ambao kwa sehemu kubwa upo nchini Brazil. Katika hilo, Bellerin anashirikiana na taasisi ya One Tree Planted.

The post Bellerin, staa wa Arsenal mwanamazingira first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/bellerin-staa-wa-arsenal-mwanamazingira/feed/ 0
Mtambo wa Gongo ampa somo Dula Mbabe https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/mtambo-ya-gongo-ampa-somo-dula-mbabe/ https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/mtambo-ya-gongo-ampa-somo-dula-mbabe/#respond Wed, 10 Nov 2021 13:52:53 +0000 https://greensports.co.tz/?p=368 *Amkumbuka Matumla Jina la Dula Mbabe ni maarufu katika ngumi hasa anapohusishwa na mpinzani wake Twaha Kiduku, awali baadhi ya mashabiki walianza kuuhusisha upinzani wao kama ule wa Rashid Matumla au Snake Boy na Maneno Oswald au Mtambo wa Gongo. Ni kwa bahati mbaya mjadala wa Dula Mbabe kwa sasa umekuwa ukihusisha zaidi vipigo anavyovipata […]

The post Mtambo wa Gongo ampa somo Dula Mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
*Amkumbuka Matumla

Jina la Dula Mbabe ni maarufu katika ngumi hasa anapohusishwa na mpinzani wake Twaha Kiduku, awali baadhi ya mashabiki walianza kuuhusisha upinzani wao kama ule wa Rashid Matumla au Snake Boy na Maneno Oswald au Mtambo wa Gongo.

Ni kwa bahati mbaya mjadala wa Dula Mbabe kwa sasa umekuwa ukihusisha zaidi vipigo anavyovipata na hivyo kuanza taratibu kufuta matarajio ya kuwapo upinzani mkali kati yake na Kiduku kama ule wa Snake Boy na Mtambo wa Gongo.

Maneno Oswald au Mtambo wa Gongo.

Na ingawa majigambo ya Dula Mbabe kabla ya pambano yamekuwa yakiwapa mashabiki wake matumaini makubwa ya ushindi lakini hali imekuwa tofauti kwani amekuwa akishindwa kutamba.

Kashindwa kutamba kwa Kiduku, ikajengeka dhana kwamba Kiduku alibebwa lakini kushindwa katika pambano lake la mwisho dhidi ya bondiaTshimanga Kantompa kutoka DR Congo, kumeibua mapya, wako wanaomtaka aachane na jina la Mbabe, aitwe tu kwa jina lake la Abdallah Pazi lakini wapo wanaomtaka astaafu ngumi, hoja ambayo imemuibia Mtambo wa Gongo.

“Hapana, si sahihi Dula Mbabe bado mdogo kwenye ngumi wazo la kustaafu ngumi si zuri badala yake ni vyema akae na kujiuliza kulikoni anapigwa vipigo mfululizo,’’ anasema Maneno katika mazungumzo yake hivi karibuni na Green Sports.

“Wanaotaka Mbabe astaafu ngumi watambue kwamba ngumi ni kazi na kama Mbabe ameichagua ngumi kuwa kazi yake kumtaka astaafu mapema ni kumnyima fursa ya kupata kipato,’’ anafafanua.

Maneno anasema kwamba anachotakiwa kufanya Mbabe nikubadili staili ya upiganaji, inawezekana wapinzani wake wameshamsoma, wanajua udhaifu wake hivyo wanautumia kumpiga.

Akifafanua zaidi Maneno anasema kuna wakati kipigo hakiepukiki kwa kila bondia lakini unapopigwa mfululizo hata mashabiki wako unawakatisha tamaa hivyo ni muhimu kujiuliza kulikoni.

Akitolea mfano pambano la Mbabe na bondia kutoka DR Congo, Maneno anasema, Mbabe alianza kupigwa kuanzia raundi ya kwanza na hakuona ngumi yoyote ya maana kutoka kwa bondia huyo na hata sare aliyotoka na Kiduku ameonyesha udhaifu, aitumie ile na mapambano mengine aliyopigwa katika maandalizi yake.

Maneno pia alieleza kushangazwa kwake na aina ya ngumi zinazomuangusha Mbabe, “ngumi inayotokea pembeni mara nyingi haina nguvu sana kama ile ya moja kwa moja, sasa Mbabe amekuwa akiangushwa kwa ngumi zinazotokea pembeni si zile za mbele moja kwa moja, hili nalo ni jambo analotakiwa kulifanyia kazi na kujiuliza tatizo ni nini hasa.”

“Mbabe pia naona kama anatumia nguvu nyingi, hawasomi wapinzani wake, ni vizuri kumsoma mpinzani badala ya kutumia nguvu nyingi, kuna mpinzani unapotumia nguvu nyingi unakuwa umemrahisishia kazi kwani atakuwa anakuzungusha tu ulingoni na kuzidi kukuchosha kabla ya kukupiga ngumi za pointi.

Mtambo wa Gongo kushoto) akiwa na Rashid Matumla

Katika hilo Maneno anamtaja Matumla akidai kuwa kuna wakati alikuwa kama anamzungusha mpinzani ulingoni na hapo ukiwa mwenye kutumia nguvu utachoka na mwisho kushindwa pambano.

Maneno pia alimtaka Mbabe kupunguza mapambano ya mara kwa mara, “kweli kuna kuhitaji pesa lakini mapumziko nayo yana umuhimu wake katika kujiandaa na pambano jingine, na hapa bila shaka pambano lake na bondia wa DR Congo limethibitisha hilo.

Kuhusu majigambo ya Mbabe, Maneno anasema hilo haliepukiki kwani bondia hawezi kuingia ulingoni kinyonge, amekubali kupigana maana yake ni kwamba anajiamini hivyo ni lazima ajigambe atakapoulizwa, na si sahihi kuwa mnyonge kabla ya pambano au kuonyesha kwamba utapigwa.

Hata hivyo, Maneno anatahadharisha kwamba hiyo haina maana ya kulewa sifa, “sina maana kwamba bondia huyo alewe sifa na kujiamini kupita kiasi kwamba lazima atashinda pambano, hapana ni lazima kuchukua tahadhari, kujiandaa vizuri na kutomdharau mpinzani wako lakini inapotokea ukaulizwa kabla ya pambano ni lazima useme kwa kujiamini na kwamba utashinda.

Upinzani na Matumla

Akizungumzia upinzani wake na Matumla, Maneno anasema kwamba wakati ule ilikuwa kama Simba na Yanga kwenye soka, yeye akitajwa kuwa Yanga na Matumla Simba

Anasema kwamba hali ile haikuwa ulingoni tu bali hata mitaani kwao kwenye vitongoji vya Keko jijini Dar es Salaam, “iwe Keko Machungwa, Keko Akida na kwingineko hadithi kubwa jioni baada ya pambano ilituhusu mimi na Rashidi (Matumla),’’ anasema.

Akimzungumzia Matumla, Maneno anasema alikuwa bondia bora na mpinzani wake waliyechoshana,  hapohapo anayakumbuka mapambano yao mawili yaliyopigwa miaka ya 2000 mwanzoni kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere zamani PTA.

Katika mapambano hayo, Maneno alimpiga Matumla katika pambano moja akapigwa katika pambano la pili. “Unajua unapocheza na bondia bora kila mtu anaamini utapigwa sasa mimi nilipompiga Matumla ikawa habari kubwa, kama unavyojua haikuishia ulingoni tu bali hata katika mitaa ya Keko mashabiki wangu walikuwa wakijivunia.

Akizungumzia siku aliyopigwa, Maneno anakiri kwamba ushindi wa pambano lao la kwanza ulimfanya alewe sifa na kujiona ana uwezo wa kumpiga Matumla hasa kwa kuwa watu walimsifia sana, “nilikuwa nasifiwa kila siku, na hiyo ni kwa sababu nilimpiga bondia bora.

Zaidi ya hilo, Maneno anasema kwamba alicheza akiwa anaumwa mkono na licha ya daktari wake kuhangaika na kumpatia tiba iliyomsaidia kujiona yuko vizuri lakini akiwa ulingoni baada ya kurushiana ngumi na mpinzani wake, mkono ulianza kuuma tena. “kama unavyojua nilikuwa na ngumi nzito lakini siku ile nacheza na Rashid (Matumla) hali ilikuwa tofauti, mkono ulinisumbua ingawa nilichomwa sindano lakini baadaye hali haikuwa nzurilakini pia nililewa sifa.

Tofauti na hali hiyo, Maneno anasema mapambano yake na Matumla yanabaki kwenye kumbukumbu zake kwa kuwa ndio mapambano pekee ambayo walau anaweza kusema yalimpa kipato cha kumfurahisha tofauti na mengine.

“Nimecheza ngumi muda mrefu tangu miaka ya 1990 lakini ni mapambano yangu na Matumla tu ambayo nilipata kati ya shilingi milioni mbili hadi tatu, hiyo ni baada ya kutoa pesa za wasaidizi wangu katika mazoezi na gharama nyingine za maandalizi,’’ anasema.

Maneno pia anasema kwamba nje ya pesa hizo ambazo hutolewa na pomota kuna pesa nyingine kutoka kwa mashabiki ambazo hazihusiani na zile za promota.

Akifafanua anasema baada ya kumpiga Matumla kuna mashabiki walikuwa wakimuita kwenye maofisi yao na kumpa pesa, “unaitwa halafu unakabidhiwa bahasha ndani ina shilingi 200,000 au 300,000, na kupongezwa kwa ushindi dhidi ya Matumla.”

Nje ya mapambano yake na Matumla, Maneno anasema katika mapambano mengine hakuwahi kupata zaidi ya shilingi 500,000 na mara nyingi ilikuwa ni chini ya 500,000.

Akizungumzia ngumi enzi zao, Maneno anasema mabondia waliibiwa sana na mapromota lakini pia ngumi za kulipwa zilitawaliwa na migogoro ya mara kwa mara, kila mtu alijiona ana haki ya kusimamia ngumi.

Anasema jambo hilo kwa kiasi fulani lilichangia mabondia kudhulumiwa kwani hakukuwa na sauti moja ya kuwasimamia, “unaenda nje ya nchi kupigana unaambiwa thamani ya pambano lako ni dola 20,000 kwa mfano lakini hadi unarudi Tanzania mfukoni una dola 1,000 tu au hata pungufu ya hiyo.”

“Wakati mwingine unaenda hata mkataba wako hujauona, unaishia kwenye ufahari wa kupanda ndege na kulala hoteli ya hadhi ya juu nje ya nchi, kwa kweli kipindi kile tulidhulumiwa sana, ukitaka kujua hilo muangalie Matumla, kapeperusha bendera ya Taifa nje, kapewa heshima hadi kwenda Ikulu lakini hali yake kwa sasa haitoi dalili zozote za bondia bora wa zamani.

Pamoja na madhila yote hayo waliyofanyiwa, Maneno anashukuru kwani yote yaliyowapata yamekuwa kama somo lenye maana kwani kwa sasa hali ni tofauti, sisi ni kama tulizitoa ngumi gizani kwani kwa sasa kuna kila ishara ya kuwapo mwanga.

Maneno anashauri mabondia wa zamani wakumbukwe na kuthaminiwa na Serikali kwa hilo lakini pia washirikishwe katika mambo mbalimbali yanayohusu ngumi nchini.

Kuhusu anachojivunia kwenye ngumi Maneno anasema bila kupepesa macho, “Bila kukuficha sina la kujivunia zaidi ya kujulikana, kweli nimejenga kibanda changu Kongowe lakini ukiniuliza la kujivunia nitakwambia ni kujulikana tu, ukipita mitaani utasikia Mtambo wa Gongo huyo au ukiwa na jambo lako utapata urahisi, ni hilo tu.

Nini ushauri wake kwa mabondia wanaochipukia? Hapo Maneno anawapa tahadhari, “wasijiingize kwenye ngumi kwa ajili ya kushiriki kwenye matukio ya kihalifu, tunawajua wengi sipendi kuwataja kwa majina ambao ngumi wamezitumia kushiriki uhalifu ikiwamo ujambazi na ubabe mitaani lakini wameuliwa hivi hivi, kwa hiyo na hawa mabondia watambue kwamba ngumi ni kama ilivyo soka, ni ajira kuna ambao wameneemeka kwa kupata ajira kupitia kwenye ngumi, wako askari polisi, magereza na wengineo.’’

The post Mtambo wa Gongo ampa somo Dula Mbabe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/11/10/mtambo-ya-gongo-ampa-somo-dula-mbabe/feed/ 0